Ufugaji wa kondoo na ng'ombe

Ufugaji wa kondoo na ng'ombe

Naombeni kwa anaejua ni kipi bora kati ya ufugaji wa kondoo na ng'ombe wa kienyeji kwa maeneo ya Kahama shinyanga. Yani kipi kinaweza kuwa kinalipa kwa uharaka kuzidi kingine?

Ahsante naomba kuwasilisha
Kibiashara ni kondoo mkuu ila uwe maeneo yenye mwinuko.

Ng'ombe wa kienyeji Kwa maeneo hayo ni changamoto sana hasa malisho watu wanalima maeneo ya kuchungia yanaisha kabisa...
 
Naombeni kwa anaejua ni kipi bora kati ya ufugaji wa kondoo na ng'ombe wa kienyeji kwa maeneo ya Kahama shinyanga. Yani kipi kinaweza kuwa kinalipa kwa uharaka kuzidi kingine?

Ahsante naomba kuwasilisha
Ni wazo zuri sana mimi nakushauri kwanza angalia uwezekano wa upatikanaji wa malisho na maji ya uhakika shambani mwako pili nakushauri ufuge Mbegu ya mifugo wano kuwa kwa uharaka kwamfano unapo fuga kondoo wa Dopper ukuaji wao ni mzuri kiasi ya kwamba mfugo akiwa na miezi 6 waweza anza kumuuza iwe kwa mbegu au kitoweo.
Hali kadhalika kwenye Ngombe nako pia kuna mbegu kama Ankole, shawel na wengineo ukuaji wao pia ni wa haraka na uzito mkubwa ambao watakusaidia kuweza kukupa faida kwa muda muafaka.
Na kwenye Mbuzi pia nako hivyo hivyo waweza nunua madume bora kama , Boer, Red kalahare, Savanha,Isiolo/Galla na ukatumia majike ya Mubende au sukuma goat, au ukaenda kwenye hivi vituo vya serekali vya kuhimilisha mbegu ukapata majike bora itakusaidia vyema ktk ufugaji wako.
ANGALIZO. Lishe bora, matibabu kwa wakati na dawa stahiki, na usimamizi wa karibu ndio nguzo imara ktk ufugaji wako. Mungu akubariki ufikie malengo yako. Karibu kwa maswali zaidi.
 
Ahsante sana mkuu
 
Huyu dume ana mwaka na miezi 3
 
Attachments

  • 20250601_104748.jpg
    20250601_104748.jpg
    1.3 MB · Views: 36
  • 20250601_104804.jpg
    20250601_104804.jpg
    1 MB · Views: 37
Back
Top Bottom