Ugoigoi wa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugoigoi wa watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by leroy, May 9, 2012.

 1. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60
  Kutoka Gazeti la Habari Leo.

  KENYA imetajwa kunufaika zaidi na Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hivyo kujipatia fedha nyingi za kigeni kutokana na kuuza nje bidhaa zinazotokana na malighafi inayozalishwa Tanzania ambayo inasuasua katika kutumia fursa zinazotokana na soko hilo.

  Hayo yamebainika jana Dar es Salaam wakati Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alipozindua Kamati ya Kitaifa ya kusimamia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la EAC.

  Sitta alisema Tanzania iko nyuma katika kutumia fursa zinazotokana na soko hilo, na kuitaka kamati hiyo ambayo wajumbe wake ni makatibu wakuu na wakuu wa taasisi mbalimbali za Serikali kuhakikisha Watanzania wanawezeshwa kutumia fursa hizo vema.

  Akitolea mfano namna Kenya inavyofaidika na Soko hilo la Pamoja, Waziri Sitta alisema machungwa mengi yanayozalishwa Muheza mkoani Tanga yanakwenda kuuzwa Kenya ambako wao hutengeneza juisi na kuisindika na kisha kuuza nchi za Mashariki ya Mbali na kujipatia fedha nyingi za kigeni.

  Mbali na kunufaika na machungwa kutoka Tanzania, nchi hiyo jirani pia imekuwa ikinufaika na mifugo kwani imebainika kuwa asilimia 80 ya nyama ya ng’ombe inayosindikwa Kenya na kuuzwa nje, inatokana na ng’ombe waliouzwa Kenya na wafugaji wa Kitanzania, tena kwa bei nafuu.

  “Wenzetu Wakenya wana benki yao ya KCB hapa nchini na ambayo sasa tunaelezwa kuwa tayari ina matawi takribani 13 katika taifa jipya la Sudan Kusini, lakini sisi kutokana na sera, benki zetu haziwezi kufanya hayo, hivyo tunashindwa kunufaika na biashara hiyo,” alisema Sitta.

  Changamoto nyingine iliyoelezwa kuwa kikwazo cha utekelezaji wa soko hilo ni nchi wanachama kuchelewa kukamilisha zoezi la kuhuisha sheria zinazosimamia utekelezaji wa Itifaki ya soko la pamoja katika nchi zao.

  Kamati hiyo ya kitaifa ya kusimamia utekelezaji wa Itifaki wa Soko la Pamoja la EAC inaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stagomena Tax na wajumbe wengine wanatoka wizara za Fedha, Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mambo ya Ndani ya Nchi, Viwanda na Biashara, Tume ya Mipango katika Ofisi ya Rais, Idara ya Uhamiaji, Benki Kuu, Ofisi ya Takwimu na ile ya Mwanasheria Mkuu.

  Wajumbe wengine wanatoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Chama cha Wenye Viwanda, Biashara na Kilimo (TCCIA), baadhi ya majukumu ya kamati hiyo ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo mbalimbali yaliyofikiwa na nchi wanachama kabla ya kukamilika kwa Itifaki ya Soko la Pamoja.

  Sitta aliongeza kuw,a mbali na kushindwa kwa Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotokana na Soko hilo la Pamoja, pia sera ya nchi ambayo haiwaruhusu Watanzania kukopesha nje au kuwekeza mitaji nje ya nchi imekuwa ikiwafanya Watanzania washindwe kunufaika fursa mbalimbali za kibiashara za jumuiya
   
 2. M

  Michael Mwakyusa JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
   
 3. M

  Michael Mwakyusa JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu ugoigoi ni matokeo ya uongozi wa kimagamba wa nchi yetu unao lack creativity na uzalendo,viongozi wengi wapo kwa ajili ya kutekeleji wa mambo yao binafsi
   
Loading...