wimbi la mbele
JF-Expert Member
- Jan 4, 2011
- 647
- 266
Weekend hii nilikuwa nafanya mzunguko nilitembea kwa gari hadi Oysterbay maeneo ya cocobeach, wakati narudi nikapita njia ambayo kisheria hairuhusiwi namimi sikujua kama hairuhusiwi kupita njia hiyo. Njia hiyo ni ile ya pale anapoishi Waziri Mkuu, askari aliyekuwa amebeba bunduki akanistopisha na kusema niteremke ndani ya gari nikaandike statement na sikuwa mimi peke yangu niliyepita kwa njia hiyo bali wengi tulipita njia hiyo na tukakamatwa.Kila mtu kaomba msamaha lakini hakuna aliyesamehewa, Kumbe nia ya hao askari ni kuomba rushwa ili wakuachie na karibia watu wote tuliopita njia hiyo walitoa rushwa kwa hao askari ndio wote tukaachiwa. Jamani hawa askari wetu mbona njaa itawaua maana inatia aibu sana.
U-turn naomba uipublish hii ili wakae watambue kuwa wanavyofanya sivyo,
Asante,
Mange naomba uifiche email yangu tafadhali.
Omg, this happened to me,nilikuwa natoka Golden Tulip ,si mnajua kile kifoleni cha pale coco beach siku za jumapili,so nikaamua kukata short cut, kumbe ile short cut bwana ni nyumbani kwa waziri mkuu hapo hapo nikasimamishwa na askari waliobeba bunduki, nikajaribu kuwaambia kuwa sikujua na sikuona alama yoyote inayosema kuwa siruhusiwi kutumia barabara hii, kwani walielewa wakaniambia haya geuza twende kituoni, ilibidi niongee nao kiutu uzima ndo wakaniachia nikaondoka.(naogopa kuongea details nsije nkaji incriminate,maana nasikia mpokea rushwa na mtoa rushwa adhabu ni ile ile)LOL
Really this has to stop especially cos inatokea nyumbani kwa waziri mkuu.
Mange
U Turn Blog