Uganda yaonya kuhusu mashambulio ya kigaidi

Uganda yaonya kuhusu mashambulio ya kigaidi

mdau wetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
548
Reaction score
62
[h=1]Polisi ya Uganda imetahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea mashambulio ya kigaidi katika nchi hiyo. Tahadhari ya polisi ya Uganda inatolewa siku chache tu baada ya jirani yake Kenya kushuhudia mashambulio ya kigaidi siku za Jumamosi na Jumapili katika miji ya Mombasa na Nairobi. Fred Ananga msemaji wa polisi ya Uganda amesema kuwa, kufuatia uwezekano huo wa kutokea mashambulio ya kigaidi, polisi ya nchi hiyo imechukua hatua za kuimarisha usalama katika mji mkuu Kampala na miji mingine mikubwa na midogo ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Msemaji wa polisi ya Uganda ameongeza kuwa, polisi ya nchi hiyo imelazimika kujiweka tayari kutokana na jirani yake Kenya kushuhudia mashambulio kadhaa ya kigaidi. Fred Ananga amewataka wananchi wa Uganda kuwa macho na kuchukua tahadhari kubwa na wakati huo huo kutoa taarifa kwa polisi mara tu watakaposhuhudia nyendo zozote zile za kutia shaka za baadhi ya watu. Aidha polisi ya Uganda imewataka wamiliki wa hoteli, maduka makubwa, mabasi, taksi na wahusika katika makanisa kutoa ushirikiano unaotakiwa kwa polisi hasa katika kipindi hiki ambacho kuna uwezekano Uganda nayo ikakabiliwa na mashambulio ya kigaidi kama yale ya Kenya[/h]
 
Du! Mabikra 72 wanatafutwa kwa kumwaga damu za watu! Huu nao ni ushetani wa aina yake!
 
Back
Top Bottom