Ufukarishaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufukarishaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Waridi, Nov 26, 2011.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu watanzania,
  Tunapoendelea kutafakari mustakabari wa taifa letu na pengine kutafuta suluhu ya matatizo lukuki yanayotukabili, nimeona niwashirikishe katika kutafakari mojawapo ya matatizo makubwa yanayotukabili, ambalo kwa bahati mbaya hatuchukui hatua zozote dhidi yake na linazidi kukomaa, matokeo yake yanaweza kuwa angamio la wengi kama sio wote.Tatizo ninalolizungumzia leo ni mchakato ambao umeendelea kwa muda mrefu, yaani UFUKARISHAJI.
  Je, ndugu zangu watanzania, nanyi mnaliona hili tatizo?
   
 2. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nataka twende taratibu katika hili, ili tuweze kuuona ukweli wote. Mchakato wa ufukarishaji una njia nyingi na una taasisi kadhaa za kuutekeleza.
  wafukarishaji wakuu wa nchi yetu kwa sasa ni BENKI YA DUNIA na SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF)
   
 3. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  kwa miaka mingi, vyombo hivi vikitumiwa na mataifa ya kibepari ya magharibi, vimeendeleza mpango wa kulifukarisha taifa letu. Vimetuweka katika mtego wa madeni ambao hatutaweza kujinasua ili tuendelee kuwa taifa la kunyanyaswa. Hivi leo Tanzania imefukarishwa kiasi kwamba inadaiwa zaidi ya Shilingi trillioni 15.
  umekuwa ni mpango wao tokea awali kwamba tufikishwe katika kona ambayo hatuwezi kulipa, ili kila sharti tutakalopewa tutimize tu, kila amri watakayotoa tutekeleze ... watanzania (viongozi kwa waongozwa) tuamke!
   
 4. a

  alkon Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba ubepari unatuongezea umaskini. Lakini nina maoni tofauti kidogo juu ya deni la taifa. Kwa kweli limekuwa kubwa, na linazidi kukua. Kimsingi, taifa kukopa si tatizo, kwani hata mataifa makubwa kama Marekani nayo yanakopa. Tatizo ninaloliona kwa Tz ni kwamba tunakopa bila malengo maalum. Hii mada inaturudisha kule kule kwamba hatuna viongozi makini. Viongozi tulionao hawataki kufikirisha bongo zao. Akili zao zote zimeishia utegemezi wa mikopo na misaada ya wahisani. Mimi naamini kwamba tungekuwa na uzalendo wa kutumia hiyo mikopo kuchochea uzalishaji wa ndani, tusingepata tatizo lolote. Lakini, kwa hali ilivyo, tunakopa, halafu badala ya kuzalisha, tunaishia kulipana posho na kuiba. Mimi hapo sioni tatizo la WB au IMF. Wao wanafanya biashara, na biashara yenyewe tunaijua vizuri kwamba ni yakinyonyaji. Hivyo, lingekuwa jukumu letu kukopa kwa malengo, huku tukiitumia mikopo hiyo kama mitaji ya uzalishaji mali, na baada ya muda fulani kuachana nayo. Wewe angalia sasa hivi: bajeti yetu ni trilioni 13.5, uwezo wetu wa ndani ni trilioni 8 (naomba kusahihishwa hapa), halafu bado tunachukua mikopo na kuishia kulipana posho na kuiba. Hapo WB na IMF wana tatizo gani? Tatizo ni sisi tusio na akili ya kutumia vema rasilimali chache tulizo nazo, ikiwemo hiyo mikopo.
   
 5. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Uko sahihi pia, hao viongozi wabovu ni sehemu ya huu ufukarishaji. WB wamo ndani, IMF huwatoi, Viongozi wetu wamo, makampuni fulani fulani (nitaeleza baadaye) yamo. Anayefukarishwa ni mwananchi, ndiye ninayelenga aone hili ili akombolewe.
  IMF licha ya mikopo, walitupatia (sisi na mataifa mengine yanayoitwa LICs) kifurushi cha Structural adjustment miaka ya 80 hadi 90. Tukalaghaiwa kwamba kingeleta ukuaji wa uchumi, badala yake kilitufukarisha zaidi na madhara yake tunayo hadi leo. Wakaja tena kwa style mpya mara hii ikiitwa MKUKUTA, badala ya kutusadia unawanufaisha wao. Kabla hatujapona vidonda na machungu, hivi juzi wameleta wanachokiita Policy Support Instrument (PSI), na viongozi wetu kama kawaida yao wanakumbatia tu. madhara ya PSI nayo yako njiani. Ni wakati wa kusema NO! kama tunataka kupona
   
