Ufanye nini tairi likipasuka (basti)

WISE 2012

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
634
460
Kuna hatua sita za kufuata ndani ya dakika mbili tangu kupasuka tairi ambazo unapaswa kuzifuata.

1. USIHAMAKI wala Kukanyaga Breki, tulia kwanza kwa sababu mara baada ya kupasuka tairi gari lako litaanza kwenda kombo na hivyo utahitajika kulimudu.

2. KAMATA USUKANI Kwa nguvu kwa mikono yote miwili, USIPINDEPINDE KONA huku ukiwa makini na barabara na vioo vya gari lako. Wakati huo soma mwenendo wa gari lako, ambapo mara nyingi litakuwa linakuvuta upande uliopasuka tairi.

3. ONGEZA MWENDO wa wastani ili kudhibiti mwenendo wa gari. Hivyo kama ulikuwa umekanyaga eksileleta usiondoe mguu haraka kwenye hiyo pedo.

4.ONDOA mguu wako taratibu kwenye eksileleta. USIJARIBU KABISA KUKANYAGA BREKI,Ukijaribu kufanya hivyo utabinuka na gari. Ilhali kama usipokanyaga breki gari litapunguza mwendo lenyewe taratibu, wakati wewe ukiwa makini kuangalia watumiaji wengine wa barabara.

5. ONDOA gia zote na uziweke kwenye nyutro huku bado ukiwa umeshikilia vema usukani wako na macho mbele kwenye barabara.

6. Baada ya muda mfupi, kulingana na mwendo wako, gari ikiwa imefika spidi chini ya 60kph, sasa kanyaga breki zako taratibu huku ukisogea kandoni mwa barabara ili usimame.

7. Hatimaye, itakuwa salama zaidi kusimamisha gari lako na kuzima injini.

Hapo utakuwa umeokoa maisha yako na ya abiria wako kutoka kifo.

NYONGEZA: Inapotokea tairi imepasuka ni mara 10 salama kuongeza mwendo kuliko kuhamisha mguu na kukanyaga breki.

Tafadhali, washirikishe na wenzio kwa kusambaza ujumbe huu. Jambo hili linaweza kumpata mtu yeyote, wakati wowote barabarani.
 
Balance ya gari inatoka wapi ukiongeza speed? huu ni utafiti kweli au ujanja wa polini? umechukulia mwendeshaji anatembea speed gani kabla ya bust? kama yupo 120 km/hr aongeze? mimi ushauri wangu mtu aendeshe speed ambayo.anaweza kulimudu gari likipata bust.60/80 km/hr
 
5. Kwa Manual lazima ukanyaje clutch kuingiza gia... kwa Auto lazima ukanyage break kubadilisha gear... hapa unazungumzia ipi?

Njia ni moja tu... ikiwa ni break zimefeli au tairi kupasuka kufanya hayo yote muda haukungoji.... pelekea pembezoni mwa bara bara likakwame huko au lipandishe kweny msingi...
 
nakumbuka ck moja nilikua safarin kwa bahati mbaya taili ya mbele ikapata pancha basi dereva hakua na papara basi aliongoza tu na huku akipunguza mwendo taratiiibu ilimchukua zaid ka km 3 ndo akasimama kwa usalama.
 
Hiyo namba tano,hiyo sentensi ya "... macho mbele kwenye barabara", ndio najaribu kuimagine jamaa lilivyotoa mimacho,huku jasho likimtiririka,hapo mdomo kafunga meno yote kayauma.
 
Kwa ile hamaki na mshtuko wa kupasukiwa tairi nadhani 10% ya wanaokutana na hali hii watafanya unayoyasema.

Mwingine atajikuta ameshakanyaga breki.
 
Kama tairi imepasukia shinyanga kwaiyo uongeze speed tu hadi ufike mwanza?
Halafu? What next?
 
Nimeshindwa kupata point,unasema liache gari mpaka lifike 60km/h je kama gari ikipasuka tairi iko kwa hizo 60km/h inapaswa kuliacha mpaka lifike speed ya ngapi?
 
Tafuta jeki na wheel spanner,kama ipo chini ya siti au kwenye buti then anzaa kazi ya kubadili..Kumbuka kuweka hand break na jeki iwe juu ya flat surface kabla hujaipadisha body ya gari juu. waweza weka jeki juu ya kipande cha mbao
 
Ukiwa dereva siku zote jichunge usipaniki.mfano mdogo maderva wengi ambao sio wazoefu wanapenda kukamata msukani kwa nguvu hasa akiwa rough road ni kosa.

