Ugeuzaji wa uvaaji wa Chupi unasaidia sana kutofumaniwa!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,882
Katika mahojiano yake exclusive na Mimi muda mfupi tu uliopita Mnajimu na Mganga mmoja ' mashuhuri ' nchini Tanzania amesema kuwa njia nzuri na ya pekee ya kukwepa ' Kufumaniwa ' ama na Mume au Mke wa Mtu ni kwa nyie wawili ambao mnakwenda ' kubanduana ' kugeuza uvaaji wa nguo zenu za ndani a.k.a Chupi.

Mnajimu na Mganga huyo aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha Watu wawili wenye mapenzi ya kuiba akimaanisha kuwa mmoja anaweza akawa ni Mume / Mpenzi wa Mtu au Mke / Mpenzi wa Mtu lakini wakaamua kuyasaliti ' Mahaba ' yao na kuamua wao kama wao kutoka ' Kimapenzi ' njia sahihi ya wao kutokuja kujulikana na Wapenzi wao halisi kuwa ' wanawasaliti ' ni ' kugeuza ' uvaaji wa ' Chupi ' zao tu hasa siku ile ambayo wanajua wanaenda ' kubanduana '.

Alisema kuwa kitendo cha kugeuza uvaaji wa ' Chupi ' kunasaidia kumfanya yule Mume au Mpenzi wako ' halisi ' asihisi chochote juu yako kama unamsaliti na kwamba kile kitendo chako cha Wewe kugeuza uvaaji wa nguo yako ya ndani ' Chupi ' kunasaidia sana kugeuza na kuyahamisha ' mawazo ' yake na inakuwa ngumu kwa yeye kugundua kama ' unamsaliti '.

Hivyo kama Wewe unajijua fika kuwa ni Mume au Mke au Mchumba wa Mtu na unataka ' kumsaliti ' mwenzio kwa kwenda ' kubanduana ' na huyo ' Hawara ' yako na usijulikane basi haraka sana hakikisha kabla ya kutoka hapo Kwako uwe umegeuza chupi yako kwa kuivaa ' nje ndani ' lakini pia mwambie na huyo Mtu wako unayeenda kukutana nae kuwa na yeye pia huko huko alipo ageuze kuvaa chupi yake ili msijulikane au msifumaniwe.

Nadhani sasa nitakuwa nimewasaidia ' Wasaliti ' wengi wa Mahusiano yao na kuanzia sasa hamtaweza tena ' kushtukiwa ' na hata ' kufumaniwa ' hivyo mambo yote kuanzia sasa ni ' mwendo mdundo '.

Naomba kuwasilisha na nitoe Shukurani zangu za dhati kabisa kwa huyu Mnajimu na Mganga ' maarufu ' ambaye aliweza kuwa muwazi kwangu na kunipa haya ' maujanja ' ya kusalitiana na kuepuka kufumaniwa na Mimi bila hiyana leo nimeona nililite kwenu ili nanyi humu mtumie hiyo ' mbinu '.

Kwa atakayefanikiwa na huu ' ujanja ' tafadhali asisite kuleta ' mrejesho ' wake humu na nimalizie tu kwa kusema kuwa hapo kikubwa ni Chupi na siyo Boksa. Usije ukajaribisha hii mbinu katika ' Boksa ' hapana hapa silaha kuu ni ' Chupi ' tu na kama huna basi na unajijua ni ' TEAM MSALITI ' wahi mchikichini ukanunue kwani zimejaa tele.
 
Mkuu post zako huwa zinakuwa ndefu kama makala za gazeti la Mawio, ukichanganya na maandishi kuwa madogo kama mbegu za mchicha, napita tu kuja kusoma koment ili nijue post ilihusu nini.
 
Back
Top Bottom