Ufanyaji wa biashara holela

Ufanyaji wa biashara holela

Majitha

Member
Joined
Jan 4, 2016
Posts
25
Reaction score
14
Habarini wana nzengo,

Nichukue fursa hii kutahadharisha kile kinachoendelea nchini na mamlaka husika zinafumbua macho na wala hazichukui hatua stahiki.

Inashangaza kwamba kwenye miji mingi nchini biashara hufanywa holela pasipo kuzingatia sehemu husiku, na hivyo utakuta wafanyabiashara wameziba njia za waenda kwa miguu kwa kupanga biashara njiani.

Sijui ni nani aliwaambia kwamba ukipanga biashara njiani ndipo inanunuliwa? Kwanza tunakosa wingo mkubwa sana na kukusanya kodi kwa hawa wanaopanga biashara njiani.
Lakini si hivyo tu bali miundo mbinu kama mitaro hualibiwa kuwa kutupa taka ngumu na plastic ambazo baadaye huziba na kufanya serikali igharimie tena ujenzi wa miundo mbinu hiyo.

Kadhia kwa waenda kwa miguu na wasafiri wengine, ambapo sehemu ambazo wangepita wao ndiko kulikopangwa bishaa na hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi kwa ujumla.

Mara nyingi nasikia kuwa viongozi wetu wanasafiri nje ya nchi kwa ziara mbalimbali, sina hakika kama wanaposafiri wanaenda wakiwa vichwa wazi au wamefungwa vitambaa machoni, sijui ni nini wanajifunza kwa nchi nyingine wanazotembelea, hii nayo inahitaji wazungu kutufundisha kuwa barabara zinatakiwa kuwa wazi kama zilivyojengwa ili kufuata utawala wa haki na sheria? Hizo 4R zinazosikika kwenye vyombo vya habari ni kejeli au kiini macho?( Ni mjumbe tu kuwaletea habari).

Mara nyingi nimesikia kuwa, nendeni Rwanda mkaone! Hivi Hiyo Rwanda inayosifiwa kwa usafi wenyewe hawana sheria na taratibu? Ni kwa sababu wameamua kufuata sheria na utaratibu za nchi. Je? TANZANIA tunashindwa wapi? Hii nayo mpaka mzungu aje kweli? Je? Rwanda inatawaliwa na wazungu? kwa nini wao waweze na sisi tushindwe?

Nimekuwa ninafuatilia sana habari za Rais kijana wa Burkina Faso ambaye amechukia madaraka juzi tu 2022, kwa hatua madhubuti anazochukua kuiletea maendeleo nchi yake pamoja na kwamba anapigwa vita ndani na nje lakini ameonyesha uthubutu, na sasa eti tunaenda kujifunza kwa raisi Traore, sasa anajenga masoko kila sehemu na amepiga marufuku mtu awaye yote kufanya biashara holela, watu wote wanapaswa kuuza bidhaa zao kwenye masoko yanayotambuliwa.


Ninashukuru nimefanikiwa kutembelea nchi nyingi za ulaya ambazo ndiyo tunazotolea mifano kuwa hatuwezi kubaki kama kisiwa lazima tujifunze kwa wenzetu, lakini tunajifunza nini? Au ndiyo tunazidi kuharibu kabisa, inashangaza sana!


Mwezi Oktoba ni mwezi wa uchaguzi, na karibuni utaona wafanyabiashara wakifanya biashara kila sehemu hata hospitalini, kwenye ofisi za serikali na kila sehemu, na ndipo utakaposikia kuwa msiwabughudhi wapiga kura wangu, yaani kila mtu afanye kila apendalo sehemu yoyote eti ndiyo kuwajali wananchi kweli? Mimi nasema hapana, kuna namna nzuri ya kuwasaidia ili nchi iwe na mwonekano mzuri.

Chukulia mfano pale Temeke mwisho, ambako gereji ziko barabarani, pamoja na kwamba zinachafua mazingira kwa mafuta na oil inayomwagwa hovyo ardhini na barabarani, lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa, viongozi wapo, serikali na mamlaka zote zinazohusika zinaona lakini nani amfunge paka kengele, hii nayo inataka mzungu aje atufundishe kupanga mji vizuri na kuondoa takataka hizo? Inashangaza sana.

Nilikuwa napita tu na kuonyesha pale ambacho hatufanyi vizuri. Basi tukiongoka tuwaimarishe ndugu zetu ili nchi iende vizuri, naondoka huku nikiweweseka, langu jina ni Sendi Muwanga.
 
Tuna changamoto sana nchi hii. Ukustaajabu ya Gongolamboto utayaona ya mbagala!
 
Inashangaza kwamba kwenye miji mingi nchini biashara hufanywa holela pasipo kuzingatia sehemu husiku, na hivyo utakuta wafanyabiashara wameziba njia za waenda kwa miguu kwa kupanga biashara njiani
Hili linanikera sana, miji inayakuwa ya hovyo, barabara nzuri Mbezi Luis, Mbagala, Mwenge na sasa hivi Gombs kuna pavements pembeni zote ni kwaajili ya biashara.

Huwa najiuliza Wizara ya viwanda na biashara ina jukumu gani kama haiwezi jenga masoko kuweka miundo mbinu mizuri kila mtu afaidi? A lawless country.
 
Back
Top Bottom