Ufisadi NHIF

Tumesikia ya ATCL makubwa na yanayohatarisha maisha ya watu , hakuna hata mkuu mmoja wa serikali aliyesimama kidete na kuisafisha manejiment au kuikemea ...

Tumesikia ya Benki ya Posta juu ya ubadhirifu na JINAI ya kughushi laikini hakuna hata kiongozi si wa shirika lenyewe,wizara au kiongozi wa ngazi za juu hata za kati kuwasafisha watendaji au kuwauliza ili watoe majibu...Imeongezeka tena ya kuwa Benki ya Posta imetumia zaidi ya DOLA za kimarekani Thelathini na tano elfu (35,000.00) karibu shillingi millioni arobaini na tatu kumpeleka india kwa ajiri ya kuchunguzwa afya makamu mwenyekiti wa BODI ambaye si mtendaji wala si mwajiriwa wa benki ya posta... Akiongozana na MKEWE pamoja na Nurse wote wakilipiwa kwa wiki mbili...hata kujiuliza kazi ya nurse kutoka Tanzania itakuwa ni ipi na kazi ya mke itakuwa ni ipi... KIMYA KIMYA serikali kama haipo...
na mengine mengi mengi... wako kimya kabisa kama hawaoni wala kusikia

Haya ya Bima ya afya yameibuka...nafikiri tuanze kupima IQ za wanaoomba uongozi Tanzania,si dhani kama viongozi wetu wengi wanao uwezo mzuri wa kufikiri bila kuwategemea washauri
 
Karibu Afisa Usalama katika Jf,

Usishangaa sana sababu hata Maafisa wa Usalama wanajua hili,Ndiyo Hata Mwanakijiji alishawahi kuhoji je kuna ulazima wa TISS kuendelea kuwapo kama kuna mambo kama haya yanaendelea na wao bado wanaangalia.Tatizo ni Mkurugenzi au?
 
Nimesoma hii story nikasema Mungu ibariki Tanzania. Hapa nimechoka mwenyewe. Kwanza NHIF staff asante sana kwa kuleta hii habari hapa JF, tutajaribu kadi tuwezavyo kuisimamia katika koo.

Invinsible naomba hili swala kama inawezekana liwe sticky on top. Nadhani hili swala linausu familia nyingi Tanzania, hili swala linawagusa walimu wa msingi na sekondari ambao wanalisha knowledge kwa vijana wetu.

Kwanza kabisa nadhani Mkurugenzi wa huo mfuko(portfolio) hafahamu kabisa swala zima la kuendesha insurance. Kwanza ningeomba maelezo ya swala zima la PREMIA, jee ni the same as premium? na kama ni sawa na premium jee kabla hawaja adopt hii system wamefanya research ya aina gani kujua ni watu gani wanachongai mfuko? Jee wana health condition za aina gani? Jee wana umri unao range vipi? Lengo zima la kufanya hii ni sababu premium payment haziwezi kufanana, kwani ni less likey kijana wa miaka 25 kulipa sawa na mzee wa miaka 50 sababu wote wana demand tofauti katika swala zima la afya.

Katika maelezo imeonyesha mkurugenzi anajifanya yupo immuni na system ambayo wote mlikubaliana. Invyoonekana mfumo ulitengenezwa kama HMO yaani Health Maintentenance Organization, mfumo unamtaka mshiriki katika mfuko kuwa na access ya baadhi ya hospital ambazo zimekubaliwa na mfuko. Basi kama hiyo ni agreement ya kwanza, hakuna anayetakiwa kuwa above the law, yaani mfuko hauwezi kudhamini mtu yoyote kutibiwa nje au kutibiwa kwenye hospital zisizo katika makubaliano na mfuko.

Ili tupate ufahamu zaidi jee unaweza tuambia huu mfumo wa premia ni nini hasa? Maana sielewi kwa nini kununuliwe mfumo? Insurance kazi yake ni kukusanya pesa na kuziwekeza kwenye liquidity asset ambazo ni rahisi kuzigeuza kuwa cash. Swala ambalo linatakiwa liangaliwe na watu wenye mueleo wa juu wa maswala ya usimamizi wa fedha. Sasa nisicho elewa ni kwanini kuwe na mfumo wa kununuliwa kutoka India?

