Ugawaji vitalu vya uwindaji wa kitalii kielektroniki ongezeko ni 196.4%

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Zoezi la ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada kwa kutumia mfumo wa kielektroniki umetajwa kuwa na faida kubwa kuliko ilivyokuwa ikitumika kwa njia ya kiutawala (administratively).

Imeelezwa tangu kuanza kwa ugawaji wa vitalu kwa njia ya mnada mwaka 2019, Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wananyamapori Tanzania (TAWA) imeendesha minada 7 ya vitalu vya uwindaji iliyohusisha vitalu 100 hadi Machi 2022.

7b95c13f-5e6c-48dd-be99-e2181b025ae1.jpg

Kaimu Kamishna wa (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda

Jumla ya Dola 9,798,000 zimepatikana wakati ingetumika mfumo wa kawaida wangepata Dola 3,306,000, hivyo kiasi kilichopatikana ni sawa na ongezeko la 196.4%.

TAWA wameeleza kuwa wataendelea na minada ya kielektroniki hadi hapo vitalu vyote vilivyopangwa kufanyiwa minada hiyo vitakapomalizika.

Kaimu Kamishna wa (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda amesema utaratibu huu ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayolenga kuongeza idadi ya watalii hadi milioni tano na mapato hadi Dola Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025.
 
Kuwa na udhibiti mzuri isije kuwa siku zijazo tutafunga safari kwenda kutazama wanyama kwenye zoo za wazungu.
 
Back
Top Bottom