Mda wote kamata usukani kwa kias cha kawaida unapojikaza kuukumbatia kwa nguvu unafanya ball joints na steering system ziwe weak na kuisha ufanisi wake kabla ya muda.

Kuna vitu vingi vya kuzingatia unapokuwa na gari hasa hizi auto ili gearbox yako idumu usipende kubadili mfano kutoka reverse kwenda drive ilhali gari inatembea unaua gearbox.na mengine mengi taeleza siku ingine saa za kulala hizi
 
Nakubaliana na wewe mkuu..maana kuna siku twasafiri na bus usiku kutoka shinyanga kwenda Mwanza..Bus la City Boy lilikiwa limetokea Dar

Jamaa walikuwa wanakimbia mno maana walichelewa kufika..njiani tairi ya mbele ikabust na dereva hakupunguza mwendo..zaidi alibaki na speed ile ile na kuliacha bus lipunguze mwendo lenyewe..mtikisiko ulikiwepo wa kutosha ila hatimae tuisimama.

Kwa pyhsics nliosoma form two..kuna kitu wanaita Inertia..ile kushika breki kwa haraka usimame ghafla..lazima itakupelekea kupinduka maana ni kitu kipo kwa motion kubwa..huwezi kukipiga stop ya ghafla namna hiyo ni more like matairi yanasimama ghafla while bus in general laendelea kutembea maana halikutegema kusimama ghafla.

Ndio maana kupinduka hapo huwezi kukwepa
 
njiani tairi ya mbele ikabust na dereve hakupunguza mwendo..zaidi alibaki na speed ile ile na kuliacha bus lipunguze mwendo lenyewe..
Unamaanisha kuwa 'dereve' haku-play part yeyote kwenye hicho kitendo mpaka basi likapunguza mwendo lenyewe na kusimama lenyewe?Another "NEW LIFE IN KYEREFASO"
 
Mh!!! Mungu anipitishe mbali na kupasuka kwa tairi, maana Sidhani kana nitakumbuka hili somo.

Ahsante kwa elimu
 
Kuna hatua 6 za kufuata ndani ya dakika 2 tangu kupasuka tairi ambazo unapaswa kuzifuata.

1. USIHAMAKI wala Kukanyaga Breki, tulia kwanza kwa sababu mara baada ya kupasuka tairi gari lako litaanza kwenda kombo na hivyo utahitajika kulimudu.

2. KAMATA USUKANI Kwa nguvu kwa mikono yote miwili, USIPINDEPINDE KONA huku ukiwa makini na barabara na vioo vya gari lako. Wakati huo soma mwenendo wa gari lako, ambapo mara nyingi litakuwa linakuvuta upande uliopasuka tairi.

3. ONGEZA MWENDO wa wastani ili kudhibiti mwenendo wa gari. Hivyo kama ulikuwa umekanyaga eksileleta usiondoe mguu haraka kwenye hiyo pedo.

4.ONDOA mguu wako taratibu kwenye eksileleta. USIJARIBU KABISA KUKANYAGA BREKI,Ukijaribu kufanya hivyo utabinuka na gari.

Ilhali kama usipokanyaga breki gari litapunguza mwendo lenyewe taratibu, wakati wewe ukiwa makini kuangalia watumiaji wengine wa barabara.

5. ONDOA gia zote na uziweke kwenye nyutro huku bado ukiwa umeshikilia vema usukani wako na macho mbele kwenye barabara.

6. Baada ya muda mfupi, kulingana na mwendo wako, gari ikiwa imefika spidi chini ya 60kph, sasa kanyaga breki zako taratibu huku ukisogea kandoni mwa barabara ili usimame.

7. Hatimaye, itakuwa salama zaidi kusimamisha gari lako na kuzima injini.
Hapo utakuwa umeokoa maisha yako na ya abiria wako kutoka kifo.

NYONGEZA: Inapotokea tairi imepasuka ni mara 10 salama kuongeza mwendo kuliko kuhamisha mguu na kukanyaga breki.

Tafadhali, washirikishe na wenzio kwa kusambazai ujumbe huu. Jambo hili linaweza kumpata mtu yeyote, wakati wowote barabarani.
 
Maneno mengi all non sense.
Ukiwa na tyre limepasuka usikanyage break wala kuongeza mwendo,toa mguu kwenye mafuta,fungua vioo maana gari iwe nzito.
 
Back
Top Bottom