Hii inatokana na kuwa na viongozi mbumbu wasio kubali kwamba hawawezi kuongoza. Kuchukua mwalim kutoka IFM does not mean kwamba ana knowledge ya kufanya investments kwenye sector ya insurance.

Kuonyesha ni jinsi gani viongozi wa huo mfuko hawana strategic plan ni kwa kuwakubalia wananchi kutumia pesa zao kisha kufanya claim at the end of the day. Jee ni kwa nini hawakuweza kuasign hospital na kisha kunegosiate na hizo hospital kwenye costs.

Nashindwa kufahamu huu mfuko ni Insurance portfolio au ni some kind of mfuko ulianzishwa ili watu wapate kuwaibia masikini? sababu characteristics zake ni za insurance lakini matendo yake ni ya kifisadi. Jee ni kwa nini wachangie ujenzi wa dhahanati ya Amana? Jee wana mfuko wanafaidika nini baada ya swala hilo? Jee premium zao zitashuka au?

Mkuu wa NHIF ulioleta hizi habari naomba uridi tena hapa jamvini kwa more clerification. Sababu naona huu ni wizi wa wananchi, ni unyanyasaji wa Watanzania, ni ubabe usio na kikomo.

JK hapo mwanzo alisema Hari mpya na kasi mpya, maisha bora kwa kila Mtanzania. Sasa swala langu ni moja kwa washauri wa JK. January Makamba naomba umuulize JK ya kwamba jee kuna maisha bora kwa kila Mtanzania kwenye swala hili. Kama serikali inashindwa kuwatetea walimu wa Shule za msingi kule Maweni, Muheza, Shelui, Kibaoni, Kibondo au kule Mkange jee serikali hii itamtetea nani? Jee haki iko wapi?

Mama Kikwete yeye alishakuwa mwalimu, jee unalionaje swala zima kama hili? Wakati wewe na wenzio kina mama Lowassa mnatumia Class A government Health Insurance hebu fikiria hawa wavuja jasho wanaongoza uchumi wa Tanzania, wavuja jasho wanafundisha majority ya Watanzania kusoma na kuandika.

Najua JK and associate wanapita hapo every day, naomba hili swala liwe challange kwa wote, najua January Makamba unatazama hapa, nakupa hili swala kama challange kwako, nafahamu kuna wawakilishi wa wizara ya afya wanachungulia hapa, nao nawapa hili swala kama challange kwao. Waziri Pinda saidia watanzania hawa. Tumeshindwa kuwakamata EPA, BUZWAGI, RICHMOND and Kiwira, Jee tutashindwa kuzuia swala linalo wagusa Watanzania wengi wa vijijini kama hili? Wapi moral wa Watanzania kwa ajiri ya Watanzania? Wapi watatezi wa wanyonge? Wapi Haki kwa wote?

Mungu ibariki Tanzania
 
Dalili ya mvua ni Mawingu, na mti wenye matunda hutupiwa mawe!!!!









 
Usishangaa sana sababu hata Maafisa wa Usalama wanajua hili,Ndiyo Hata Mwanakijiji alishawahi kuhoji je kuna ulazima wa TISS kuendelea kuwapo kama kuna mambo kama haya yanaendelea na wao bado wanaangalia.Tatizo ni Mkurugenzi au?

Mkuu Gembe,

Heshima mbele, hivi karibuni tulikuwa kwenye kufuatilia ile topic ya kumtaka mkurugenzi wa sasa ajiuzulu kama tulivyokuwa tumeahidi, mkuu tuliyoyagundua according to the dataz ni aibu tupu, ni kwamba yule mstaafu kumbe alichofanya ni kumuachia mkuu wa sasa cheo cha jina tu, kumbe yule mstaafu mpaka leo bado anai-run ile idara kwa manufaa yake binafsi na kikundi chake flani,

