Ufidi mradi wa food aid counterpart

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,274
9,910
Kwa muda mrefu nimekuwa nafuatilia haka kamradi cha Food Aid Counterpart waliopo pale lumumba street kunaonekana kunaufisadi wa kutisha.

Mradi huu upo katikati ya wizara ya fedha, kilimo na Japan ambao hutoa funds.

Mradi huu hotoa fedha kwenye miradi mbalimbali ya kilimo baada ya kupata michanganuo ya miradi hiyo, na hapo ndipo mchezo unapochezwa kwani baadhi ya maofisa wa wizara ya Fedha kilimo na chakula na Mabosi wa mradi kupitia watu mbalimbali huandaa mradi mthalani mradi wa kuchimbwa bwawa singida ilitolewa milioni 900 kupitia kwa jamaa mmoja alikuwa askar magereza ambeye ndiyo aliandaa mradi huo lakini kihalisi mradi huo ulitumia milion 300 kiasi kilicho baki waligawana. Hata maofisa wanapokwenda kukagua mradi husika tazari unakuta keshapata gawio lake na hata wakati mwingine ofisa haendi anamwambia dereva apaki gari na lisionekane kwa siku 2 au 3.
Ukiangalia mabosi wa mradi huo walivyojilimbikizia mali utashangaa mfano Dr. Wilbard Lorri Slaa aliyegombea ubunge karatu jamaa alikwapu hela sana ktpitia miradi hewa na taarifa nilizonazo nasikia anataka kurudi kwenye mradi kuchukuwa nafasi yake inayokaimiwa na mtu mwingine.
Wakati mwingine ilikufunika mambo yasitoke nje hawa jamaa hutoa bakishishi kwa wafanyakazi wa chini
 
Back
Top Bottom