Ufisadi wa fedha za elimu bure wagundulika

Ufisadi wa fedha za elimu bure wagundulika

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,051
FEDHA zilizotengwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kugharimia elimu ya bure nchini, zimeanza kutafunwa baada ya kubaini kuwapo kwa udanganyifu unaofanywa na walimu wakuu kwa kuongeza idadi ya wanafunzi hewa ili kupata fedha zaidi.

Zoezi la kuhakiki wanafunzi limekuja baada ya Rais Magufuli aliwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote, kushughulikia udanganyifu unaofanywa na walimu wakuu wanaotafuna fedha kwa kuweka wanafunzi hewa katika suala la elimu bure baada ya serikali kuanza kutoa elimu bure Januari mwaka huu, ikitenga Sh bilioni 18.7 kila mwezi.

Kutokana na hali hiyo, Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam na Manispaa ya Arusha, zimebaini udanganyifu huo na kuanza kuchukua hatua za awali kwa kusimamisha walimu wakuu wa shule husika na pia kuziagiza mamlaka husika kuwavua uongozi walimu hao.

Taarifa za awali zimeonyesha mpaka sasa katika Mkoa wa Simiyu wamebainika kuwepo wanafunzi hewa 2331 ambapo zaidi ya milioni 10 kila mwezi zikipokelewa kwa wanafunzi hewa.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya shule za msingi za serikali 516 na shule za sekondari za serikali 140, ambapo jumla ya walimu wakuu wa shule zote wapatao 656 watavuliwa madaraka yao kuanzia sasa na kutakiwa kurudisha pesa hizo.

Uongozi wa Wilaya ya Kinondoni umemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, kuwavua vyeo walimu wakuu 68 wa shule za msingi kwa tuhuma za udanganyifu wa takwimu juu ya elimu bure na pia umeandika barua kwa Katibu Tawala wa Mkoa ili kumuomba awavue vyeo walimu wakuu 22 wa shule za sekondari. Zaidi ya Sh milioni 70 zimepokelewa kwa wanafunzi hewa.

Kila Mwalimu Mkuu aliyehusika kusababisha ubadhirifu huo wa fedha, atatakiwa kulipa fedha zote kutoka katika mshahara wake huku hatua nyingine zikichukuliwa na Tume ya Utumishi wa Walimu.

Hadi kufikia jana, Wilaya ya Kinondoni imebaini wanafunzi hewa 3,462 kutoka shule 68 za msingi na wanafunzi 2,534 kutoka shule 22 za sekondari. Baadhi ya shule za msingi zilizokutwa na wanafunzi hewa ni Msisiri B, Msewe, Golani, Kibangu, Kimara Baruti, Ubungo Kisiwani, Shekilango, Tandale, Makoka, Mbezi Luis, Kijitonyama, Kinondoni, Mburahati, Makumbusho, Makongo, Kawe A na Ubungo Plaza.

Shule za sekondari ni Boko, Bunju A, Kambangwa, Kawe Ukwamani, Kigogo, Kiluvya, Mbweni, Matosa, Maramba Mawili, Mburahati, Salma Kikwete, Saranga, Temboni, Mabibo, Makoka, Luguruni na Mtakuja.

Katika Mkoa wa Arusha, Walimu Wakuu wa shule za msingi 11 na sekondari 12 wamesimamishwa kazi kwa sababu ya kuongeza idadi ya wanafunzi hewa ili kupata fedha nyingi katika mgawo wa fedha za elimu bure.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo ameunda timu maalumu kwa ajili ya kuhakiki tena kwa mara ya pili, idadi ya wanafunzi hewa katika shule mbalimbali za serikali walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 26.12.

Baadhi ya shule za sekondari zilizoongeza idadi ya wanafunzi ni Arusha Day, Baraa, Kaloleni, Kimaseki, Kinana, Morona, Moshono, Naura, Ngarenaro, Oloirieni na Suye ambapo wamesababisha serikali hasara ya Sh milioni 23.3.

Baadhi ya shule za msingi ni Azimio, Kimandolu, Magereza, Maweni, Moshono, Naura, Njiro Hill, Olkeryani, Salei, Sokon 1, Terrat na Wema na kwa shule hizo za msingi wameisababishia serikali hasara ya Sh 3,940,008.

