Ufisadi TRA mpakani

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Waziri ashuhudia uozo TRA mpakani

2009-04-21 21:25:42
Na Mwandishi Wetu


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Ngara, imepewa siku 21 kutoa idadi ya magari yanayosafirisha mafuta kwenda Rwanda na Burundi kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala, alitoa agizo hilo baada ya kuchanganywa na taarifa za idadi ya magari yanayosafirisha mafuta kupitia vituo vya ushuru forodha vya Kabanga na Rusumo.

Dk Kamala alisema alifikia uamuzi huo baada ya kufanya utafiti wa uliomsaidia kubaini udanganyifu unaofanywa na maofisa wa forodha kuhusu magari yanayopita vituoni hapo.

Baada ya kupewa takwimu ya magari kwa mwezi kwenye vituo hivyo, alibaini kuwepo tofauti na zile alizopata kutoka kwa maofisa wa forodha Rwanda Kituo cha Rusumo.

Alisema alibaini idadi kubwa ya magari yanayopakia mafuta yanayopita Bandari ya Dar-es-Salaam kuelekea Rwanda na Burundi hayafiki, bali yanauzwa njiani.Dk Kamala alisema kinachofika mipakani ni makarasi kwa ajili ya kugongwa mihuri ofisi za mapato kwa ajili ya kumbukumbu.

``Haiwezekani takwimu zikatofautiana, magari yanayotoka Bandari ya Dar-es-Salaam kuelekea nchi za Rwanda na Burundi yanaonekana mengi yanapofika mipakani ni machache, jamani hiyo inamaanisha nini?``alihoji

Alisema taarifa ya Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Rusumo, Epaphras Makoko, kuhusu takwimu za magari hayo inatofautina sana na ile ya Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato ya Rwanda, Shwaka Alex, Kituo cha Rusumo upande wa Rwanda.

Alex alisema kwa mwezi ni wastani wa magari 30 yanayopita, huku Kaimu afisa forodha upande wa Tanzania anadai ni magari 100.

Waziri Kamala alihoji chanzo cha kutofautiana kwa takwimu hizo na kutaka uongozi wa vituo vya forodha vilivyoko Ngara kuandaa taarifa kuanzia mwaka 2005 hadi sasa.

DK Kamala alisema kitendo cha maofisa wa TRA kushirikiana na wajanja wachache, ni kibaya kwa sababu wanatia hasara serikali.

``Sikuja kutembelea vituo hivi kwa kubahatisha, nimekuja baada ya kuelezwa mchezo mchafu unaofanywa na maofisa wa TRA wa kutumia nafasi zenu kufanya ubadhirifu``alisema.
 
Back
Top Bottom