Matokeo yake ni kwamba huko ndani sasa kuna division kubwa, kati ya wenye nguvu na wasiokuwa nazo, ukweli tulioupata ni kwamba huyu wa sasa hana uwezo wa kufanya kitu chochote, na kwa mara ya kwanza tunaendelea kupata picha kamili ya ushiriki wa mstaafu wa idara kwenye kuwapa mtandao madaraka, kumbe ni wao wawili yeye na mkapa ndio waliohusika hasa, na huyu mstaafu ndiye hasa aliyekuwa a link kwa kuwa nduma kuwili kwa sababu kumbe kuna watu waliokuwa wakirekodi vikao vyake vingi vya siri kati yake na ra na el, kule Dodoma,

The bottom line ni kwamba ameiacha idara kwenye hali ngumu sana kikazi kwa sababu kuna wanaoendelea kumpelekea kila kitu kama vile bado ni bosi, na yeye ndiye anyeendelea kutoa maamuzi yote mazito, kwa hiyo ndugu zangu tunayo kazi kubwa sana as a nation, lakini hatutachoka hata siku moja, tutaendela kuzitafuta dataz na kuzifikisha panapotakiwa ili zifanyiwe kazi,

According to the more dataz... ni kwamba wabunge wengi wanasubiri kikao kijacho cha bajeti, moto utawaka sana!

Mungu Aibariki Bongo Yetu!
 
Wana JF wenzangu, mimi nawapongeza sana kwa kuanika uoza unaofanyika kutoka kila eneo hapa Tz.Nasikitika kwamba majority ya raia wanaishi katika maisha duni na watu wachache wanatumia hela ya walipa kodi kijitajirisha.Kibaya zaidi mafisadi hawa hawachukuliwi hatua kali na jamii yetu inazidi kuwa maskini.

Hatua ya kuwa expose ni moja ya hatua poa kabisa lakini kinachotakiwa hapa ni kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili wahukumiwe kwa uhalifu waliotenda dhidi ya jamii.

Sijaona concrete action towards mafisadi kutoka kwa vyombo vyetu vinavyosimamia sheria.Mafisadi yanawadharau watendaji wa serikali.Mafisadi yana uwezo mkubwa wa kifedha na yanakandamiza juhudi za wanajamii kutafuta haki.

Tunaipigia kelele serikali ichukue hatua thabiti lakini naona serikali imekuwa kibogoyo,haina meno.

Tutafika? Nani wa kutufikisha kwenye haki yetu?

Wale wenye dhamana ya kutulinda na maovu wako pamoja na timu ya mafisadi.Kama hawako na mafisadi basi wachukue hatua ya dhati ya kufanya "operation fagia ufisadi" na kuleta heshima kwa taifa.

Kama hizi ni ndoto za kufikirika basi na tukae na kuishi kama tulivyo.Tukubali kunyanyaswa na wenye fedha zilizopatikana kwa njia za uhalifu.

Sasa sijui hata naandika nini...nachanganyikiwa....mwisho wake hata sijui.Ewe Mungu iondoe nchi hii kwenye ufisadi uliokubuhu ili watoto wa Tanzania waishi kwa amani na salama.Amin.
 
Lazima tukubali kuwa ile idara sasa hivi haipo kwani mambo yanayofanyika yanawadhalilisha sana, na kama hipo basi wafanyakazi wake ni wazembe sana au kama wanafanya kazi sawasawa wanamdhalilisha mkuu wa kaya kwani inawezekana wanamshauri lakini yeye hawezi kuchukua hatua madhubuti kwa wakati mpaka SFO waingilie kati.
 
Kwa kweli issue imefika mahali pake...wanajamii tuipigie debe huyu anayejiita mkubwa aadabishwe. Issue za mfuko wa Bima ya Afya imekuwa ni wimbo kwa walimu na walala hoi. Vimshahara vyenyewe vya kubeep halafu vinakatwa kila mwezi kwa geresha kuwa watapata huduma bora za afya. Kila siku wakienda hospitali wanaishia kupewa viasprini na kuambiwa dawa hakuna wakati bwana mkubwa anapeleka wife nje ya nchi na hospitali za maana kwa kutumia hela hizo hizo za michango ya walala hoi........ Hii nchi Jamani, ukifikiria sana unaweza ukatoa mtu roho...................
 

Hili nalo inabidi liwekwe miguuni pa Kikwete.

Kikwete chonde chonde usiniangushe hata kwenye hili. Au unasubiria makachero wa nje waje kutusadia hapa pia?
 
