Ufisadi serikali ya wanafunzi mzumbe dsm campus | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi serikali ya wanafunzi mzumbe dsm campus

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yo Yo, May 25, 2012.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Wanamzumbe naomba niwasalimu kabla ya kuwahabarisheni yale msiyoyafahamu, kuna WIZI na UFISADI mkubwa umetokea katika pesa zetu tunazochanga kama ada ya association, Siwezi pita vumbi wakati lami ipo....Raisi ambaye anatakiwa kuondoka madarakani anafahamika kama MOSES MOMBA(DISSERTATION) amekwapua fedha taslimu 32,000,000(wanafunzi 1600 ada 20,000) katika akaunti na ushahidi ukiwepo. Rais huyu anafanya mambo mengi ambayo inasemekana anasapotiwa na menejiment mfano mzuri huwa ana tabia ya kuwatukana classreps pale anapoletewa matatizo..............je unaweza kuamini darasa moja msimbazi huchanga pesa kwa classrep ili aje kuchukua matangazo UPANGA!!!!!!!!!!!!!!!

  Hakuna chuo kina matatizo Dar kama Mzumbe, hakuna chuo wanafunzi wanateseka kama mzumbe, hakuna library ya kutosha,hakuna bookshop, hakuna sehemu za kusomea,hakuna stationary za kutosha,hakuna AC za kueleweka,msimbazi ndio kero wanafunzi wamekuwa kama watumwa wa ada(mamilioni) wanayolipa.....tulitegemea pesa yetu ya MUSO iweze kutufuta machozi ila mtu mmoja (MOMBA) akishirikiana na mmoja kati ya lecturers wa menejiment wametafuna pesa zetu...

  Je unamfahamu FRED NGAJIRO...huyu ndie mwanafunzi aliyeshinda urais kwa kishindo ili ampokee momba kijiti ila mpaka leo hajaapishwa!!!!!!!!!!!!!! Je unajua sababu,,,,,,,,Ngajiro ni mwanaharakati mzuri sana na mpinga ufisadi aliahidi kuweka kila kitu sawa ila inasemekana haelewani na MOMBA na ndio sababu hataki kumuapisha kisa mtu aliyemuweka yeye anaitwa JOHN D. NGOWI ambaye alishindwaSi unajua gari linalovutwa haliwezi kuovertake....NGOWI alikuwa mshindi wa tatu ila aliappeal matokeo kwa kushinikizwa na MOMBA kuwa atapewa URAIS kwa sharti la kutochunguza shillingi 32,000,000...Hivi sasa Ngajiro anaishi kwa vitisho vikubwa na manyanyaso mengi maana hili linasemekana kwa habari zisizo rasmi linasapotiwa na MBWAMBO...sasa hatujui kama mkuu nae ni mshiriki katika huu mchezo...

  KWANINI RAIS TULIYEMCHAGUA HAAPISHWI MPAKA SASA,SIKILIZA, Menejiment ina buy time ili tumalize mitihani wamuapishe JOHN NGOWI...wanataka kuweka Rais wao sasa kwanini walitupotezea muda wa kupiga kura...NDUGU zangu sisi ni wasomi tukikubaliana na hili tutakuwa hatujitendei haki,Classreps tunawatesa ilibid wapewe hata allowance ya vocha tu ambayo ni ndogo sana........Momba aliilipa electro cometteeya watu watatu sh 30,000 kila mtu na alitoa hela kwenye walet, je pesa ya umoja ndio inatolewa bila kusainiwa? NDUGU unaijua hiyo bajeti aliyosema ilitumika!!!!!!!!!!!!!!!!!AIBU AIBU AIBU TUPUUUUUU!!!!! Mimi ni mmoja kati ya classreps ndio maana najua uchungu wa ile pesa yetu....MOMBA amekula pesa ya intake yao 2010 amekula yetu ya 2011 na kuna uwezekano anataka kula na ya 2012....je huu woga ni halali yetu watu wa level ya masters!!!!!!!!!!!!!!!!!

  WATU WALIFELI SANA SEMESTER YA KWANZAila momba alisaini matokeo bila kubisha kisa sisi sio classmates wake,alikubali sera ya kulipa vitabu kisa yeye hakuchajiwa maana alikuwa dissertation,alikubali wenzake wakapangiwa dissertation supervisors wa morogoro na mpaka leo wanalia maana wanaishi Dar, tunadai hela za vitabu 250,000 huwa hana hata time....MTU HUYU HANA TOFAUTI NA UKIMWI maana ANAUA BILA AIBU..NGAJIRO Alipambana sana na matatizo akiwa classrep MBA wote ni mashaidi na mimi binafsi ameniahidi yote haya ni madogo atayasolve,Jamani NGAJIRO atakuwa na uchungu na sisi maana tumemchagua.....nlimuuliza Jana Ngajiro ameuchukuliaje huu uonevu akajibu hivi``CALAMITY IS A TOUCHSTONE OF A BRAVEMIND, NILIANZA NA MUNGU NA NITAMALIZA NA MUNGU”....hii statement ni ya kijasiri ila inaonesha anakosa kampani ya watu anaotaka kuwatatulia matatizo yao........

  Jamani tusipomuapisha raisi wetu tutegemee disco na sap za kutosha semester hii,tutegemee kupangiwa supervisors wa morogoro na kutorudishiwa 250,000 za vitabu,,,Ngajiro alishinda kura madarasa yote ya msimbazi yaliyopiga kura Je aliwapa Rushwa?.hakuna mtu hata mmoja ambaye alifika nusu yake katika urais sasa appeal zinatoka wapi...

  Wenzetu wa procurement saa10 hawakupiga kura kwa sababu kubwa MOMBA aliwadharau siku ya uchaguzi pia aliwaambia HATA WASIPOPIGA KURA WATATAWALIWA TU ila yeye amelipotosha hili,poleni sana ndugu ila naamin Ngajiro might sound the best...MOMBA aliwahi kusema WANAWAKE WA MZUMBE NIWACHAFU SANA(wengine ni mama zake kabisa) mbele ya darasa la MPA ya asubuhi na wote ni mashahidi na ndio sababu wanamchukia...

  RAI YANGU KWENU naomba naomba tuwe pamoja kwa hili ikiwezekana kumface MBWAMBO tuhakikishe Ngajiro anaapishwa kabla hatujaanza mitihani,MOMBA ashughulikiwe na wabunge ambao ni maclassrep...Huyu Ngowi asemwe kwa Busara na uwazi maana anatusaliti wenzake tulioingia intake moja...wagombea wote walioshindwa hawana shida na Ngajiro kasoro huyu kibaraka wa Momba
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,912
  Trophy Points: 280
  hongera zao kwa kuanza ufisadi wakiwa watoto, pesa ambazo mnachanga ila hampewi tathmini ya kwamba zilitumikaje ni kitu cha ajabu sana
   
Loading...