Ufahamu mzunguko wa uchaguzi Tanzania

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Ndugu wanajamvi, Tanzania Kama ilivyo nyingine duniani huendesha shughuli za Uchaguzi kwa mafanikio makubwa kwa kutumia utaratibu wa mzunguko wa Uchaguzi (Election Cycle) ambao shughuli zake hugawanywa katika awamu tatu yaani 1. Kabla ya Uchaguzi 2. Wakati wa Uchaguzi na 3. Baada ya Uchaguzi

Katika awamu zote hizo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hutekeleza mfumo wa mzunguko wa Uchaguzi kama ifuatavyo.

1. KABLA YA UCHAGUZI.
Katika kipindi hiki shughuli zinazofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni pamoja na
  • Uandaaji wa Bajeti
  • Uandikishaji wa Wapiga Kura
  • Ununuzi wa vifaa
  • Uandaaji wa Kalenda na Mpango wa Utekelezaji
  • Marekebisho ya Sheria na Maelekezo ya Watendaji na Wadau wa Uchaguzi
  • Mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi na
  • Utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura.
2. WAKATI WA UCHAGUZI.
Katika kipindi hiki Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya shughuli zifuatazo
  • Uteuzi wa wagombea
  • Uratibu wa Kampeni za Wagombea
  • Utekelezaji wa Kamati za Maadili
  • Usajili wa Watazamaji wa Uchaguzi
  • Kuchapa na Kusambaza Karatasi za Kura
  • Kugawa na Kusambaza Vifaa vya Uchaguzi
  • Upigaji Kura
  • Kuhesabu Kura na
  • Kutangaza Matokeo ya Uchaguzi
3. BAADA YA UCHAGUZI
Katika kipindi hicho Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya shughuli zifuatazo
  • Kuandaa taarifa ya Uchaguzi Mkuu
  • Kushughulikia Kesi za Uchaguzi
  • Kufanya Tathmini ya Baada ya Uchaguzi Mkuu
  • Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi
  • Kupitia na Kuboresha Daftari la wapiga Kura
  • Kupitia na Kuboresha Mifumo ya Uchaguzi
  • Kupitia na kuboresha mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi
  • Kupitia na kuboresha muundo wa Tume
  • Ukaguzi wa matumizi ya fedha na vifaa vilivyotumika katika Uchaguzi Mkuu
  • Kupitia Mpango Mkakati na
  • Kuandaa Mpango Kazi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaofuata.

Chanzo: NEC
 
Back
Top Bottom