Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,187
- 10,664
Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imetangaza kuwa wanajeshi watano waliopatikana na hatia watachukuliwa hatua za kisheria. Askari hao watano walihusika na jinai kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwadahlilisha kingono watoto wadogo Jamhuri ya Afrika ya Kati. Askari wa Ufaransa waliingia katika nchi hiyo ya Kiafrika mwaka 2013 kwa kisingizio cha kurejesha amani kufuatia vita vya ndani katila nchi hiyo iliyokuwa koloni lake. Askari wa Ufaransa huko CAR, maarufu kama Sangaris, pia wanatuhumiwa kuunga mkono genge la kigaidi la Anti Balaka ambalo lilikuwa likitekeleza mauaji ya umati dhidi ya Waislamu nchini humo.
Hivi karibuni pia Umoja wa Mataifa ulisema askari wa kusimamia amani wa umoja huo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) wanawahadaa kwa pesa wasichana wadogo wakiwemo wa miaka 13 ili kufanya nao ngono.
Askari hao wanadaiwa kutoka nchi za Gabon, Ufaransa, Morocco na Burundi. Ripoti ya MINUSCA katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imeeleza kuwa, imezitaka nchi tatu ambazo askari wake wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na vitendo vichafu vya kuwabaka wasichana katika mji mkuu Bangui kufanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo.
cc Ufaransa yakiri kuwa askari wake walitekeleza jinai dhidi ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati - Pars Today