Ufisadi unavyotufukarisha watz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi unavyotufukarisha watz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babalao 2, Oct 3, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,271
  Trophy Points: 280
  Katika kitabu "AFRICA'S ODIOUS DEBTS": HOW FOREIGN LOANS AND CAPITAL FLIGHT BLED A CONTNENT.

  Kimeweza kuweka wazi ni jinsi gani UFISADI umedidimiza taifa letu. Kwa kifupi ni kwamba kati ya mwaka 1970 - 2010 kiasi cha Dola za kimarekani 11.4/ bilioni zimetoroshwa nje kutoka Tanzania. Hii ni pesa ambayo imetoroshwa kwa njia mbalimbali na wahusika ni Wawekezaji, wanasiasa, watendaji, maofisa wa jeshi, Usalama wa Taifa na Wafanyabiashara.

  Kiasi hicho kingeweza kujenga km 800 za barabara za lami kwa kila mwaka mmoja na kwa gharama za sasa kwa tanzania yenye mtandao wa barabara wa km 85000 tungekuwa tumesogea mbali. Au angalau kuweka umeme kwa vijiji 1300 kwa mwaka tena kwa mikoa iliyo mbali na grid ya taifa kwa kila mwaka mmoja na hyo ni 10% ya vijiji vyote tanzania.

  Kwa mtindo huu umepelekea kuwa na watu wachache yapata 30% kumiliki 75% ya pato la taifa. Je hawa 70% ambao ni mafukara kumiliki 25% ya pato la taifa ni haki au yote hii ni kufukarishana tu. Watunga sera za madini gesi na mafuta wote hawa wamegeuka wanyonyaji kwa kuweka sera zinazowajali matajiri na kuwasahau wananchi wa kawaida.

  Kumbuka ufisadi mkubwa umefanyika baada ya tafiti za uranium, gesi na mafuta kuanza. Tuache uwoga tutetee rasilimali zetu wenzetu siera leone wametoa amri kurejeshwa kwa mali na fedha zilizofichwa nje ya nchi yao na wameanza utekelezaji wenye mafanikio makubwa. WOGA NDIYO UFUKARA WETU.
   
 2. J

  Joyfull Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very true this is very bad we should have confidence
   
 3. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Nani wa kumfunga paka kengere, wacha siku yao inakuja na wala haitakawia
   
 4. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe acha tu tunaamka japo polepole mno. Tutawapiga mapanga hivi karibuni. Hizo hela watakufa wala familia zao hazitafaidi chochote. Waache wachekelee tu siku yaja!
   
 5. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kuna mzee mmoja aliniambiaga nje kuna zaidi ya hizo dola 11.4 billion. kipindi cha mwinyi kuna wahindi walikula fedha za misaada na mpaka fedha za bajeti. kuna watu tanzania wana migodi yao binafsi na hawalipi kodi na fedha zote zinaenda nje..
   
Loading...