CHANZO:Habarileo
 
Tumekuwa taifa la watu wasioogopa rushwa au ufisadi. Watanzania tumekuwa ‘sugu’.

Kama taifa inabidi tujiulize maswali magumu na kuyatafutia majibu. Uwepo wa sheria umedhihirisha hauzuii baadhi ya watu kula rushwa au ufisadi.

Ufisadi na rushwa umekuwa kama ni sehemu ya mila na desturi!

Kama taifa tumefikia hatua ya kukubali na kuwaheshimu sana wala rushwa au mafisadi.

Tembea na gari uone jinsi traffic police wanavyochukua rushwa ya shilingi 5000 au 10,000 na kuweka mfukoni kwa kusaidiwa na madereva. Dereva yuko tayari kulipa shilingi 5000 au 10,000 kama rushwa kwa polisi badala ya shilingi 30,000 za faini.

Nenda kwenye hospitali ukajionee jinsi ambavyo wagonjwa wanalazimishwa kutoa rushwa.

Ingia kwenye maofisi ya serikali ushuhudie jinsi ambavyo wafanyakazi wanachukia usipotoa rushwa.

Kinachoshangaza sana ni baadhi ya wananchi kudhani nilizotaja ni rushwa ndogondogo ambazo hawadhani kama zina madhara makubwa na kwa maana hiyo wako tayari kutoa!

Kama taifa, tumejikwaa wapi?

Kuna baadhi ya watu watasema mwarobaini ni Katiba Mpya. Je, ni kweli?

Kuna wengine watasema, mwarobaini ni mfumo. Je ni kweli?

Kuna wengine watasema, mwarobaini ni CCM kuondolewa madarakani. Je ni kweli?

Kuna wengine watasema, tatizo ni mfumo wa elimu. Je ni kweli?

The list goes on and on...
 
Pole zao hawajasoma bado tu nyakati. hii awamu itasomba wengi, watu wabadilike jamani
 
Usiombe uwe na shauri mahakamani, hususan mahakama za mwanzo na zile za wilaya.

Kama huna hela ya supu na soda utajuta!
 
Trafiki ruksa kupewa 5000 ya kubrash viatu Sasa walimu hatupewi hâta 200 yakunywa maziwa?? Elimu bure tuiendee kiutaratibu,tusiwahi kufukuzana...nivema shule husika zikafafanua jinsi zilivyotumia hizi pesa,Kama zilitumika kuboresha mazingira ya kujifunzia hakuna haja kufukuza wakuu Wa shule.
Karne ya 21, shule nyingi hazina walimu wa sayansi,madawati,umeme hâta wasola,computer hâta moja,vifaa vya maabara,maabara,vifaa vya michezo,jengo la utawala,samani za ofisi,vyoo vya walimu/wanafunzi,maji Safi,bwalo la kulia chakula...nk. Alafu tunataka nchi ya viwanda!! Kwa wataalamu gani tunaowaandaa? Hawa wanaokaa chini? Utawezaje mwandiko kama unakaa kwenyejiwe? Maskini Tanzania yangu tunakosa maarifa
 
Usiombe uwe na shauri mahakamani, hususan mahakama za mwanzo na zile za wilaya.

Kama huna hela ya supu na soda utajuta!
Kuna wazee wa mahakama wamekuwa kama madalali wa mahakimu kwa rushwa.

Kinachoshangaza zaidi ni kuona baadhi ya wananchi wako tayari na wana furaha kutoa rushwa ili wapate huduma mapema.

Wewe usiyetoa rushwa au unapinga rushwa ndio unaonekana mtu wa ajabu badala ya watoa rushwa na wapokea rushwa.
 
Hali inatisha hapa nchi, tulipofikia inabidi Mh rais JPM apige magoti awaombea watanzania anaowaongoza kwa Mungu. Ndio soma hata Biblia kitabu cha 2 Wafalme. Kuna wakati ilibidi mtawala kuombea watawaliwa baada ya hali kuwa mbaya. Tumegeuka kuwa Taifa la watu wa ajabuajabu.
 