Kinchosikitisha zaidi ni huyo mwanausalama wa taifa aliyegeuka kuwa fisadi anavyoshirikiana na mkurugenzi kuufilisi huo mfuko wa walimu walalahoi.
Inasikitisha na kukatisha tamaa kwa kweli.
 
kwani mafisadi wakitaka kula lazima watalazimisha mambo ili mradi wapate mahali pa kutafunia. Kwani ATCL imekuwaje watu wamelazimisha kukodi dege bovu ili wapate pa kula.
Utakapozungumzia matengenezo unatengeneza mpaka matumbo ya watu hata hili la Bima la afya ndio wale wale huenda hata huyo Humba anapata kiburi kuna mafisadi wakubwa wanamlinda....Iko siku yake naye tutamuweka sawa tu aeleze ukweli wa unachojua.....

Hivi Dr.Mwakyusa anayajua haya kama waziri mwenye dhamana au ndio wale wale funika kombe mwanaharamu apite???
 
Mkuu wa NHIF ulioleta hizi habari naomba uridi tena hapa jamvini kwa more clerification. Sababu naona huu ni wizi wa wananchi, ni unyanyasaji wa Watanzania, ni ubabe usio na kikomo.

Mtanganyika,

Tunashukuru. Tunasikitika kwamba Mkuu wa NHIF ameshindwa kurudi kwa wakati muafaka kuelezezea kwa upana yale ambayo ulikuwa umeyauliza ni kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wake.

Kwa siku tatu (3) zilizopita, NHIF Staff ameshindwa kabisa kuacess hii forum na amekuwa akijaribu mara kwa mara na kuishia kuambiwa kwamba User name na password ni incorrect. Sasa sijui kama huu ni ufisadi ndani ya Jamii Forum ama ni hali ya kawaida ambay oinawatokea watu wote.

Hata hivyo kuna usemi huwa napenda kuutumia kwamba, "Hata Punda Akifa Mzigo lazima Ufike!" kwa hiyo hili jukumu nalichukua mimi na kuhakikisha ya kwamba yale ambayo NHIF alitaka kuyaweka bayanayanawafikia.

Hatima ya Ufisadi huu lazima itafahamika na yale ambayo wanataka yafichike yatawekwa wazi!

Mpaka Kieleweke!
 


Pengine amesahau signature yake mwambie awasiliane na Admin au Invisible.

Thanks
 
Mods
Kuna wanaJF walipropose hii thread iwekwe sticky haapo juu ili isipotee hadi kieleweke
 
Nawashukuru wote kwamba nimefanikiwa kurudi katika Forum. Naomba niongezee haya yafuatayo katika mjadala mzima wa Ufisadi unaoendelea hapa NHIF.


"Awali ya yote napenda kuwashukuru wana JF wote kwa mchango wenu katika mjadala huu. Mmetupa moyo sana na hamasa kubwa na hivyo kudhihirisha kuwa wapo watanzania wenzetu katika maeneo mbalimbali ya dunia wenye uchungu na nchi yao. Asanteni sana. Pia kwa namna ya Kipekee na namshukuru ndugu Field Marshal ES kwa kufikisha kilio chetu katika mamlaka ya juu zaidi.

Mtusamehe kwa kuwa hatujaonekana tena tangu tuwalishe malezo yetu juu ya ufisadi wa NHIF unaongozwa na Humba! Tangu tumeandika JF juu ya ufisadi wa NHIF bwana Humba ameitisha kikao cha ‘management' na moja ya mambo waliojadili ni juu ya kuanikwa kwa udhaifu wake wa kioungozi. Alianza kwa kukurupuka kusaka vielelezo vya "Baraka" za wizara kumruhusu mkewe kutibiwa nje ya nchi kwa gharama ya Mfuko! Itakumbukwa,kama nilivyoeleza awali ushawishi mkubwa wa Humba kwa uongozi wa wizara ya Afya hususani Katibu mkuu wa wizara ambae nae ni mmojawapo wa watu wanaofaidika na "Hisani " Za Humba. Pia cha ziada ikiwa ni utaratibu wa kawaida kwa mtu kupewa Baraka na wizara ili atibiwe nje na kwa gharama za Mfuko, kwanini utaratibu huu usiwe wazi kwa wanachama wote? Kwanini usiwekwe? Yeye na wapambe wake wanamsaka kwa udi na uvumba mtu alie leta taarifa hapa. Uzuri ni kwamba wapo baadhi ya washauri wake waliomhakikishia kuwa JF haisomwi na watu wengi kwa hiyo hatapata madhara makubwa!


