Ufumbuzi wetu huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufumbuzi wetu huu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwame Nkrumah, Sep 18, 2009.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Tumeongea sana, tumelalamika sana, mbaya zaidi TUMEPUUZWA sana.
  Matatizo yetu yameongelewa sana, yanajulikana sana, mipango mingi sana imewekwa lakini hatujaona utatuzi wake. Ufisadi unaendelea, mikataba mizitomizito inaendelea kusainiwa , tunaambiwa ni kwa manufaa yetu lakini hatujui inatunufaisha vipi. Wasemalo watawala ni sheria, hakuna kuhoji.
  Nchi zote zinazotuzunguka [even tiny Malawi] kwa namna moja au nyingine zimebadilisha matabaka ya uongozi katika nchi zao. Ni Tanzania tu ndiyo imebaki na tabaka lile lile tangu uhuru mpaka leo.
  Baada ya kusoma mada hii, utajua nini cha kufanya, kitafanyika vipi na lini kifanyike.
  Ufumbuzi wake ni kwa sisi wana JF tukubaliane na kumuomba mwanajamii mwenzetu Mh. Zitto Kabwe agombee Urais na tupigane ashinde Urais. Tuweke Ikulu mwana JF. ATUTUMIKIE wananchi wa Tanzania. Tutampa kazi tatu tu za kufanya, kutuletea maendeleo, kutuletea maendeleo na kutuletea maendeleo.
  Ningependa kusema mapema kabisa mimi simjui Mh. Zitto zaidi ya kumuona kwenye TV na kufuatilia anavyoweka maslahi ya Taifa mbele, sijawahi kumuona, siyo kabila lake, siyo muislam mwenzake, sitoki Kigoma wala sijawahi kufika huko,na wala sina kadi ya Chadema.
  Tukirejea Historia ya mageuzi nchini, yalianzishwa na watu wasiozidi 15 , akina Selasini,Komu, Marando, Lamwai, Mtikila na wenzao. Leo JF ina wanachama zaidi ya 13,000 na wote tunachukia ufisadi. Wengine wanaweza kusema mbona watu wenyewe wengi mpo nje? Jibu ni kwamba hata ukombozi wa Afrika ulipata vuguvugu baada ya vita ya kwanza na pili duniani, baada ya Waafrika kurejea kutoka vitani na kurudi na mbinu mpya za mapambano dhidi ya mkoloni.Sasa tupo katika mapambano , ni mapambano ya aina nyingine ya kumng’oa mkoloni mweusi. Watu hawa walio nje wanaweza kuja na mawazo mapya, mbinu mpya, teknolojia mpya na kasi mpya.Ukiangalia nchi zilizoendelea ghafla kama vile za Chui wa Asia, kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kwa kutumia raia wao walio nje na baadaye kurudi nyumbani kujenga mataifa yao.
  Vuguvugu la sasa litaendeshwa kwa kuunganisha nguvu hizi mbili, walio ndani na walio nje pia.Tuunganishe nguvu kwa kuung’oa utawala wa kifisadi na usio na tija wa CCM na vibaraka wao na kumuweka Zitto madarakani.Simpendekezi Zitto na CHADEMA kwa kuwa tu eti ni mpinzani bali kwa njia mbadala za maendeleo kwa sababu njia za chama tawala cha sasa zimeshindwa, na hata wapo wanaodiriki kusema zimeturudisha nyuma.
  Kama ambavyo Obama aliweza kuwashawishi watu wengi kwamba anafaa kuwa Rais baada ya kutoa hotuba yake kwa chama chake cha Democrat kule Boston mwaka 2004, na mimi nimeshawishika na Zitto siyo tu kwa hotuba yake aliyoiweka hapa ambayo aliitoa kwa wapiga kura wake wa Kigoma bali pia kwa mapambano yake yasiyoisha dhidi ya mafisadi, na pia kuwa na msimamo dhabiti na kutokuyumba kwa yale anayoyaamini. mfano mzuri ni ununuzi wa mitambo ya Dowans, wengi wetu tulipinga msimamo wake lakini Zitto alitetea msimamo wake humu ndani, magazetini na kwenye mahojiano mbalimbali.Kwa maana nyingine Zitto haendeshwi na kura za maoni.
  Ninaungana na mwandishi mahiri Tanzania Absalom Kibanda, ambaye licha ya kupinga Mh.Zitto kugombea uenyekiti wa CHADEMA alimuita Mh. Zitto “ a visionary leader’ katika moja ya mabandiko yake humu JF. Lakini mtu ambaye alimwelezea Zitto kwa ukamilifu zaidi ni mwanachama wa JF Bluray, yeye aliandika kwamba “he raises the right issues and makes the right choices”
  Kuna watu waliwahi kusema eti JF iwe chama cha siasa. Mimi nakataa wazo hilo. Tutumie mbinu wanazotumia wao, walipitisha sheria ya takrima na wanaitumia vilivyo kwa manufaa yao.. Tuchukue mbinu zao, tuzikumbatie na na tuzitumie kwa manufaa yetu.
  Mgombea wetu asigombee mwaka 2010, bali 2015.Ni ndoto ambayo haiwezi kutimilika kwa mgombea wa upinzani kushinda urais dhidi ya mgombea wa CCM ambaye mwenyekiti wake, ambaye pia ni mgombea wa urais kupitia chama hicho,ni yeye pia ambaye huteua Tume ya Uchaguzi, hii ni sawa na kuwa una kesi tayari mahakamani, halafu wewe ndiye unachagua hakimu wa kusikiliza kesi yako! Kwa wakati huu tuweke mazingira mazuri ya mgombea wetu kushinda kwa kubadilisha pamoja na mambo mengi tume ya uchaguzi iwe huru.
  Tuanzishe interest group ambayo lengo lake ni kumuweka Mh. Zitto madarakani, Kama nakala za ripoti ya meremeta ziliuzika katika masaa 24, inaonyesha jinsi gani ufisadi unachukiwa, na jinsi gani wananchi wapo tayari kwa mabadiliko. Mabadiliko yanawezekana. Kauli mbiu yetu ya kumuweka Mh.Zitto madarakani itakuwa “REJESHA TANZANIA YETU”
  Anatakiwa tu jemedari wa kupanga, kuhimiza, kutoa motisha na kuongoza mapambano haya.
  Kutegemea kwamba maendeleo yatapatikana na ufisadi utazimwa chini ya utawala wa CCM ni sawa na kuzima moto na syringe, badala ya firehorse.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ni wazo zuri
   
 3. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ufumbuzi wa tatizo lako ni kujiunga na chama cha Zitto Kabwe. Kitakupatia mgombea kama Dr Slaa au Mbowe kuongoza serikali ya nchi au upinzani hadi hapo Zitto atakapofikia umri wa miaka 40 au zaidi. Yeye sasa ana miaka 33 tu.
   
Loading...