Ni vizuri tukajua kuwa mkwepa kodi yoyote huko kwa wenzetu hufungwa au kufilisiwa bila huruma kwa maana huyu anaikosesha mapato serikali na matokeo ni kudorora kwa huduma za umma.Napata wasiwasi kuwa Nndondo anafaidika mno na mapato ya Mariedo kiasi cha kupoteza povu jingi na kujiapisha na kutusomesha sisi tusiojua smartness za mitaani,na kejeli kuwa yote ni majungu,kama vile kakariri maneno ya watuhumiwa wa EPA waliotajwa na Baba Slaa pale Mwembe Yanga!
Halafu katika kukua kiroho kiukweli lazima uweze kukemea dhambi za waziwazi kama hii vinginevyo basi bado uko Misri-kiroho that is!