Uganda: Kizza Besigye akamatwa na Polisi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Msemaji wa chama cha Forum for Democratic Change Ssemujju Ibrahim Nganda amethibitisha kwamba mgombea urais wa chama hicho Dkt Kizza Besigye amekamatwa.

Amekamatwa akiwa eneo la Naguru, Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.

Wafuasi wa upinzani, Besigye akiwemo, walitaka kukagua nyumba hiyo lakini wakazuiwa.

Besigye alikamatwa na maafisa wa polisi walioondoka naye kutoka eneo hilo.

Haijabainika amepelekwa wapi.
 
Hivi huyu jamaa mbona anaonewa sana,kila uchaguzi huishia kunyanyaswa tu,kama wewe museveni unajihisi unakubalika na waganda unamuhofia nn Kizza?, GENTAMYCINE ,mshauri Raisi wako kuwa muda wa yeye kung'atuka umefika,au anataka kufia madarakani nini?
 
Sasa kama kakamatwa anategemea kutangazwa kuwa yeye ndiye kashinda kweli? Hapa ndipo napo yakumbuka Maneno ya Yesu Kristo "Je ikiwa mti mbichi unatendewe hivi Itakuwaje kwa mti mkavu"?
 
Msemaji wa chama cha Forum for Democratic Change Ssemujju Ibrahim Nganda amethibitisha kwamba mgombea urais wa chama hicho Dkt Kizza Besigye amekamatwa.

Amekamatwa akiwa eneo la Naguru, Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.

Wafuasi wa upinzani, Besigye akiwemo, walitaka kukagua nyumba hiyo lakini wakazuiwa.

Besigye alikamatwa na maafisa wa polisi walioondoka naye kutoka eneo hilo.

Haijabainika amepelekwa wapi.
Ea haiwezi kuongozwa na upinzani
 
ccm nao si wapo huko.majina ndio tofauti ausio jamani.hii issu ya uchaguzi inamaliza pesa sana tungekua tu kama kwa mfalme mswati
 
Afrika hakuna demokrasia bali kuna maigizo ya demokrasia....
Tena maigizo yasiyo na kificho, maana Tangu napata akili sijawahi kuona nchi yoyote Afrika ikifuata Misingi ya Kidemokrasia hasa hili la uhuru wa mawazo,ukiwa mpenda haki na msema kweli utapakwa chombo au utafanywa kama walichofanywa akina kubenea na bwa kibanda.
 
Demokrasia ya Marekani imegoma kufanya kazi Afrika, hamna nchi hata moja iliyofaulu kuonyesha demokrasia ya kweli. Itakua bora tutafute mfumo tofauti.
 
Back
Top Bottom