sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 649
Hali ni mbaya sana kila kona madudu tu.OMG! Tumekwisha! nachanganyikiwa na sijui ni curse na lipi! ahh! God bless Tz!
Kwa utawala huu wa VASCO DA GAMA a.k.a De Lima. tutasikia mengi sana. Ndugu yangu mwana JF Sulphadoxine hata sasa tunapoongea CAG akipelekwa pale DAMPO- Tabata na akafanya ukaguzi atabaini UFISADI mkubwa sana na wakutisha. Haya ndiyo madhara ya kuwa na viongozi watokanao na CCM.Wakaguzi wabaini ufujaji pesa za miradi
Mabilioni ya pesa za walipa kodi yayeyuka
Kashfa kwenye ununuzi wa mashangingi 68
Wafadhili watishia kuzuia misaada yao
SOURCE:GAZETI LA KULIKONI LA LEO 19/8/2011 -25/8/2011
<br />Hali ni mbaya sana kila kona madudu tu.
the best doctor is changes...hapa ukimwita mungu atakuona pungwani wa mawazo wakati akili ya kujua mema na mabaya umepewe..sasa wataka mungu aje kufanya nini..kupiga kura???? Tukubali tusikubali..mabadiliko ni lazima kwa maslahi ya taifa zima.eeh, nchi kwishne, nukanuka, ozaoza, inapumulia mashine 99%, inahitaji madaktari bingwa kuokoa maisha la si hivyo tutaangamia nayo, mungu sikia kilio chetu.
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imekumbwa na kashfa kubwa baada ya ukaguzi maalumu uliofanywa kwenye miradi ya maji nchi nzima kubaini tuhuma za ufisadi, uzembe wa maofisa na matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi kwenye wizara hiyo.
Ukaguzi maalumu (special audit) uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenye programu ya maendeleo ya sekta ya maji (2007-2010) umebaini malipo mengi ya utata kwenye miradi ya maji nchini na matumizi mabaya ya pesa za umma.
Katika moja ya tuhuma hizo za ufisadi, Wizara ya Maji na Umwagiliaji imebainika kutumia zaidi ya dola za Marekani milioni 39 (takribani shilingi bilioni 63) kwenye mazingira ya utata bila kuzingatia miradi iliyopo kwenye mpango kazi wa mwaka wa wizara hiyo.
"Shughuli za manunuzi ndani ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji hazifanywi kuendana na mpango wa manunuzi wa kila mwaka," imesema sehemu hiyo ya ripoti mpya ya CAG kutokana na ukaguzi uliofanywa Septemba mwaka jana.