Ufisadi huduma ya chanjo ya 'yellow fever' hapa nchini

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Shikamoni wandugu.

Kumekuwa na figisufigisu nyingi sana katika huduma ya chanjo ya homa ya manjano /chanzo ya kimataifa (Yellow Fever Vaccination),hasa gharama ya huduma hii.

Gharama hiyo hapa nchini hutofautiana sehemu na sehemu, kituo na kituo wakati ni huduma hiyohiyo inayoratibiwa na Wizara ya Afya Jinsia na Watoto hapa nchini Tanzania.

Mathalani, ukienda:-

1. Hospital ya Mnazi mmoja ya jijini Dsm, wanatoa hiyo huduma kwa TZS 55,000 (Elfu Hamsini na tano);

2. Holili Mkoani Kilimanjaro TZS 20,000 (Elfu Ishirini);

3. Azam Marines pale Posta - Dsm wanatoza TZS 20,000

4. JN & K International Airports wanatoza 40 USD

Sasa basi, gharama ya huduma hii kwann inadiffer wakati huduma zote zinaratibiwa na Wizara (moja) hiyohiyo?

Ni mradi wa mtu binafsi au nn hapo?

Kama jipu lipo, lipasuliwe.
 
sitaki kukumbuka siku niliyoangaika kuipata, mnazi mmoja wameanza kutoa tena coz walisitisha utoaji, ikawa ni Azam Marines Posta tu ndio wanatoa, tena siku 2 tu kwenye wiki, ukienda alfajiri unachoma jioni
 
Mnazi mmoja nilipata hiyo service kwa elf kumi tuu hiyo 55,000 unatupiga fix mkuu
 
Shikamoni wandugu.

Kumekuwa na figisufigisu nyingi sana katika huduma ya chanjo ya homa ya manjano /chanzo ya kimataifa (Yellow Fever Vaccination),hasa gharama ya huduma hii.

Gharama hiyo hapa nchini hutofautiana sehemu na sehemu, kituo na kituo wakati ni huduma hiyohiyo inayoratibiwa na Wizara ya Afya Jinsia na Watoto hapa nchini Tanzania.

Mathalani, ukienda:-

1. Hospital ya Mnazi mmoja ya jijini Dsm, wanatoa hiyo huduma kwa TZS 55,000 (Elfu Hamsini na tano);

2. Holili Mkoani Kilimanjaro TZS 20,000 (Elfu Ishirini);

3. Azam Marines pale Posta - Dsm wanatoza TZS 20,000

4. JN & K International Airports wanatoza 40 USD

Sasa basi, gharama ya huduma hii kwann inadiffer wakati huduma zote zinaratibiwa na Wizara (moja) hiyohiyo?

Ni mradi wa mtu binafsi au nn hapo?

Kama jipu lipo, lipasuliwe.

What?? 55,000/= au nimekosea.. hii si 5,000/= tu? kuna nini cha ziada kama tayari ulishalipia na unayo kadi? Hii ni nini tena??
 
sitaki kukumbuka siku niliyoangaika kuipata, mnazi mmoja wameanza kutoa tena coz walisitisha utoaji, ikawa ni Azam Marines Posta tu ndio wanatoa, tena siku 2 tu kwenye wiki, ukienda alfajiri unachoma jioni
Mwanza pale naponilifanyiwa figisuhizo kwani nilipay 50 kabla ata cjatoka nikaona mwenzangu anapatiwa hiyo kitu kwa 20 tu nikajua tayari
Wabongo wako kazini
 
WP_20170228_15_53_31_Pro.jpg
 
WP_20170228_15_53_20_Pro.jpg
Nimekuwekea na picha mkulu ujionee hiz vitu ni bora ziwekewe utaratibu wa kuambiwa bei kabisa kua hapa ni kiasi flani ndio upate chanjo kuna watu wanapigwa mpaka laki ,je vipi kuhusu yale maswali ambayo yapo kwenye ile fomu ya kujaza kabala hawajaku vaccinate
 
Mwaka Jana nilichoma pale Horohoro border Tsh 20000 lakini pia nasikia wamebadili zile kadi.
 
Mimi nlichanja pale bandarini kwa elf 20 lakini napo kuna jinsi wanakuchanja kwa elf 15 haupewi risiti wanajua wenyewe wanavyofanya. Nahisi huwa wanapunguza cc sijui ama wanavyojua wao
 
Back
Top Bottom