Ufafanuzi wakuu juu ya mahusiano yangu

Ufafanuzi wakuu juu ya mahusiano yangu

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
496
Reaction score
379
Napenda kutoa taarifa kuwa ni kweli nili-post thread hapa ikiwa na kichwa cha habari, "Ninyi Mabinti acheni hizo"

Katika thread ile niliongelea namna nilivyopata misuko suko ya kimahusiano katika kumpata mchumba wangu, kwanza, ni kweli nilimpata, ila sasa tatizo lingine limejitokeza hapa kati kati.

Kwanza hadi sasa hatujaoana, kisa?

Baba ya binti amekuwa ni mtu wa safari nyingi sana, kila tukipanga tarehe ya kupeleka posa then mahari anaridhia vizuri sana lakini sasa siku moja kabla wanaahirisha, wao wanasema kuwa baba mara ameenda moshi, mara kesho atakuwa na wageni kutoka Uswisi mara yupo mwanza!

Mimi nikaongea na baba yake moja kwa moja, akasema bado yupo busy sana, baba yake ni mfanya biashara wa kahawa, so huwa anaenda moshi kuangalia kahawa,

sasa mimi hadi nimechoka coz, toka mwaka jana wana-postpone hadi hii leo.

Wazazi wangu waliniita na kunipa baraka mpya kuwa nitafute binti mwingine na huyo nimweleze hali halisi, nimemweleza binti na yeye hadi sasa yupo kimya hajatoa jibu lolote.

Asanteni, najua kuna waliopata usumbufu katika hili baada ya kuona tena natafuta mke.
 
Ushauri wangu kwako ndugu, fata moyo wako kwasababu ww ndiye muoaji hivo ww ndiye utayeishi na huyo mke. Nakushauri ufate moyo wako
 
Kifedha hali yako na familia kiujumla ipoje?

Upande wa binti familia yao ipoje kifedha?
 
Kifedha hali yako na familia kiujumla ipoje?

Upande wa binti familia yao ipoje kifedha?

Kwao binti ndo hivo binti ni mwalimu, baba yake ndo hivo ni mfanyabiashara na mama yake ni mama wa home but ana duka hapa kwake.
 
piga ''mbami'' wewe...!! Watkufanya boya mpaka lini? Watu wengne bana...
 
so hii thread ni maalum kwa kusaka mchumba?...maana sijaelewa!

naweza sema ndiyo au hapana maana kuna reference ya mwaka jana nilokuwa nashukuru but jana nimepost nyingine ya kusaka mchumba, sasa kuna watu wanaweza kwa namna moja au nyingine kudhani kuwa mimi ni tapeli, but am not of such type.
 
Kifedha hali yako na familia kiujumla ipoje?

Upande wa binti familia yao ipoje kifedha?

Kwetu, Baba ni Ofisa fulani serikalini na mimi nina kazi yangu, mama mfanyabiashara.
 
Mi naona hapo hakuna mke... jus fynd another one na nijuavyo mimi, posa anapokea uncle and not Daddy
 
piga ''mbami'' wewe...!! Watkufanya boya mpaka lini? Watu wengne bana...

Hapana mkuu, wazazi wangu hawatapenda wao wanataka procedure zote zifuatwe ndo niweze kumfaidi vizuri.
 
Mi naona hapo hakuna mke... jus fynd another one na nijuavyo mimi, posa anapokea uncle and not Daddy

Ndo hapo sasa! baba yake anasema angependa na yeye awepo, sasa yupo too busy toka mwaka jana hadi sasa!
 
ushauri wangu mke ni kifungo cha maisha kama hivi ni mwazo hata ndoa babdo mambo yamekuwa hivi sijui miaka 20 ijayo kama mnaweza kuwa na furaha ,....... usilazimishe ndoa rafiki isijekuwa mateso badae....

kama binti ni mchaga we ni cha saka ujue hapo huna chako labda binti akomae......haina maana wachaga wote wanafanya hivyo...

kama we ni mchaga jaribu kufuatilia ukoo wako na ukoo wake yawezekana kuna namna ambavyo inaleta vikwazo...
muulize binti je yupo serious?
 
Hapana mkuu, wazazi wangu hawatapenda wao wanataka procedure zote zifuatwe ndo niweze kumfaidi vizuri.

anhaaa...; procedure.!! Labolatory hapo si ndio??
Endelea fuata procedure...
 
ushauri wangu mke ni kifungo cha maisha kama hivi ni mwazo hata ndoa babdo mambo yamekuwa hivi sijui miaka 20 ijayo kama mnaweza kuwa na furaha ,....... usilazimishe ndoa rafiki isijekuwa mateso badae....

kama binti ni mchaga we ni cha saka ujue hapo huna chako labda binti akomae......haina maana wachaga wote wanafanya hivyo...

kama we ni mchaga jaribu kufuatilia ukoo wako na ukoo wake yawezekana kuna namna ambavyo inaleta vikwazo...
muulize binti je yupo serious?

anafuata procedure,,, nampa pole sana.
 
hapo ndugu naona angalia ustaarabu mwingine.

ok, ndo maana jana nimeanza process upya za kusaka mke mwingine, ila nikaona yafaa nitoe ufafanuzi kwa yaliyotokea ila watu wengine wasije dhani kuwa mimi ni tapeli na un-seriousness.
 
Kwetu, Baba ni Ofisa fulani serikalini na mimi nina kazi yangu, mama mfanyabiashara.

Okey' kwaakili yakawaida yakibinaadam niliyonayo nadhani kuna haya yafuatayo;

1) hiyo familia ina aina fulani ya kiburi na dharau

2) huenda binti hakupendi' ila kuna kitu ambacho kinamfanya ashindwe kukupa makavu live kwamba hayupo tayari' kwahiyo anamtumia babayake kumdefence

3) jichunguze kwanza' huanda kuna kitu au tabia fulani ambayo haiwapendezi wao toka kwako nawewe haujaitambua' hivyo wao wapo mguu ndani' mguu nje.


Kwa uzoefu mdogo nilionao familia nyingi zakiume ndio zinakuwaga na excuse nyingi wakati wa kuoa' kwahiyo maranyingi zinapanga nakupangua hizo tarehe za mahali!

Wakati kwaupande wa mwanamke' familia wanakuwa wanaitamani siku hiyo ifike haraka' maana ni heshima kwao na kwajamii waliyopo!

Sasa iweje hawa wakwe zako watarajiwa wao ndo wawe kikwazo cha wewe kushindwa kuoa binti yao?

Tena eti sababu Mzee wake yupo busy' tena sio maramoja several times?

Au kutoa mahali ni zoezi la wiki moja kikwao?
 
Back
Top Bottom