Ufisadi mwingine kncu...........

Ufisadi mwingine kncu...........

Joined
Jan 2, 2013
Posts
16
Reaction score
3
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa kilimanjaro kncu mernad swai ameandaa kiasi cha sh laki tano kwa kila mjumbe wa mkutano mkuu maalumu ili kumkingia kifua asivuliwe wadhfa huo.
Taarifa za kuaminika kutoka katika ofisi hiyo zinaeleza kuwa kutona ufisadi uliopo katika chama hicho tayari wajumbe wa mkutano mkuu walikuwa wajipanga kumvua mwenyekiti cheo chake lakini ameshtuka mapema na mpango huo.
Moja wa mjumbe wa bodi hiyo ya kncu ambayye pia ni katibu wa mbunge wa moshi vijijini bwana mallya alisema kuwa kncu wanajua walikoitoa hivyo majungu majungu hayawezi kumtoa mtu madarakani na watapambana hadi kieleweke.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa mallya pamoja na kaimu mhasibu wa cham,a hicho ndugu temba ndio waliopewa tender hiyo ya kusambaza fedha hizo ambapo kila mjumbe anapitishiwa nyumbani kwa usiri mkubwa na tayri wameanza katika wilaya za moshi vijijini siha rombo na sasa waanaelekea vunjo.
Mwenyekiti wa bodi ya kncu aliopulizwa juu ya uhalali wa ugawaji wa fedha hizo alikiri kujua mchakato huo inagawa hakutoa ufafanuzi kuwa ni za nini lakini alipobanwa zaidi alikiri ni za kulipa wakulima mafao yao ingawa mgawo huo hutolewa nyakati za usiku.
Kwa kipindi kirefu hivi sasa kumekuwa na vuta nikuvute ndani ya chama kikuu cha ushirika kncu kutokana na ubadhirifu ambao umefanywa na mwenyekiti wa bodi hiyo huku ukianikwa na mbunge wa vunjo agustine mrema lakini wakati huo huo Cyril chami mbunge wa moshi vijijini anamkingia kifua kupitia kwa katibu wake bwana mallya ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo ya kncu.
TAKUKURU ,MRAJISI WA VYAMA VYA USHIRIKA,POLISI NA WASAMARIA WEMA NA WASOMI JITOENI TUNUSURU USHIRIKA KILIMANJARO….
 
Back
Top Bottom