 6. a

  alkon Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli. Mimi ni mkereketwa sana wa maendeleo ya watu wa kawaida. Nasikitika sana kwamba tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru huku hatuna hata uwezo wa kujilisha wenyewe, kusimamia elimu, wala matibabu. Nilipokuwa shuleni, nililishwa hii nadharia ya ubepari na nikaipokea kweli kweli. Kwa kweli enzi za Mwalimu Nyerere mtu yeyote timamu hakuwa na sababu ya kutoamini maneno yake kwa sababu alisimamia maneno yake kivitendo. Alikuwa amejitoa kweli kweli kwa ajili ya uzalendo wa nchi. Ni wazi kwamba kuna mambo mengi yalimshinda (hasa uchumi), lakini itoshe tu kumshukuru kwa ajili ya uzalendo wake na jitihada alizoonyesha. Hata huko kushindwa kwake hakukuja hivi hivi. Kilichotumaliza moja kwa moja ni Vita ya Kagera na ukame wa miaka ya '80 mwanzoni. Pamoja na hayo, alijitahidi kwa uwezo wake wote, na alituachia mashirika ya umma na vitu vingine vingi vya kukumbuka. Kikubwa kuliko vyote alichotuachia ni amani, uzalendo, na mshikamano wa kitaifa. Ni vema pia tukajikumbusha kwamba mafanikio haya hayakuja hivi hivi, bali yalitokana na utawala wa sheria, kusimamia haki, na kusimamia tabaka la wanyonge.

  Leo hii haya mambo yote hakuna. Huwezi kutofautisha kati ya bepari wa Ulaya na fisadi wa Tz. Bepari anaiba anapeleka kwao, mafisadi nao wanaiba wanatia mfukoni. Mimi nina imani kwamba hata kile kidogo tunachoachiwa na mabepari tungekisimamia vizuri, nchi yetu bado ingeonekana ni tajiri tu. Nchi kama Ghana wamepitia sera hizo hizo za SAP, lakini leo hatufanani nao. Hata hapa jirani yetu, nchi ya Rwanda ambayo imetoka vitani hivi karibuni tu, tayari wameanza kutupita kwa kasi. Siri kubwa ni kwamba Kagame hataki mchezo. Halafu, mpaka miaka ya '60 na '70, hatukuwa na tofauti kubwa sana na nchi kama China, Singapore, na Brazil. Lakini leo ona walipo. Pamoja na uchapakazi, China hawacheki na mafisadi. Anayebainika anafungwa, hata kunyongwa. Kwa kuwa sisi hapa tumeamua kuwekeza katika manenomaneno, ujanjaujanja, na ubabaishaji, hatuwezi hata siku moja kutegemea kutoka kwenye lindi la ufukara. Kwa kuwa hao WB na IMF wameshatugundua kwamba hatuna akili, hawataisha kubuni majina, mara SAP, mara MKUKUTA, mara PSI, n.k.

  Ukitaka kuona uwezekano kwamba nchi yetu inaweza kabisa kupiga hatua fulani hata katikati ya hayo masharti ya WB na IMF, kumbuka enzi za Mkapa. Kuna mambo kadhaa huwa sikubaliani na Mkapa (hasa kuwatupa wanyonge), lakini huwa namkubali kwenye uchapakazi na usimamizi makini. Kikwete angeanzia pale alipoachia Mkapa na akaongeza kasi kidogo, leo tusingekuwa tunazodoleana kama tunavyofanya sasa hivi. Mkapa alijenga mazingira ya uwekezaji, akapunguza deni la taifa, na kukuza akiba ya nchi. Zipo tuhuma kwamba yeye na watu wake wa karibu walifanya ufisadi kupitia mageuzi hayo, lakini nisingependa kuelekea huko kwa sasa. Kihistoria, mageuzi yote makubwa kama hayo lazima huwa yanakuja na mapungufu na changamoto fulani. Upungufu mkubwa wa Mkapa, kwa mtazamo wangu, ulikuwa ni ukosefu wa trickle-down effect ya uchumi kwa wananchi wa kawaida. Rasilimali zote kubwa za kitaifa (hasa fedha) zililimbikizwa mikononi mwa serikali kuu na mashirika yake, huku wananchi wa kawaida wakibaki watazamaji tu. Hivyo, jukumu namba moja la Kikwete lilikuwa ni kuhakikisha kwamba pato la taifa linashushwa chini ili lisaidie kunyanyua maisha ya wanyonge. Wazo lake la "mabilioni" lilikuwa ni zuri sana, isipokuwa lilikosa usimamizi na hivyo kuishia kuneemesha mabenki na wajanja wachache. Wazo kama lile lingesimamiwa vizuri (yaani kuwawezesha wanyonge kimitaji), nchi yetu isingekuwa hapa tulipo leo. Muda ulivyozidi kwenda, Kikwete akaanza kutapanya mali badala ya kuzalisha, watendaji wake nao wakamsoma na kuungana naye kufilisi nchi. Mwisho wa yote, nchi imefilisika, deni la taifa limekuwa kubwa, ufisadi umetapakaa kila kona, maisha yamekuwa magumu, na wananchi wamekata tamaa na kuanza kuichukia serikali (angalia maandamano).

