Ufisadi wa kutisha na usanii kwenye chuo cha madaktari Ifakara

spleen

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
3,740
6,295
Ni st francis university college of health and allied science(kilichopo ifakara,morogoro).

1.Kuhusu usanii.
Hili ndio jambo la hatari zaidi,huwezi amini kwenye chuo hiki kozi za kusoma hadi wiki kumi wao wanasoma wiki 2 tu na kufanya mtihani wa kumaliza kozi husika,mfano mzuri ni wanafunzi wanaoenda mirembe kwa ajili ya somo la psychiatry huwa wanakaa wiki 4 tu,wakati wenzao wa bugando,udom na kairuki wanakaa zaidi ya wiki 8.

Unakuta wanafunzi wa mwaka wa pili somo kama pathology ambalo ndio msingi kabisa wa udaktari wao husoma kwa wiki mbili tu.
Ukija kwa wanafunzi wa mwaka wa tano,somo kama otolaryngology(mambo ya pua,sikio na koo),opthalmology(macho),wanafunzi wa chuo hiki husoma kwa wiki mbili tu bila kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye somo husika.

2.Kuhusu ufisadi.
Huwezi amini ada kamili ya chuo hiki ni shilingi 2.6 million,lakini kwa kushirikiana na tcu,uongozi wa st francis umefanikiwa kuidanganya bodi ya mikopo ambapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza hadi wa tatu wanaletewa kiasi cha ada 3.1 million,nyongeza ya laki tano tofauti kabisa na kiasi halisi cha ada husika,lakini cha kusikitisha zaidi,hiyo nyongeza ya ada inachukuliwa na uongozi wa chuo kwa matumizi yao binafsi bila ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa wanafunzi.

Hebu chukulia wanafunzi wa mwaka wa 1-3 ni takribani 400.
400*500000=200,000,000/= kwa mwaka.

Jiulize ni wanafunzi wangapi wanakosa mikopo kwenye vyuo vingine?


Natoa wito kwa serikali na wadau mbalimbali wa elimu kwa kuzingatia uzito wa suala la afya kwa binadamu,ni vyema wakayatatua haya matatizo kwani ni kesho na keshokutwa huyu daktari ambaye anaandaliwa katika misingi isiyotimiza viwango vya ubora wa elimu ndio atakuja kukutibu wewe,rafiki yako,mtoto wako ama mke/mume wako.
 
sijasikia jipu upizani majipu yote ccm

48460-140.jpg


swissme
 
Back
Top Bottom