Huwa sipendi kuiamini hii serikali ya mheshimiwa sana.maana kila cku inakuja na mbinu za kukwepa kutumia pesa kwa visingizio vingi vingi.Tatizo ni moja serikali ya mtukufu sana haina pesa na si jingine.
 
FEDHA zilizotengwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kugharimia elimu ya bure nchini, zimeanza kutafunwa baada ya kubaini kuwapo kwa udanganyifu unaofanywa na walimu wakuu kwa kuongeza idadi ya wanafunzi hewa ili kupata fedha zaidi.

Kutokana na hali hiyo, wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam na Manispaa ya Arusha, zimebaini udanganyifu huo na kuchukua hatua za awali kwa kusimamisha walimu wakuu wa shule husika na pia kuziagiza mamlaka husika kuwavua uongozi walimu hao.

Hivi karibuni, Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa wilaya zote, kushughulikia udanganyifu unaofanywa na walimu wakuu wanaotafuna fedha kwa kuweka wanafunzi hewa katika suala la elimu bure baada ya serikali kuanza kutoa elimu bure Januari mwaka huu, ikitenga Sh bilioni 18.7 kila mwezi.

Wanafunzi hewa Kinondoni

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam kuwa kubainika kwa wanafunzi hao kumekuja baada ya kuagiza mkurugenzi na watendaji kufanya uhakiki shule kwa shule ili kubaini wanafunzi hewa, waliowekwa na walimu wakuu wasiokuwa na uzalendo na kujipatia fedha kinyume cha sheria.

“Hadi kufikia leo (jana) tumebaini wanafunzi hewa 3,462 kutoka shule 68 za msingi na wanafunzi 2,534 kutoka shule 22 za sekondari ambao wameingizwa, ni jambo la kusikitisha fedha za serikali zinapotea kwa sababu ya walimu wakuu wasio waaminifu,” alisema Hapi.

Alizitaja baadhi ya shule za msingi zilizokutwa na wanafunzi hewa ni Msisiri B, Msewe, Golani, Kibangu, Kimara Baruti, Ubungo Kisiwani, Shekilango, Tandale, Makoka, Mbezi Luis, Kijitonyama, Kinondoni, Mburahati, Makumbusho, Makongo, Kawe A na Ubungo Plaza.

Shule za sekondari ni Boko, Bunju A, Kambangwa, Kawe Ukwamani, Kigogo, Kiluvya, Mbweni, Matosa, Maramba Mawili, Mburahati, Salma Kikwete, Saranga, Temboni, Mabibo, Makoka, Luguruni na Mtakuja.

Hapi alisema baada ya kubainika mambo yote hayo, hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, kuwavua vyeo walimu wakuu 68 wa shule za msingi kwa tuhuma za udanganyifu wa takwimu juu ya elimu bure.

“Licha ya kumuagiza hilo nimemuagiza pia mkurugenzi nafasi hizo 68 za walimu hao wapewe vijana wanaokidhi sifa na wenye uwezo wa kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano, tunataka tuwaondoe watumishi wote wenye madaraka ambao bado wanafanya kazi kwa mazoea,” aliongeza.

Aliongeza kuwa, kwa kuwa walimu wa shule za Sekondari, wapo chini ya Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa tayari wamemuandikia katibu huyo barua na kuwaomba awavue vyeo walimu wakuu 22 wa shule za sekondari, waliopeleka takwimu za uongo na kusababisha zaidi ya Sh milioni 70 kwenda kinyume cha matarajio.

Aliongeza kuwa, kila mwalimu mkuu aliyehusika kusababisha ubadhirifu huo wa fedha, atatakiwa kulipa fedha zote kutoka katika mshahara wake.

“Kwanza anashushwa cheo na kuwa mwalimu wa kawaida pili atachukuliwa hatua nyingine kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu lakini tatu atalipa fedha zote zilizopelekwa katika shule yake kinyume na utaratibu kutokana na udanganyifu alioufanya,” alisisitiza Hapi.

Pia Hapi alisema wameshamuandikia barua Mkurugenzi wa Tume ya Utumishi ya Walimu, kuhakikisha hatua nyingine kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya walimu hao.

