Ufisadi KNCU na TCCCO

Ufisadi KNCU na TCCCO

dira

Member
Joined
Jun 8, 2012
Posts
18
Reaction score
1
Hivi karibuni kumekuwa na malumbano kati ya uongozi wa kampuni ya kukobolea kahawa ya moshi Tanganyika Coffee Curing Company(TCCCO) na baadhi ya vingozi wa vyama vya ushirika Kilimanjaro kuhusiana na uuzwaji wa mali za kampuni hiyo ambayo wanachama wake ni vyama vya ushirika Kilimanjaro na arusha.

Ugomvi huu umetokana na uongozi wa tccco kuamua kuuza baadhi ya nyumba za kampuni hiyo ili kulipia madeni makubwa ambayo inakabiliana nayo pamoja na kununua mashine ya kisasa ya kukobolea kahawa jambo ambalo wanachama wengi wa vyma vya ushirika hawaradhii

Kwanza kabisa wanadai si vyema kuuza mali za kampuni ambazo ni muhimu kama nyumba kwa ajili ya kununulia mashine ambazo hata hivyo bei zake ni za chini ikilinganishwa na dhamani ya nyumba hizo kwa miaka mingi ijayo na ambazo zinaweza kutumika kama raslimali muhimu

Wanadai ya kuwa nyumba hizo ambazo zilijengwa kwa miaka mingi iliyopita kwa juhudi za wazee ambao walijitolea kwa hali na ziuzwa leo hii kupata raslimali kama hizo haitakuwa rahisi tena.

La pili wanadai ya kuwa kuna harufu ya ufisadi na rushwa katika uuzwaji wa mali hizo na kwamba mbali na kuwa zinauzwa kwa tenda lakini tayari viongozi wa tccco washajua ni nani wanemlenga na pia washajitayarisha kwa hilo

Inadaiwa ya kuwa mwenyekiti wa bodi ya tccco menard swai tayari alishafanya maamuzi ya kumuuzia mfanyabiashara mmoja tajiri wa kitanzania anaefanya biashara zake nchini Nigeria na kwamba tayari alishapatiwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kufanikisha hilo fedha ambazo alitumiwa kupitia wakili mmoja swahiba wa mfanyabiashara huyo ambae ana ofisi zake katika jingo la kncu ambalo linamilikiwa na chama cha kncu ambacho swai pia ni mwenyekiti wake

Inasemekana alianza juhudi za kumuuzia mfanyabishara huyo jingo hilo ambalo liko katikatikati ya mji miaka kadhaa iliyopita kabla ya wanachama na wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro waishio nje ya mkoa huo kuingilia kati na ndipo akatumia nguvu ya fedha alizotumiwa kwa kuwahonga baadhi ya wanacham wa kncu ambao walipitisha nyumba hizo ziuzwe

Pia pamoja na kwamba mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alishazuia uuzwaji wa nyumba hizo inadaiwa swai alikwenda mbali zaidi na kutuma ujumbe kwa waziri wa kilimo charistopher chiza huku yeye mwenyewe akijitoa kwenye safari hiyo ili kuondoa mashaka ya kuwa alikuwa na mbinu za kuuza nyumba hizo kwa maslahi binafsi

Cha ajabu pamoja na kauli ya rais kikwete ya kuwa mali za ushirika hazitauzwa tena, waziri chiza inasemekana alitoa idhini kw aujummbe huo ya kuwa nyumba hizo ziuzwe na kuwa malalamiko ya wanachama yalikuwa ni ya wivu mtupu. Inasemekana alimwelekeza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro leonidas gama kutengua kizuizi chake ili nyumba hizo ziuzwe na tayari kuna taarifa ya kuwa matangazo yashatolewa na wakati wowote zitauzwa

Kwa kweli hali hii inasikitisha sana haswa ikitilwa maanani ya kuwa kuna njia mbadala zinaweza kutumika ili kunusuru nyumba hizo ambazo ni raslimali muhimu kwa taasisi hiyo

Ndiyo maana wanachama wakamuomba kiongozi wao wan chi aingilie kati maana tayari wameshaona mali nyingi za kampuni hiyo zikiuzwa bila faida yoyote pia amechukua baadhi ya mashine na mitambo akaipeleka kwenye shamba la mzee Edwin mtei ambae inasemekana ni baba mkwe wake lakini hakuna naehoji hilo kwa vile yeye nimwenyekiti na mwenye sauti ya mwisho

Swai pamoja na kwamba ni mwenyekiti amedaiwa kuuza mashine mbalimbali ikiwemo moja ambayo ilinunuliwa lakini kabla haijafanya kazi ikauzwa kwa mchimbaji madini mmoja wa huko mbuguni. Pia mtambo wa kutengeza mkaa unaotokana na makapi ya kahawa umeuzwa magari karibu yote ya kampuni yameuzwa lakini yeye anasema na kuna taarifa kuwa juzi aliitisha kikao na waandishi wa habri na kuwaeleza ya kuwa uuzwaji wa nyumba hizo hautsitishwa tena kwa maana una mkono wa rais kwa maana ya ruhusa ya waziri na mkuu wa mkoa

Pia anajivuna kwa kusema ya kuwa hata serikali kupitia ccm inajua ya kuwa fedha hizo atazitumiaa kwa ajili ya kugombea ubunge jimbo la hai kupitia ccm ndiyo maana wamemruhusu maana mara ya kwanza viongozi walikuwa na wasiwasi angegombea kwa chadema kwa kutumia fehda zilizotoka kwa wakulima

Kilio chetu ni kwa
 
chiza ni janga sana katika mambo ya ushirika, haupendi ndio maana katoa kibali.....
 
Tunafukua makaburi ....
Swai yupo wapi sasa enzi hizi za "ukila fedha za umma nasema lazima utazitapika tu"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom