Ugaidi, Siasa na Athari zake

Ugaidi, Siasa na Athari zake

Tanganyika jeki

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2011
Posts
243
Reaction score
89
1. Je, kwa Serikali kutumia nguvu kubwa kuitangazia dunia kuwa Tanzania kuna magaidi na uwepo wa vitendo vya ugaidi kwa kuwakamata na kuwafungulia kesi 'viongozi na wanachama wa Chadema' hakuna athari zozote kiuchumi?

2. Je, iwapo kama tetesi na shutuma kutoka Chadema ni sahihi ya kuwa kesi hizo zinabambikiziwa na ni za kisiasa zisizohusiana kabisa na ugaidi. Je, hiyo si matumizi mabaya ya sheria hiyo ya ugaidi? Na nini athari za baadaye kwa sheria yenyewe?

3: Pia, ni taswira gani tunayoionesha dunia jinsi tunavyoweza shughulikia masuala ya nyeti na ya 'kweli' ya ugaidi km milipuko miwili ya mabomu ya Arusha iwapo 'intelijensia' yetu bado haijaweza kujua kiini cha ugaidi huo?

4. Iwapo tukio la tindikali la Igunga ni 'ugaidi', ni magaidi wangapi ambao tumewahukumu kwa kesi batili au tumewaacha mitaani wakitanua wakati ni 'magaidi'?

Nawaza kwa kujiuliza kwa sauti.
 
Usiwe na hofu! Hiyo ndiyo style ya ccm kukata roho! Sasa hivi wanatumia njia yoyote katika kupumua pumzi ya mwisho bila kujali iwapo njia hiyo ni hatari kwa taifa na hata kwa wao wenyewe!!
 
1. Je, kwa Serikali kutumia nguvu kubwa kuitangazia dunia kuwa Tanzania kuna magaidi na uwepo wa vitendo vya ugaidi kwa kuwakamata na kuwafungulia kesi 'viongozi na wanachama wa Chadema' hakuna athari zozote kiuchumi?

2. Je, iwapo kama tetesi na shutuma kutoka Chadema ni sahihi ya kuwa kesi hizo zinabambikiziwa na ni za kisiasa zisizohusiana kabisa na ugaidi. Je, hiyo si matumizi mabaya ya sheria hiyo ya ugaidi? Na nini athari za baadaye kwa sheria yenyewe?

3: Pia, ni taswira gani tunayoionesha dunia jinsi tunavyoweza shughulikia masuala ya nyeti na ya 'kweli' ya ugaidi km milipuko miwili ya mabomu ya Arusha iwapo 'intelijensia' yetu bado haijaweza kujua kiini cha ugaidi huo?

4. Iwapo tukio la tindikali la Igunga ni 'ugaidi', ni magaidi wangapi ambao tumewahukumu kwa kesi batili au tumewaacha mitaani wakitanua wakati ni 'magaidi'?

Nawaza kwa kujiuliza kwa sauti.

Siku ya Kwanza Marekani ilipotoa list ya magaidi 32 wanne kati yao wakawa watanzania Membe alipiga kelele kuwa TZ kuna amani hakuna Magaidi, sijuwi kama wanelewa maana hasa ya Ugaidi na impact yake!
 
Wana JF naomba mnikumbushe!...yule gaidi ailiye mmwagia tindikali Kubenea kesi yake itatajwalini?..nashangaa sana kusikia polisi ikihangaika na kesi ya ugaidi ya igunga wakati hawajatimiza ahadi ya mkuu wa nchi ya kuwakamata waliomdhuru kubenea.
Kampeni zinazoendelea sasa ni dalili ya mwisho wa ccm. RIP chama kikongwe
 
Back
Top Bottom