commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,957
Ndugu wadau,
Nimejiuliza bila kupata jibu na nikaona ni vema kulileta hapa jamvini ili tulijadili.
Hivi sasa ni kipindi cha kuanza muhula mpya wa shule za msingi na sekondari kote nchini .
Tatizo kubwa lililojitokeza hapa ni jinsi baadhi ya shule zimewaandikia wazazi orodha ndefu ya vifaa vinavyotakiwa.mfano mmoja ni shule moja ya mjini mwanza,ya sekondari(jina nalihifadhi) ambayo imeorodhesha mengi ila nitataja yanayotia shaka kama ifutavyo.
1:Taaluma.-30.000/=
2;kuboresha elimu-30.000/=
3:maabara.-10.000/=
4:ukarabati.-10.000/=
5:Tahadhari.-10.000/=(hairejeshwi)
6.kitambulisho-6000/=
7.sururu.(haikuandikwa bei).
8:Rim double A.15.000/=
9:T-shirt.13.000/=
10😀awati.35.000/=
11:mlinzi.10.000/=
Sasa nitaanza kwa kuchambua moja moja kama ifuatavyo.
Taaluma,*30.000/=
Mwanafunzi wa shule ya msingi anapofaulu kwenda sekondari lengo linakuwa ni kujiongezea kiwango cha taaluma ya elimu ya sekondari.na shule husika inakuwa na walimu wanaolipwa mshahara na serikali.je haya malipo yanakuwa ya nini?
Kuboresha elimu.*30.000/=
Ni jukumu la kila mwalimu mkuu kuhakikisha anakuwa makini kusimamia shule anayoiongoza akishirikiana na walimu wenzake ili kutoa elimu yenye ubora unaostahili kulingana na taaluma waliyoisomea sasa wakati umeorodhesha malipo ya taaluma inakuwaje tena unamtoza maboresho ya elimu?je mshahara wanaolipwa walimu unakuwa wa nini?
Tahadhari.*10.000/=
Mwanafunzi ni wa kutwa na kila siku anarudi nyumbani.na nina imani kila siku hupewa hela ya kujikimu ikiwemo chai na nauli.na mara nyingi walimu huhitaji mzazi aache namba za simu za mzazi.na linapotokea lolote mara nyingi utabeepiwa.
Kitambulisho.*6000/=
Hili ni jambo zuri.kwani linamtambulisha mwanafunzi popote pale na kwa lolo te lile linaloweza kumtokea.tatizo ni kwamba katika shule nyingi na hata hii ambayo ninatumia rekodi zake.mwanafunzi analipa hela lakini hapewi kitambulisho husika kwa wakati pamoja na bei kuwa na walakini kwani picha mwanafunzi anapeleka akiwa amepiga kwa gharama zake.
Sururu.*(haikuandikwa bei)
Hainiingii akilini ni sururu ngapi zinahitajika il kufanyia usafi wa mazingira ya shule.mathalan ni sururu ngapi zimekwisha kusanywa na uongozi wa shule kila mwaka na je zipo katika hifadhi gani ndani ya shule maana inapaswa kuwa shehena kubwa.
Rim double A.*15.000/=
Ni jambo zuri kwa mwanafunzi kuwa na karatasi za kumtosha katika kipindi chote cha muhula wa masomo.lakini je kwa wanafunzi wastani wa mia tatu arobaini,na kila mtoto rim moja ya shs 15.000/= ni sawa na shs milioni tano laki moja na sitini alfu.
Haiishii hapo kwani pamoja na malipo kufanyika bado mzazi hutakiwa kumpa mtoto hela za machapisho(printing),katika kila kipindi cha mitihani.
Je kuna uhakika gani kwamba rim hizo huwa hazirudishwi kinyemela katika masoko na kuuzwa tena.kwani nimejaribu kufuatilia na kugundua kwamba huwa ni muda mchache tu baada ya mihula kuanza na mashuleni ukienda na kumuomba mwalimu husika akuonyeshe shehena hiyo huwezi amini kile utakachokikuta kikiwa kimesalio store rooms.hii ni takriban nchi nzima.
T/shirt 13.00/=
Hili walakini pia ni pale bei zinapokuwa na tofauti kubwa kati ya shule na shule.mfano shule iliyoko jirani na hii wao wametoza shs 6.000/= tu.
Walakini mwingine ni pale ambapo mzazi analazimishwa kununua toka shuleni wakati bidhaa husika na rangi tajwa vinakuwepo madukani pia.
Dawati.*35.000/=
Kila mwaka wanafunzi wapya wanasajiliwa na kutozwa gharama hizi.na ukweli ni kwamba shule nyingi zilikwishaachana na uhaba wa madawati.hivyo ghrama zilipaswa kushuka na kuwa za ukarabati.
Mlinzi*10:000/=
Suala la ulinzi na usalama kwa mali za shule ni suala la kupewa kipaumbele,lakini utata ni pale ambapo mshahara wa mlinzi au walinzi unapobaki kuwa siri.na hapohapo ukipiga hesabu za haraka kwa darasa moja tu lenye wanafunzi mia tatu arobaini kila mmoja@ shs 10.000/=ni sawa na shilingi milioni tatu na laki nne.kwa mwaka kwa darasa moja tu.je kwa shule nzima ni shilingi ngapi hukusanywa?
Na je hela hii inayosalia huenda au kutunzwa kwenye akaunti ipi,maana hela ya mlinzi inaelezwa kulipwa kwa uongozi wa shule moja kwa moja na si kwa akaunti ya shule kwenye benki.
Na walinzi wengi wa shule hizi za kata si wa makampuni ya ulinzi bali ni wa mikataba binafsi kati yao na walimu wakuu husika.
Walakini ni pale malipo yoote niliyoyataja hapa yanapo elekezwa shuleni moja kwa moja.tofauti na pesa ya malipo ya ada ambayo huelekezwa kulipwa katika akaunti ya benki moja kwa moja.
Je kulikoni yoote haya kuachwa yakiendelea kote nchini na serikali na wizara yake ya elimu ikilifumbia macho suala hili nyeti kwa kizazi cha taifa hili la watoto wa walalahoi?
Ieleweke kuwa mbali ya haya bado kuna kero ya umbali kutoka makazi ya mwanafunzi na shule husika.na kwa wale wa vijijini hulazimika kutembea umbali mrefu au kwenda kupanga vyumba karibu na shule.
Wakati huyu wa mjini huanza siku kwa kugombana na kondakta kabla hata ya kufika darasani.
Je ni kwa sababu wakubwa waneemeka wa nchi hii wakiwasomesha watoto wao shule za wakubwa? Na hivyo kutokuwa na uchungu na mlala hoi wa nchi hii, kwani ujinga wa mlala hoi ndio faida ya mneemeka?
Binafsi napenda mzazi kuchangia elimu kwa mtoto wake.
tatizo ni pale yanapojitokeza mazingira ya ufisadi kama haya.bila kuzingatia mzazi anavyohangaika kupata hata hiyo hela ya lishe kwa familia husika.
Naomba kuwakilisha.........