Wanafunzi hewa

Arusha Mkoani Arusha, walimu wakuu wa shule za msingi 11 na sekondari 12 wamesimamishwa kazi na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha, Athuman Kihamia kwa sababu ya kuongeza idadi ya wanafunzi hewa ili kupata fedha nyingi katika mgawo wa fedha za elimu bure.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo ameunda timu maalumu kwa ajili ya kuhakiki tena kwa mara ya pili, idadi ya wanafunzi hewa katika shule mbalimbali za serikali walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 26.12.

Kihamia alisema uchunguzi walioufanya awali kupitia waratibu wa elimu, wenyeviti na wajumbe wa Bodi na kamati za shule, wakuu wa shule zote za sekondari, wamebaini kuwa shule 11 za msingi zimeongezewa wanafunzi hewa 907.

Alisema wanafunzi hao hewa wameisababishia serikali hasara ya Sh milioni 23.3 kwa shule za sekondari katika kipindi cha Januari hadi Julai mwaka huu na uchunguzi bado unaendelea ili kubaini shule hizo 11 zilizozidishiwa wanafunzi 907.

“Shule za sekondari idadi imeongezewa jumla ya 942 jambo ambalo halikubaliki hata kidogo na Rais alishasema,” alisema Kihamia na kuzitaja sekondari zilizoongeza idadi ya wanafunzi ni Arusha Day, Baraa, Kaloleni, Kimaseki, Kinana, Morona, Moshono, Naura, Ngarenaro, Oloirieni na Suye.

“Tumegundua wanafunzi hao hewa na hakuna fedha ya serikali itakayoachwa iende kwenye mikono ya watu kiholela holela hapana hivyo nimechukua hatua ya kuwasimamisha kazi na wanahojiwa hao wakuu wa shule pamoja na waratibu wa elimu kata, ikithibitika wamekula hela hizo hatua stahiki zitachukuliwa, kwa nini serikali ikose mapato na hela zipo,” alisema mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake, DC Gambo alisema amepokea taarifa za shule za msingi za serikali 11 zenye wanafunzi ambao hawapo shuleni kulingana na hali halisi ya wanafunzi waliopo darasani na kwamba wanafunzi 907 wanapelekewa fedha wakati hawapo shuleni.

Alitaja shule hizo kuwa ni Azimio, Kimandolu, Magereza, Maweni, Moshono, Naura, Njiro Hill, Olkeryani, Salei, Sokon 1, Terrat na Wema na kwa shule hizo za msingi wameisababishia serikali hasara ya Sh 3,940,008.

Gambo alimwagiza Mkurugenzi wa Jiji kuwachukulia hatua walimu hao, akiwemo Ofisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Hussein Mghewa kujieleza kwa Mkurugenzi amechukua hatua gani kabla ya timu hiyo kuundwa. Pia alisisitiza timu maalumu ya Kamati ya Ulinzi na Usalama, imeundwa ili kubaini wanafunzi wengine hewa.

Imeandikwa na Sophia Mwambe, Dar na Veronica Mheta, Arusha.
 
FEDHA zilizotengwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kugharimia elimu ya bure nchini, zimeanza kutafunwa baada ya kubaini kuwapo kwa udanganyifu unaofanywa na walimu wakuu kwa kuongeza idadi ya wanafunzi hewa ili kupata fedha zaidi.

Zoezi la kuhakiki wanafunzi limekuja baada ya Rais Magufuli aliwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote, kushughulikia udanganyifu unaofanywa na walimu wakuu wanaotafuna fedha kwa kuweka wanafunzi hewa katika suala la elimu bure baada ya serikali kuanza kutoa elimu bure Januari mwaka huu, ikitenga Sh bilioni 18.7 kila mwezi.

Kutokana na hali hiyo, Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam na Manispaa ya Arusha, zimebaini udanganyifu huo na kuanza kuchukua hatua za awali kwa kusimamisha walimu wakuu wa shule husika na pia kuziagiza mamlaka husika kuwavua uongozi walimu hao.

