Ufisadi wa bilion 230 za mabehewa 'feki' mazito yaibuka, sasa Waziri Mwakyembe kitanzini

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Na KAROLI VINSENT.

ALIYEKUWA Waziri wa Uchukuzi ambaye sasa ni waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Dokta Harrison Mwakyembe amehusika kwa kiasi kikubwa kwenye Kashfa kubwa ya mabehewa ya mizigo 274, iliyoitia hasara Serikali ya Kikwete zaidi ya Bilioni 230

"Waziri Mwakyembe ambaye alijivika vazi la kondoo kwa umma kana kwamba ni miongoni mwa mawaziri wanaofanyaka kazi kwa weledi kwa kuweza kulinda mali za umma,ni wazi vazi hilo limeanza kumvuka."

Taarifa za Dokta Mwakyembe kuhusika kwenye Ufisadi huo mkubwa kabisa kwenye masuala ya Reli nchini kuwai tokea tangu Uhuru inakuja ikiwa siku moja kupita baada ya waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta kuwasimamisha watendaji wa Juu wa Mamlaka ya Reli ya Kati nchini TRL kutokana na kashfa hizo, ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

Tume hiyo ya uchunguzi ambayo inafanywa kwa kushirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi katika Sekta ya Umma (PPRA), na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,ambayo itachukua wiki tatu kuchunguza tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu aliyoko kwenye wizara ya Uchukuzi ameuambia mtandao huu kwamba ni wazi serikali inafanya kiini macho kuwasimamishwa Watendaji hao na anadai ni kama inafanya kitendo cha kuwatoa kafara ili kuwalinda mawaziri waliohusika kwenye ufisadi huo.

"Hapo ni anachofanya sitta ni kiini macho tu,aiingii akilini kabisa yaani watendaji hao wadogo wa TRL,waamue na wafikie makubaliano ya kuiilipa kampuni ya India Bilioni 230 zote bila kupata Baraka za waziri wa Uchukuzi na hata Waziri wa Fedha?maana pesa nyingi sana hizo Bilioni 230 ndugu sio pesa ndogo hapo kuna msululu wa Mawaziri wengi kuhusika,na anachofanya Sitta ni kudanganya umma tu".

Waziri Sitta aliwasimamisha watendaji hao kwa kile anachodai kuvunja makubaliano ya Mkataba kwa kitendo cha kuilipa Kampuni ya Hindustan & Industrial Engineering Limited ya India asilimia 1oo za pesa kabla ya kumaliza mkataba.

Kwa mujibu wa Waziri Sitta anasema pesa ziingetakiwa zilipwe kwa mafungu yaani asilimia 50 za kugiza na asilimia 50 iliyobaki ingelipwa pale mabehewa hayo zaidi ya 200 kuwasili na kuyajalibu kama yanafaa au la.

Watendaji wa TRL waliosimamishwa na Waziri Sitta ili kupisha uchunguzi ni Mkurugenzi Mtendaji, Kipallo Kisamfu, Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomiles, Mhasibu Mkuu, Mbaraka Mchopa, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiraga na Meneja Mkuu wa Manunuzi wa kampuni hiyo, Ferdinand Soka.

Chanzo kingine kinasema kitendo cha Rais Kikwete kumtoa waziri Mwakyembe wizara ya uchukuzi kunatokana na kujilidhisha pasipo na shaka waziri huyo alihusika na kuleta mabehewa hayo mabovu.

"Sikufichi Yule bwana, Kikwete kamuokoa sana maana alijua kwa umakini wa vyama vya upinzani wasingekubali na wangelipeleka suala lile Bungeni na yangefichuka mengi sana maana ufisadi ni mkubwa sana na amgusi waziri huyo wako wengi sana,wewe unafikili hata huyo Mwigulu angepona naye? naye angeisha tu pesa hazitoki bila wizara ya fedha kulidhia".

Kwa upande wake naye Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila ameumbia mtandao huu kwamba Malipo ya Bilioni 23o kwenye kampuni hiyo ya India hayawezi kutolewa bila idhini ya kikao cha baraza la mawazili na anadai kama ingekuwa nchi makini hapa kungetakiwa hata waziri mwakyembe pamoja na katibu Mkuu Wizara yaUchukuzi wangefukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.

"Bilioni 230 zinapotea hivyo sio pesa ndogo haiwezekani watendaji hao wandogo waidhinishe pesa hiyo bila waziri Mwakyembe kujua na hata Katibu mkuu uchukuzi bila kujua kama kungekuwa na serikali makini sana hata wasingebaki hata ki
 
Mtaalam wa majungu, hebu fuatilia nani alianzisha uchunguzi wa hilo sakata, ili ukate kiu yako ya junguzz!!
 
Haya sasa hizo ni Bil 230, hapo juzi tumetoka kwenye kashfa ya Bil 320, Ule wa Epa ulikuwa Bil 130, Richmond Ths.130kila siku kwa mwaka mmoja, RADAR Bil 40.....!!!!!

