Ufisadi una msaada kwa jamii. Tuwe wakweli

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2019
Posts
1,949
Reaction score
4,425
Ufisadi japo wengi wanauponda ila mimi binafsi naona una msaada kwa kiasi flani. Ni watu wachache sana Tanzania hii wanauwezo wa kumiliki bilioni 5.

Mtumishi wa umma au Mwanasiasa akipiga bilioni 5 anaweza hata kujenga hoteli watu wakapata ajira. Hizo pesa za ufisadi zinaweza hata kuanzisha makampuni yakatengeneza ajira kwa watu wengi.

Binafsi naona ufisadi unasaidia kwa kiasi flani.
 
Yaani unatetea mtumishi wa umma au mwanasiasa apige bil. 5 ili afanye investment ambayo hana uzoefu nayo? unajua ni watu wangapi wameathirika kwa kukosa dawa au kwa kupita kwenye barabara yenye mashimo? serikali inao uwezo wa kutengeza mabilionea kwa kutumia wafanyabiashara au wawekezaji waliopo kwa kuwapunguzia au kuwasamehe kodi nk. na siyo kwa watumishi au wanasiasa kukwapua pesa za umma.....umeleta hoja ya kipuuzi ndugu.
 

Its not that serious mkuu. Acha pesa isambae
 
Its not that serious mkuu. Acha pesa isambae
Aliyekwambia pesa inasambaa kwa watu wachache kukwapua ni nani? serikali inaweza kuongeza matumizi kwenye miradi yake (government spending) na hata kuongeza ajira na mishahara ya watumishi na pesa ikasambaa mitaani na siyo kwa watu wachache kuiba, bado unaendelea kutetea utopolo, wewe utakuwa fisadi unayetaka kuhalalisha ufisadi wako kwa kutafuta support ya members humu.......hovyo sana.
 
Na hapo unaweza kukuta ana degree. Hii nchi kazi ipo, yaani Mtu anaamini uchumi wa nchi utajengwa kwa kuiba pesa. Astaghfirullah astaghfirullah astaghfirullah......
 

Asilimia kubwa ya watanzania ni wezi,wanao dai uzalendo ni kwamba awaja shilikishwa kwenye mgao.
 
Itategemea kama fisadi atakuwa na wazo hilo! Wengine walimbikiza nje ya nchi.
 
Hizo pesa zitakazoibiwa zitakosesha maendelea mengi na makubwa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…