Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,163
Bwana mmoja aliyekulia maisha ya kawaida tu, alipata habari mjomba wake aliyekua anaishi Switzerland alifariki, yule bwana akiwa kijana wa miaka 25 aliambiwa anahitajika ubalozini apewe viza kwani yeye ndiye mrithi wa mali za mjomba wake.
Baada ya mazishi kijana alipewa pesa, nyumba na magari. Aliamua kuuza vilivyouzika na kuja kuwekeza nyumbani.
Alioa binti jirani yake, binti huyo mrembo alishawahi kuwa miss wa taifa. Pamoja na kuishi maisha mazuri lakini kijana hakuwa mfujaji wa pesa.
Walifanikiwa kupata watoto wanne wa kike. Kumbe ile hali ilimsononesha sana yule bwana. Mke alipoinua ujauzito wa tano alimpeleka hospitali ya serikali kujifungua wakati kawaida aijifungulia Agha Khan.
Kumbe yule bwana alipanga na mkunga akitokea mtoto wa kike ambadilishie na wa kiume pale wodini. Kwa nguvu ya pesa yale yalitendeka.
Hivi ni wanaume wangapi wako tayari kulea mtoto ambae si damu yale mradi tu ni wakiume?