Halafu kuna watu wanasimama mbele ya kadamnasi na kudai ati nchi hii ni maskini na kwamba hawajui umasikini huo umesababishwa na nini...!!!

Kazi kwelikweli

BACK TANGANYIKA
 
Wanakusanya Pesa za Uchaguzi 2015 ,unadhani kuhonga Kanga siku ni dili.
Wapiga kura wameshakuwa wajanja wanataka hadi simu za Kichina kwa hiyo unaweza kuona kiasi gani wa pesa zinahitajika.
 
Yerricko umeleeta habari nzur sana! Ninachoona hapa hata kama waziri angekuwa msafi vp ni hawa ccm wanatafuta hela za kampeni

kwa ujumla mkataba wowote ambao utafanywa na wizara lazima fungu la kampeni iwepo!

Tuendelee kupashana habari!!!!
 
Taratibu za manunuzi huanzia kwenye kitengo cha manunuzi cha taasisi ya serikali. Halafu inakuja bodi ya zabuni na mwisho bodi ya wakurugenzi ya taasisi kama vile TRL.
Hadi hapo waziri anaambulia kupokea taarifa tu.
Kwa waziri anayefuata taratibu za kisheria za utendaji serikalini kama Mwakyembe hapo hawezi kuhusika kabisa.
 
Imekaa kituhumatuhuma pia. Huenda uchunguzi utakapokamilika tukajikuta tunalaumu tume kwa kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa. Kwa Mwakyembe ni ngumu kukwepa hata kama binafsi hakuweka mkono. Muhimu ni ukweli kwamba lazima awajibike nalo kwani madudu yalifanyika katika himaya yake.
 
Mtaalam wa majungu, hebu fuatilia nani alianzisha uchunguzi wa hilo sakata, ili ukate kiu yako ya junguzz!!

Nımekubali kuwa kuna baadhi ya mada tunazıjadili huku tukijiamini sana kumbe ukweli unakuwa ni mwingne.Watendaji aliowataja Sita walishasimamishwa na Mwakyembe baadhi yao.Mhandisi mitamba alıshasimamishwa siku nyingi na kamati ya uchunguzı ılishaundwa toka enzi za Mwakyembe.
 
Ikiwa maelezo yako ni hayo sidhani kama yanamtia hatiani waziri. Katika mfumo wa utawala, waziri hahusiki popote katika malipo, na hata kuidhinisha malipo. Labda ungenema katibu mkuu. Ingawa ni kweli kwa fedha nyingi namna hiyo kulipwa zote kwa wakati mmoja kinyume cha mkataba lazima kuna mtandao wa wakubwa wengi wanaohusika na hasa ndani ya wizara ya fedha.
 
Hivi TRL wana uwezo wa kuwa na Bilioni 230 za kuwalipa wahindi?

kama wangekuwa na financial capacity hii sidhani kama wangekuwa walipo. Mtoa tuhuma tazama figures zako vizuri.
 
Haya sasa hizo ni Bil 230, hapo juzi tumetoka kwenye kashfa ya Bil 320, Ule wa Epa ulikuwa Bil 130, Richmond Ths.130kila siku kwa mwaka mmoja, RADAR Bil 40.....!!!!!

Halafu kuna watu wanasimama mbele ya kadamnasi na kudai ati nchi hii ni maskini na kwamba hawajui umasikini huo umesababishwa na nini...!!!

Kazi kwelikweli

BACK TANGANYIKA
Dear American friends, first and foremost, I would like to admit that I have no clue as to why my Country Tanzania is poor but what I know, without any doubt, is that your country is rich and therefore I am here to ask for your help. 😂😁😁😁

Halafu hapa home,
Ndugu wananchi, ninataka niwahakikishieni ile pesa ya escrow sio ya umma!
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1429371910.470214.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1429371910.470214.jpg
    33.1 KB · Views: 495
Taratibu za manunuzi huanzia kwenye kitengo cha manunuzi cha taasisi ya serikali. Halafu inakuja bodi ya zabuni na mwisho bodi ya wakurugenzi ya taasisi kama vile TRL.
Hadi hapo waziri anaambulia kupokea taarifa tu.
Kwa waziri anayefuata taratibu za kisheria za utendaji serikalini kama Mwakyembe hapo hawezi kuhusika kabisa.

Yaaani Kupokea mabehewa anahusika ila kwenye malipo ndo hausiki sio?
 
Wanakusanya Pesa za Uchaguzi 2015 ,unadhani kuhonga Kanga siku ni dili.
Wapiga kura wameshakuwa wajanja wanataka hadi simu za Kichina kwa hiyo unaweza kuona kiasi gani wa pesa zinahitajika.

Mkuu...cjui umewaza nini kwahiyo wapigaKURA nao wako kiDijitali wanataka kuwa kwenye FESIBUKU....kwanamna. hiyo....Lazima Nchi ifiliske
 
Back
Top Bottom