Taarifa za awali zimeonyesha mpaka sasa katika Mkoa wa Simiyu wamebainika kuwepo wanafunzi hewa 2331 ambapo zaidi ya milioni 10 kila mwezi zikipokelewa kwa wanafunzi hewa.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya shule za msingi za serikali 516 na shule za sekondari za serikali 140, ambapo jumla ya walimu wakuu wa shule zote wapatao 656 watavuliwa madaraka yao kuanzia sasa na kutakiwa kurudisha pesa hizo.

Uongozi wa Wilaya ya Kinondoni umemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, kuwavua vyeo walimu wakuu 68 wa shule za msingi kwa tuhuma za udanganyifu wa takwimu juu ya elimu bure na pia umeandika barua kwa Katibu Tawala wa Mkoa ili kumuomba awavue vyeo walimu wakuu 22 wa shule za sekondari. Zaidi ya Sh milioni 70 zimepokelewa kwa wanafunzi hewa.

Kila Mwalimu Mkuu aliyehusika kusababisha ubadhirifu huo wa fedha, atatakiwa kulipa fedha zote kutoka katika mshahara wake huku hatua nyingine zikichukuliwa na Tume ya Utumishi wa Walimu.

Hadi kufikia jana, Wilaya ya Kinondoni imebaini wanafunzi hewa 3,462 kutoka shule 68 za msingi na wanafunzi 2,534 kutoka shule 22 za sekondari. Baadhi ya shule za msingi zilizokutwa na wanafunzi hewa ni Msisiri B, Msewe, Golani, Kibangu, Kimara Baruti, Ubungo Kisiwani, Shekilango, Tandale, Makoka, Mbezi Luis, Kijitonyama, Kinondoni, Mburahati, Makumbusho, Makongo, Kawe A na Ubungo Plaza.

Shule za sekondari ni Boko, Bunju A, Kambangwa, Kawe Ukwamani, Kigogo, Kiluvya, Mbweni, Matosa, Maramba Mawili, Mburahati, Salma Kikwete, Saranga, Temboni, Mabibo, Makoka, Luguruni na Mtakuja.

Katika Mkoa wa Arusha, Walimu Wakuu wa shule za msingi 11 na sekondari 12 wamesimamishwa kazi kwa sababu ya kuongeza idadi ya wanafunzi hewa ili kupata fedha nyingi katika mgawo wa fedha za elimu bure.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo ameunda timu maalumu kwa ajili ya kuhakiki tena kwa mara ya pili, idadi ya wanafunzi hewa katika shule mbalimbali za serikali walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 26.12.

Baadhi ya shule za sekondari zilizoongeza idadi ya wanafunzi ni Arusha Day, Baraa, Kaloleni, Kimaseki, Kinana, Morona, Moshono, Naura, Ngarenaro, Oloirieni na Suye ambapo wamesababisha serikali hasara ya Sh milioni 23.3.

Baadhi ya shule za msingi ni Azimio, Kimandolu, Magereza, Maweni, Moshono, Naura, Njiro Hill, Olkeryani, Salei, Sokon 1, Terrat na Wema na kwa shule hizo za msingi wameisababishia serikali hasara ya Sh 3,940,008.

CHANZO:Habarileo
Hao wanafunzi hewa wanaoongezwa hizo PESA zinakwenda mifukoni mwa watu? Mtaishi kwa uongo mpaka lini?
 
Katika hili naiunga mkono serikali, uozo ulikuwa mwingi. Wa Tanzania wengi kwa sasa ni wala rushwa na wadanganyifu high class, no wonder watu wanalalamika pesa hakuna, walizoea kuiba.
 
Hivi no link tutaanza kujadili mambo Mazuri ya nchi yetu...kila Siku fulani mbaya sidhani kama mungu anapenda
 
Tundu Lissu, ambaye ni wakili wa Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amepangua maombi ya wananchi wanne wanaopinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu yaliyompa ushindi mteja wake.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa tena baada ya Mahakama ya Rufaa kufuta uamuzi wa Mahakama Kuu uliotupilia mbali hoja za kupinga matokeo hayo, ambazo ziliwasilishwa na wafuasi wanne wa aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo, Steven Wasira (CCM).

Jaji Mohamed Gwae wa Mahakama Kuu, alitupilia mbali kesi hiyo baada ya kukubali pingamizi la Lissu kuwa wafuasi hao hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo.
 
Back
Top Bottom