Upo ufisadi mwingine katika ujenzi wa jengo la NHIF liliopo Kursani ambao kwa sasa ndio makoa makuu ya NHIF. Gharama za awali za jengo zilisemwa kuwa ni Bilioni Mbili, cha kusikitisha ni kwamba gharama za ujenzi zimezidi mno kiasi cha awali kilichokubaliwa. Nasaka Nyaraka za kiasi halisi cha fedha kilichotumika kama ziada ya Bilioni mbili halafu nitawaletea hapa!!! Sasa kuna hali ya kutoamniniana baada ya habari hii kutoka, ila tutajitahidi kupata taarifa kamili.


Yupo aliuliza kuhusu mfumo wa Premia. Mfumo wa PREMIA sio Premium bali ni ‘software' iliyotazamiwa kuharakisha malipo ya wateja(mahospitali). Mpaka sasa mfumo haujaanza kazi baada ya matumizi yanaozidi Bilioni moja katika mfumo huo.


Kwa yule anaeulizia mawasiliano kamili ya Mkurugenzi wa NHIF bwana Humba ni haya Hapa:
Simu ya Mkononi: 0784650090
0784852339
Simu ya Mezani: 2133972
Email: ehumba@nhif.or.tz
ebdhumba@yahoo .com

Zipo taarifa nyeti tukifanikiwa kuzipata zitakuwa zimeanika kwa ufasaha ufisadi wa NHIF. Tunajitahidi, tukipata tutauleta hapa.

Asanteni
 
Kikwete Ana Kazi Sana Na Nchi Hii....tumuulize Swali Moja Tu"ataifanyia Nini Nchi Hii"
 
Inaelekea ufisadi umejikita vilivyo kila mahali. Inabidi tuutafute mzizi wa ufisadi tuung'oe la sivyo itakuwa kama tuna-prune matawi tu wakati mti unaendelea kushamiri...
 

Thanks kwa kuja hapa kutufanyia clarification sasa nimeelewa zaidi kabisa kuhusu hiyo software ya Premia. Swala la kwanza jee swala zima la kuadopt PREMIA lilikubadilika miongoni mwa wanachama? Jee hii software itakuwa implimented kwenye kila kituo cha afya ambacho wanachama watatibiwa?

Ni wazi kabisa hili swala la kuadopt software kwa ajili ya kufanya malipo ni danganya toto, kwani kwa asilimia kubwa sana hapo Tanzania tekinologia hiyo itakubwa na ukinzani mkubwa. Jee ni kwanini swala la PREMIA halikuwekwa kama long term project? Maana sioni umuhimu wa kuadopt software itakayo tumika only Dar au kwenye miji mikubwa pekee kwani ndiko kwenye computer.

Jee mlikubaliana kuhusu ujenzi wa jengo la NHIF? Na kama halikuwepo kwenye makubaliano jee ni nani alianzisha, na kwa faida gani?
 
Kikwete Ana Kazi Sana Na Nchi Hii....tumuulize Swali Moja Tu"ataifanyia Nini Nchi Hii"

Nadhani katika harakati zake za kuwania Uraisi wa Tanzania mwaka 2005 Kikwete hakuwahi kufikiria kwamba anatakiwa kuitumikia nchi yake Tanzania.

Pamoja na kashfa zote ambazo zimemzunguka hajawahi hata mara moja kupambana na hawa mafisadi bila ya kuwaogopa!!! amekuwa ni mwoga na anadiriki kuendelea kumbatiana na hawa waovu MAFISADI waliomzunguka! Kila nikifikiria sisi walalahoi na huu mfuko wa Bima ya Afya, nafikia kwamba kuna siku mafisadi watatoka kwa mtutu!!!

Ikiwa tu rais ataendelea kutabasamu kinafiki hadharani... Kudhihirisha kwamba mafisadi watakingiana vifua always!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…