Ufugaji wa kondoo na ng'ombe

Ufugaji wa kondoo na ng'ombe

Naombeni kwa anaejua ni kipi bora kati ya ufugaji wa kondoo na ng'ombe wa kienyeji kwa maeneo ya Kahama shinyanga. Yani kipi kinaweza kuwa kinalipa kwa uharaka kuzidi kingine?

Ahsante naomba kuwasilisha
Mkuu, vyote ni vinalipa LAKINI inategemea na factor nying, mfano malengo yako, soko lako mtaji ulionao NK
Ni vizuri ukajiuliza kwa context ya TANZANIA kati ya nyama ya KOndoo, mbuzi na ngombe nini kinalika zaidi? mara nyingi ukitoa mikoa ya Arusha na kwa mbali Singida sijawahi ona NYAMA ya KONDOO buchani, najaribu kusema nini, fuga kitu ambacho hata ukiwa na shida unaweza peleka buchani ukapata pesa, walaji wa kondoo ni wachache saana miongoni mwetu watanzania

UFUGAJI unalipa KAMA utatumia akili,, usifuge kama babu zetu walivyokuwa wanafuga,,, anza na malisho pata malisho ya kutosha, nunua ngombe kipindi cha kiangazi ..wape balanced diet ndani ya miezi mitatu peleka buchani, hiii hata kama unauishi eneo dogo unaweza kufanya==same applied hata kwa mbuzi...hutaingia garama kubwa na wala hutakaa na mifugo muda mrefu

Kidumu chama cha MAPINDUZI
 
Shida ya ng’ombe ni malisho lakin pia wanabagua sana vakula na ukizingatia mkoa unaokaa ni semi desert
Kwa ushauri wangu fuga kondoo na Mbuzi hao malisho yao hayana shida na wanakula chochote ata mifagio wanakula lakin pia hawana galama sana ktk matibabu na mabanda na hata eneo hawaitaji kubwa sana.
 
Naomba kama hauto jali ungaliweka hapa ili iwe msaada kwa wengine pia watakapo hitaji upatikanaji wa hizo mbegu. Mfano kwangu naweza msaidia kupata Met Master, Dopper, na Black head.
Sawa mkuu🙏🙏

Kondoo wapo kahama sehemu Moja maalufu Kwa jina la salawe Kuna mnada mmoja mkubwa hufanyika mhangu Kila jmosi ya wiki.

Ni muda wa masaa2-3 kutoka kahama ctd stend na kutoka mwanza nyegezi hayazidi masaa3-4 kulingana na gari. Nauli haizidi 6000 Kwa sehemu zote ukipigwa sana basi 7000

Nilibahatika kununua kondoo 6 mnadani na wengine nikauziwa na mfugaji binafisi wote wakiwa na afya njema.
IMG_20230317_095229_925.jpg

Bahati mbaya Sina picha zaidi mkuu ila Kuna clip ngoja niikate then niiweke pia
 
Back
Top Bottom