Ufisadi TPDC na Songas

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
%28TPDC.jpg

HARUFU ya ufisadi imeonekana kwenye Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni ya kuzalisha umeme kwa gesi ya Songas, ambayo shirika hilo lina hisa.

Akisoma ripoti yake mbele ya waandishi wa habari jana, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad, alisema katika mwaka wa fedha 2014/2015, Songas ililipa gawio la dola za Marekani milioni 3.9 kwa TPDC.

“ Hata hivyo, katika mapitio ya vitabu vya hesabu vya Songas vinavyoishia Desemba 31, 2014 vilivyokaguliwa, tulibaini kuwa Songas ilitangaza kulipa gawio la dola za Marekani milioni 15.

“Kutokana na TPDC kuhodhi asilimia 29 ya hisa katika kampuni ya Songas, ilipaswa kupokea kiasi cha dola za Kimarekani milioni 4.35. Hii inaamanisha kuwa, kiasi cha Dola za Marekani 477,000 sawa na Sh. milioni 965 hazikulipwa kwa Shirika kama gawio kutoka Songas,” alisema.

Alisema pia kuwa kutokuwepo kwa bodi za mashirika ya umma imekuwa changamoto nyingine aliyokutana nayo, ambayo katika mwaka wa ukaguzi wa 2014/15, kulikuwa na mashirika 22 ambayo hayakuwa na bodi za wakurugenzi, hatua ambayo ilisababisha taasisi husika kukosa usimamizi.

Alisema pia wamebaini udhaifu kwenye kurejeshwa mikopo inayotolewa na Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), iliyotolewa chini ya mpango wa kusafirisha bidhaa nje kwa dhamana ya Serikali.

“Benki ya Maendeleo ambayo ni Benki Tanzu ya Benki ya Rasilimali Tanzania, inaidai Kampuni ya Agricultural and Animal Feed Industry (SAAFI) Sh. bilioni 2.5, ilizoikopesha kwa ajili ya kuiwezesha kampuni kulipa mkopo wa Sh bilioni 15 uliotolewa na serikali kupitia mpango wa
kusafirisha bidhaa nje kwa dhamana ya Serikali.

‘Kiasi chote cha Sh bilioni 17.5 hakijareshwa kwa zaidi ya miaka 10 sasa, kwa kuwa utendaji wa kampuni ya SAAFI haukuwa wa kuridhisha. Benki ya Rasilimali Tanzania iliamua kuubadilisha mkopo huo kuwa asilimia 20 ya uwekezaji wa benki katika kampuni hiyo.

“Menejimenti haikutoa maelezo ya kuridhisha juu ya vigezo vilivyotumika kumiliki asilimia 20 tu wakati sehemu kubwa ya mali za Kampuni hii zimepatikana kwa mkopo wa serikali,” alisema.

Alisema kampuni zingine tano zilikuwa na deni katika mpango huo lenye thamani ya Sh bilioni 45.71.
Alisema kampuni hizo ni Arusha Blooms Ltd (Sh. bilioni 10.1), Kiliflora Ltd (Sh. bilioni 11.8), Tengeru Flowers Ltd (Sh, bilioni 7.5); na Mount Meru Flowers (Sh. bilioni 16.3).

“Ninaishauri Menejimenti ya TIB kufuatilia urejeshaji wa madeni haya na mengineyo ili kuepuka kudhoofisha utendaji wa Benki,” alisema.

Kuhusu Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), alisema amebaini kuwepo na malipo ya asilimia 90 ya fedha za mkataba bila kuwepo kwa dhamana.

“NDC iliingia mkataba wa kusanifu, kusambaza, kufunga, kupima na kuweka kiwanda cha uzalishaji wa viuatilifu na ujenzi wa maabara ya kibaolojia na kifamasia (LABIOFAM) wenye thamani ya Euro milioni 16.8.

“Lengo ni kupunguza malaria na matumizi ya serikali kwenye ununuzi wa dawa na gharama nyingine zinatokana na kupambana na malaria.

Ukaguzi ulibaini kuwa shirika lililipa asilimia 90 ya fedha za mkataba kwa LABIOFAM bila kuwepo kwa dhamana yoyote,” alisema.

Alisema pamoja na ufunguzi rasmi wa kiwanda uliofanyika Julai 2, 2015, hadi sasa kiwanda bado hakijaanza uzalishaji kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyobainika wakati wa majaribio ya mitambo siku chache kabla ya ufunguzi rasmi.

“Sambamba na gharama za matumizi mengine, NDC inalipa mshahara kwa meneja wa mradi ambaye yupo kwenye eneo la ujenzi wa kiwanda.

“Shirika pia lilianzisha Kampuni ya Tanzania Biotech Products ambayo imeajiri Zaidi ya wafanyakazi 130 ambao wanalipwa mishahara kila mwezi licha ya mradi kuchelewa kuanza uzalishaji,” alisema.

Alisema kutokuthibitishwa kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 600 kama mtaji wa Sichuan Hongda Ltd, Septemba 21, 2011, NDC, Sichuan Hongda (Group) Company Limited na Tanzania China International Mineral Resources LTD (TCIMRL) walitia saini mkataba wa ubia wa kuendesha Tanzania China International Mineral Resources Ltd, ikiwa ni kampuni iliyoanzishwa ili kutekeleza mradi wa Mchuchuma na Liganga.

“Sichuan Hongda (Group) Company Ltd ilikubali kuchangia kiasi cha dola za Marekani milioni 600 kama mtaji kwa TCIMRL ili zitumike kwa ajili ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi.

“Hata hivyo, nilibaini hapakuwepo na utaratibu uliowekwa wa kuweza kuhakiki na kuthibitisha kiasi cha pesa kilichotolewa na Hongda hadi sasa kama sehemu ya mtaji iliyokubali kutoa.

“Baada ya kupitia mkataba wa ubia ilibainika kwamba, Sichuan Hongda (Group) Company Ltd inamiliki asilimia 80 ya hisa za TCIMRL wakati asilimia 20 inamilikiwa na Shirika la Maendeleo la Taifa. Bado uchangiaji wa ziada wa kiasi kisichozidi dola za Marekani bilioni 2.4 utadhaminiwa na mali za kampuni ya ubia zikijumuisha haki za uchimbaji badala ya rasilimali za Hongda Sichuan (Group),” alisema.

Alisema umiliki wa asilimia 20 wa NDC ndani ya TCIMRL haujahusisha ukweli kwamba mkopo huo unadhaminiwa na mali za kampuni ikiwemo haki za uchimbaji.

Source: Nipashe
 
Fedha nyingine itapatikana kutokana na vyanzo hivi kusaidia bajeti 2017/2018 kama hizi takwimu zitadhibitishwa!
 
"Senkiyuu veree macheee,wanaosema ndiyo na waseme...ndiyoooo "
 
Back
Top Bottom