Januari 15, 2026 wananchi wa Uganda walishiriki katika zoezi la upigaji wa kura nchini humo kuwachagua viongozi ikiwemo Rais ambapo kinyang'anyiro ni kikali kati ya Rais Yoweiri Museveni (NRM) na Robert Kyagulanyi (Bobi wine) wa NUP.
Madai
Januari 16, 2026 Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram amechapisha Video yenye ujumbe (Caption) inayoeleza kuwa ujumbe unaoeleza kuwa purukushani zimetokea jijini Kampala kati ya Polisi na wafuasi wa Mgombea wa Urais, Robert Kyagulanyi Bobi Wine.
Uhalisia wa video hiyo
Baada ya ufuatiliaji wa kina kwa kutumia nyenzo za kidigitali imebainika kuwa video hiyo si ya tukio la mwaka 2026.
Video hiyo imekuwepo mtandaoni kuanzia Desemba 2025, ambapo ufuatiliaji umeonesha pia miongoni mwa vyanzo vya awali vilichapisha video hiyo Desemba 16, 2025.
Mtumiaji mmoja
alichapisha video hiyo Desemba 16, 2025 na kuandika ujumbe unaoashiria kuwa ni tulio lililotokea Desemba 15, 2025 katika mkutano wa kampeni wa Bobi Wine katika eneo la Namungoona huko Kampala. Tazama
hapa kuona chanzo kingine kilichochapisha video hiyo.
Aidha hakuna chanzo chochote kilichoripoti kutokea kwa maandamano au uwepo wa vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Bobi Wine huko Kampala.