Ufisadi mwingine nyumbani kwa mzee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi mwingine nyumbani kwa mzee

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Aug 19, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ikulu lawamani
  • Yafuja mamilioni kwa chakula cha jioni

  na Edward Kinabo


  [​IMG]
  WAKATI baadhi ya wadadisi wa mambo wakihoji faida gani taifa lilipata kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa uchumi wa dunia (WEF), imebainika kuwa Ofisi ya Rais - Ikulu ilifuja fedha za umma takriban sh milioni 367 kwa hafla ya chakula cha jioni kwa wajumbe wa mkutano huo.
  Mkutano wa uchumi wa dunia ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano ‘Mlimani City’ jijini Dar es Salaam, kuanzia Mei 5 hadi 7, mwaka huu.
  Taarifa za uchunguzi kutoka kwenye mfumo wa ufuatiliaji rushwa ulio chini ya shirika lisilo la kiserikali la ‘Agenda Participation’, zimethibitisha Ikulu kutumia vibaya fedha za umma katika hafla hiyo ya chakula cha jioni.
  Aidha, ukubwa wa bajeti ya chakula hicho cha jioni na mkataba mzima wa tukio hilo baina ya Ikulu na kampuni ya waandaaji, vyote kwa pamoja vimeashiria kuwapo kwa mazingira ya rushwa katika maandalizi ya tukio hilo, hasa kutokana na kujumuishwa kwa mahitaji mengi yasiyokuwa na ulazima, licha ya kuwa yaligharamiwa kwa gharama kubwa.
  Tanzania Daima linayo nakala ya mkataba wa maandalizi wa tukio hilo ulioingiwa na Ofisi ya Rais - Ikulu na Kampuni ya ‘Round Trip Event and Production Tanzania’, inayoonyesha vipengele kadhaa vya makubaliano vilivyotiliwa shaka kubwa na watafiti hao wa rushwa.
  Mkataba huo ulitiwa saini Machi 31, mwaka huu na Katibu Mkuu wa Ikulu akishuhudiwa na Ofisa mwingine wa ofisi hiyo anayefahamika kwa jina la Mussa M. Makuya, huku mtia saini wa kampuni hiyo akiwa Prashant Powar.
  Moja ya mambo yanayodaiwa kutoa mwanya kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika tukio hilo ni mkataba huo kuwa na mlolongo mrefu wa bidhaa mbalimbali bila kuonyesha bei mahususi za kila bidhaa na badala yake jumla kuu kuwekwa bila hata kuchanganuliwa jinsi ilivyofikiwa.
  Kwa mujibu wa mkataba huo, mialiko kwa waliohudhuria hafla hiyo iliigharimu serikali sh 8,250,000, mapambo na ukumbi sh 85,800,000, muziki na vipaza sauti sh 19,800,000. Matumizi mengine ni taa maalumu iliyogharimu sh 39,600,000, mfumo maalumu wa video sh 13,200,000, graffiti maalumu sh 6,600,000, burudani ya kawaida sh 13,200,000, burudani za jukwaani sh 15,180,000 na sh 3,300,000 zilizotumika kwa mawasiliano.

  Pia sh 26,400,000 zilitumika kulipa watendaji kazi wote waliohusika na menejimenti ya tukio hilo, sh 33,000,000 gharama ya usimamizi wa tukio na sh 27,060,000 zilitumika kwa vitu vya ziada na dharura.
  Hata hivyo, upembuzi wa kawaida wa orodha ya mahitaji hayo ulionyesha wazi kuwa baadhi ya bidhaa na huduma zilizotolewa hazikuwa na ulazima wowote.
  Kilichowashangaza zaidi wafuatiliaji wa masuala ya rushwa ni jenereta la kufua umeme kukodiwa kwa sh 19,800,000 wakati uongozi wa ukumbi wa Mlimani City ulikwisha kutoa umeme na jenereta la dharura.
  “Kwa mfano, jukwaa la kuchezea lililonyanyuliwa na tingatinga, maonyesho kwenye makabati ya maonyesho na mfumo wa mawasiliano, viliwekwa kwenye bajeti wakati hakukuwa na ulazima huo, kwani ukumbi ulikuwa umewekwa vizuri na hakukuhitajika nyongeza hizo, hususan kwa lengo la kurahisisha uchezaji wa muziki,” ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo.
  Kibaya zaidi, baadhi ya bidhaa na huduma zilizokuwa zimeorodheshwa ziliwekewa mabano kuashiria kwamba zingetumika tu kama zingehitajika, hali iliyotia shaka kujua zilizolipiwa na zile ambazo hazikulipiwa, wakati mkataba ulisainiwa ukionyesha idadi kuu ya pesa ya bidhaa zote zilizoorodheshwa.
  “Swali la kujibiwa ni je, kwa huduma zile ambazo hazikutumika au kuhitajika, nini kilifanyika ?” ilihoji sehemu ya utafiti huo.
  Gazeti hili lilipowasiliana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kupata majibu yake juu ya mkataba huo na matumizi hayo makubwa ya fedha za walipa kodi, alikataa kulizungumzia suala hilo kwa sababu ya kile alichokieleza kuwa yupo likizo.
  “Sasa bwana hilo suala mimi siwezi kukujibu…nipo likizo, umesikia…nipo likizo,” alisema Luhanjo na kukata simu.
  Serikali imekuwa lawamani mara kwa mara kwa matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma, yakiwamo yale yahusuyo safari na mikutano ambayo baadaye mafanikio yake kwa taifa huwa vigumu kuonekana au kuelezeka. Huko nyuma serikali iliwahi kushutumiwa kwa kutumia mamilioni ya shilingi kugharamia mkutano wa Sullivan mwaka 2008. Mkutano huo uliofanyika Arusha uliwakutanisha zaidi ya wajumbe 500, ambapo wengi wao walitoka Marekani ya Kaskazini.


  Source: Tanzania Daima 19 August 2010
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ...zati is bongo bana.....!
   
 3. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  :humble:Solution ni kuing'oa hii mamlaka isiyo na maadili ya matumizi ya fedha za umma kupitia sanduku la kura
  tanzania bila ccm inawezekana:ban:
   
 4. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  mlitaka waibe kwa style ya epa tena? sasa hivi wanazichota kidogokidogo kila fursa inapopatikana, wakichota kwa mkupuo mmoja si mnashtuka sikuhizi???????
   
Loading...