  Nimefurahia hitimisho lako kwamba ubepari wa kimataifa na uongozi mbaya vyote vinahusika kudidimiza nchi yetu. Miaka ya nyuma nilidhani ubepari unachangia kwa 70% na uongozi mbaya kwa 30%, lakini leo maoni yangu ni kwamba uongozi mbaya ndio wenye 70% na ubepari wa kimataifa 30%. Uchambuzi ninaopata shida kidogo kukubaliana nao ni ule wa miaka iliyopita kwamba mfumo wa kimataifa ndio unahusika na ufukara wetu. Hapana. Hiyo framework nadhani ilifaa kuelezea hali ya mambo miaka ya '60 na '70 kwa sababu tulikuwa ndo tumetoka kwenye ukoloni, hivyo nchi ilikuwa changa, haikuwa na wasomi, na mfumo wa utawala ulikuwa bado ni dhaifu. Lakini leo hii, baada ya miaka 50, na hasa hasa tukizingatia kwamba misingi ya utaifa tayari tunayo, na wasomi wapo wa kila aina, sababu kubwa inayobaki kuelezea ufukara wetu ni kwamba tuna viongozi walafi, wasio na upeo wa kiuongozi, na wasiozingatia maslahi ya nchi.

  Asante.
   
 7. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hadi leo ndugu yangu, mfumo wa kimataifa (kwa maoni yangu) unahusika kwa zaidi ya 50% katika kutufukarisha. Huu mfumo ambao leo unaitwa neo-liberalism + utandawazi; ndio umefungua njia zaidi ili mnyonge akamuliwe hadi tone la mwisho. Ndio umetuletea makampuni yanayotushawishi kuamini kwamba vitu vyao fulani NI MAHITAJI YA LAZIMA/MUHIMU wakati SIO. Mara baada ya kukubali mahitaji hayo, tumejikuta tukipandishiwa bei za huduma zao kila uchao. Fikiria kwa mfano; mawasiliano ya simu, ndio ni muhimu kuwasiliana, lakini angalia biashara ya mawasiliano inavyokamua watu, gharama za kupiga simu zilivyo juu, vifaa vya mawasiliano bei zake zilivyo ghali, angalia faida inayokusanywa na makampuni hayo. Yote inatokana na kumfukarisha kisawasawa mnyonge.
  Ni wakati pengine wa kuwaambia, Vodacom, tiGO, Airtel na wengine, kwamba ndio tunahitaji kuwasiliana lakini mkome kutukamua. Kama wewe ndugu yangu unafanya kazi Tanzania, hebu piga mahesabu ni kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa ajili ya kuilisha simu, kabla hujamiliki simu ilikuwaje?
   
 8. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sehemu nyingine ya ufukarishaji wa watanzania iko katika kuwapatia watanzania wengi elimu duni isyoweza kuwasaidia kumudu maisha yao. Elimu ya namna hii iko katika shule za msingi na sekondarizisizokuwa na walimu wala vifaa vya kufundishia. wananchi wanadanganywa na wanasiasa kwamba wanapewa elimu, kumbe wanapewa garasa litakalokuwa mzigo katika maisha yao. Watanzania tunapaswa kuikataa kwa nguvu zote elimu hii kabla haijaendelea kuleta madhara makubwa!
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ufukara ni janga la pili baada Ufisadi ambao karibia viongozi wetu wote ni mafisadi
   
 10. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ufukarishaji mwingine umewajia watanzania kwa njia ya uwekezaji na uchimbaji madini. Kufukarishwa ni pamoja na kunyang'anywa ardhi, na kuondolewa kwenye maeneno ya makazi, kisa uwekezaji.
  Ni kama vile andiko linatimizwa kwa watanzania 'asiye nacho ananyang'anywa hata kile kidogo kilichosalia'
   
Loading...