Ufaulu wa kidato cha nne2017

Ufaulu wa kidato cha nne2017

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,735
Reaction score
4,932
TAKWIMU ZA ELIMU ZINAHITAJI ZAIDI YA TUNACHOKIONA AU KUSIKIA.
Ni ukweli usiopingika kuwa elimu yetu inahitaji zaidi ya maneno ya ushawishi tunayoyasikia mara kwa mara.
Tusishangae kusikia kuwa ufaulu wa kidato Cha nne kwa mwaka 2017 umeongezeka lakini kama wadau wa Elimu tuangalie nyuma ya takwimu uhalisia unasema nini?
Mathalani mwaka 2013 ufaulu ulikuwa 58.25%,mwaka 2014 ulipanda ukawa 68.33%,mwaka2015ulishuka ukawa 67.53,mwaka2016ulipanda ukawa 70.09,mwaka 20017inasemekana ufaulu ni 77%.
Maswali ya kujiuliza ni:
1.Je asilimia hizo zinabeba picha halisi ya mkuo (growth)wa Elimu Nchini?
2.Je asilimia hizo zinaonesha ufanisi wa ndani(internal efficiency)wa Elimu?
3.Je asilimia hizo zinaonesha wanafunzi wote wenye sifa stahiki na vigezo kubalifu vya ufaulu wenye tija?
Bado ipo tuna kila sababu kuangalia takwimu tunazopewa zimebeba nini ndani yake na siyo kuangalia kile kinachooneshwa kwa haraka na takwimu hizo.
Siyo jambo la kushangaza takwimu kutuonesha tofauti na "MUONO HALISI"au takwimu kushawishi na kutupatia hali ya kuridhika hata kama hatupaswi kuridhika.
Takwimu ni muhimu lakini kinachofichwa na takwimu ni muhimu zaidi ya kile kinachoonekana.
 
kuna kitu ndani ya uhalisia kwa maelezo yako mtoa mada hebu fafanua kidogo tuweze kuelewa
 
Kuna vijana wengi mno wanabebwa na takwimu kuwa wamefaulu lakini kiuhalisia ni hatari
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Niliuwa field nafundisha mwaka uliopita kusema ukweli wanafunzi niliowakuta huko mashuleni napata taabu sn kuamini takwimu za ufauru kuonyesha kupanda kiasi hicho.Nmekuta wanafunz wanauwezo mdogo mno sjui necta wanafauru vp? Naona tunajitekenya na kucheka wenyewe.
 
IMG-20180130-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom