Ufisadi hospitali ya Rufaa Bombo, mamilioni yatumika kulipa interns hewa!

Ufisadi hospitali ya Rufaa Bombo, mamilioni yatumika kulipa interns hewa!

tangaraha

Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
51
Reaction score
9
Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga na Bombo Dr. Karia, kaimu wake Dr. Naima, muhasibu wa hospitali na kiongozi wa interns wa hapa Dr. Mwema wameshirikiana kuiibia serikali kiasi cha tsh milioni 8.8 kupitia malipo hewa kwa interns waliomaliza muda wao.

Wamefanikiwa kwa kuchomeka majina 10 ya interns waliomaliza muda wao katika maombi ya posho ya kujikimu ya mwezi october 2012.
nimejionea karatasi ya majina ya malipo kwa muhasibu ikiwa na majina ya waliomaliza ambao wamesainiwa (ghushiwa) eti wamechukua malipo yao wakati hawana habari na hayo malipo kwani walishamaliza na kupewa vyeti vyao.

Madaktari hao waliomaliza na kuondoka waliofojiwa saini zao na jamaa kuweka kibindoni tsh milioni 8.8 ni:

Dr. Abasi, Dr. Rajab Husein, Dr. Hessein Sepoko, Dr. Awe, Dr. Gladys Yona, Dr. Serina, Dr. Patrick, Dr. Zaharia, Dr. Agnes na Dr. Daniel.
nikiwa mmoja wa interns waliopo hapa nimeshuhudia saini ya Dr. Awe na Dr. Abasi ikiwa imefojiwa.
 
Hivi kiongozi wa intern hapo ni nani? Hawa jamaa wa vyuo vingine dhaifu sana! Huwa nawaaminia jamaa wa muhas, wamezoea michimbuko.
 
Hivi kiongozi wa intern hapo ni nani? Hawa jamaa wa vyuo vingine dhaifu sana! Huwa nawaaminia jamaa wa muhas, wamezoea michimbuko.
ni dr. mwema, kamaliza muhas. kwakua yeye ndo anaandaa list inasainiwa then anaipeleka wizarani mwenyewe. lazima ajue kama kuna majina hewa au laa
 
Huu mchezo ni wa kawaida sana hasa kwa hospitali za rufaa hususani KCMC, Bugando, Mbeya Rufaa na Muhimbili.

Ni issue zinazopigwa kwa ufundi mkubwa, wachezaji wakiwa wahasibu wa hospitali, wakurugenzi na watendaji fulani pale wizarani. Mtasiwa, Nkya, Mponda na Nyoni hizi issue wamepiga sana. Wizi wa pesa kwa kutumia kivuli cha ''Interns'' ni kitu cha kawaida sana katika utendaji wa wizara wa sasa.

Nina wahurumia sana hawa ''Intern'' namna wanavyotumia kama Condoms. Sometimes ni bora kuwa Bar maid kuliko kuwa Intern Doctor hapa Bongo.

Kifupi malipo yoyote yanayofanywa na wizara ya afya ujue 30% ni malipo hewa kabisa!!!

Mkuu hii kitu itaisha siku ukiona CCM inaondoka madarakani, vinginevyo haiwezekani.
 
mmmmmmmm haya ngoja tusubiri na sisi wa mwakani tuone aisee itakuaje
 
Kiasi hicho cha pesa wanayotuhumiwa na nguvu uliyotumia kuhakikish wanaumbuka sijui kama sio chuki binafsi.
 
kuna muhasibu mmoja pale wizarani anaitwa dagaa,huyu muhasibu ni bandidu sana,mara nyingi huchelewesha malipo ya interns na kupelekea migogoro.nadhani jamaa anazungushaga fedha hizo ili kujipatia faida.
 
Huu mchezo ni wa kawaida sana hasa kwa hospitali za rufaa hususani KCMC, Bugando, Mbeya Rufaa na Muhimbili.

Ni issue zinazopigwa kwa ufundi mkubwa, wachezaji wakiwa wahasibu wa hospitali, wakurugenzi na watendaji fulani pale wizarani. Mtasiwa, Nkya, Mponda na Nyoni hizi issue wamepiga sana. Wizi wa pesa kwa kutumia kivuli cha ''Interns'' ni kitu cha kawaida sana katika utendaji wa wizara wa sasa.

Nina wahurumia sana hawa ''Intern'' namna wanavyotumia kama Condoms. Sometimes ni bora kuwa Bar maid kuliko kuwa Intern Doctor hapa Bongo.

Kifupi malipo yoyote yanayofanywa na wizara ya afya ujue 30% ni malipo hewa kabisa!!!

Mkuu hii kitu itaisha siku ukiona CCM inaondoka madarakani, vinginevyo haiwezekani.

duh! wizara hii ya afya inawafanyakazi hewa wa kutosha tu, hadi interns hewa. yaani cku ya mwisho itakuja kuwa na wagonjwa hewa wanaotibiwa kwa mamilioni.
 
Kiasi hicho cha pesa wanayotuhumiwa na nguvu uliyotumia kuhakikish wanaumbuka sijui kama sio chuki binafsi.

ndugu afwe ndugu afwe inamaana mtu akiiba kidogo asichunguzwe? na unanishangaza unaposema ninachuki binafsi na uongozi wa hospitali, hakuna hicho kitu. fikiria hospitali zote zenye interns kila sehemu waongezee milioni 10 hewa, kwa mwezi jumla ni ngapi? kwa mwaka je? utaona ni pesa nyingi zinaibiwa. tunareport hivi ili wanaowasimamia wajue na wachukue hatua stahiki kupunguza upoteaji wa fedha za uma.
wewe waona ni taarifa ndogo, ila ni kubwa sana na wahusika wakijua tu wameanikwa jamii forum najua kesho watakuwa wanahaha janja yao imegundulika.
 
Naheshimu maoni yako, ila hukutilia maanani kulinganisha nguvu iliyotumika na hata hisia za hasira zilizopo kwenye taarifa yako. Otherwise hata leo tunatofautiana n wanao amini kuwa mtu akihisiwa ameiba milioni tano, ni sahihi kuunda tume itumie milioni 100 kuchunguza tuhuma hizo. Na ethics za kutoa taarifa, inapokuwa ni tuhuma vyeo vyao vingetosha badala ya kutaja majina halisi ya watu. Siwajui na siko huko Tanga kwa hiyo usiwe na shaka na conflict of interest juu yangu
 
mwizi ni mwizi tu hata kama kaiba tshs 500, ila mkuu hako kamchezo kapo sana, na ndio maana hakuna mfumo thabiti wa kulipa interns, hapa wizarani huwa ni blah blah tu ili kuhakikisha malipo yanachelewa na list ya interns mara nyingi huwa feki
 
Back
Top Bottom