Ufisadi mwingine wanahabari kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi mwingine wanahabari kilimanjaro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by STINGER, May 3, 2012.

 1. S

  STINGER Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  viongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa kilimanajro mecki wameingia kwenye kashfa nyingine nzito safari hii ikiwa ni ya ufisadi kwa kutumia fedha kwa udanganyifu.

  Ufisadi huu wameufanya siku kadhaa zilizopita wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyo fanyika moshi na kuandaliwa na utpc.

  Viongozi hawa wametumia stakabadhi za uongo kuhalalisha ufisadi wao tena kwa kushirikiana na kncu, walewale ambao walikuwa wakishirikiana nao katika ufisadi wa kuuza sukari kwa wakenya nje ya nchi.

  Wameshirikiana kwa kupewa stakabadhi zenye kuonyesha malipo ya juu tofauti na yale waliyoyafanya.

  Kwa mfano malipo yaliyo kwenye risiti kwa ajili ya kukodisha ukumbi ni tofauti na yale ambayo wamelipa kncu yenyewe na hata malipo ya chakula na vinywaji ka ajili ya wanasemina imegushiwa kwa viongozi hao kudai risiti zenye kuonyesha laipo ya juu kuliko matumizi waliyofanya.

  Chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi huo kinaeleza kuwa viongozi hao wasio waadilifu wamekuwa akiingiza kati ya 70,000 hadi 80,000 kwa siku katika semina hiyo ya siku nne.

  Viongozi hao ni wamekuwa wakifanya hivyo bila ridhaa ya wenzao wengine hivyo kusababisha siri hiyo kuwa wazi. Viongozi hao ni pamoja na wale waliotuhumiwa kwenye biashara haramu ya sukari nao ni makamu mwenyekiti makundi, katibu msaidizi nakajumo, mweka hazina msaidizi rodrick na mweka hazina jane.

  Pia viongozi hawa wanatuhumiwa kukata malipo ya siku moja kwa wanahabari 3 ambao walikuwa kwenye semina hiyo ambayo ni 25,000 kila mmoja kwa kutoka wakati semina inaendelea kwa madai ya kuwa ni agizo la utpc. Wamesema huku wakikataa kutoa ushahidi wa maandishi kuwa asilimia 20 ya makato hayo ynarudi utpc na 80 kwa mfuko wa mecki. Sasa tujiulize kama utpc wanahaja na hizo 5,000 kama makato ya watoro wa semina, wakati wahusika waliaga viongozi kutokana na dharura za kikazi. Kuna ambao wana mahusiano yasiyo rasmi na naadhi ya viongozi ammbao nao waliondoka lakini hawakukatwa malipo yao.

  Wanahabari nyie mnaaminiwa kwa kufichua maovu, basi iundwe tune kuchunguza haya yote yaliyotokea na pia kama utpc inaweza kuungana na vilabu kufanya makato kama haya maana katika semina hiyo alikuwepo mwakilishi wa utpc yenyewe.
   
 2. I

  IVETA Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! is it true? tume ni muhimu maana wanahabari wanatakiwa kuwa waadilifu. tunawaamini.
   
Loading...