Ufafanuzi wa Mapigo Kumi ya Wamisri!

Bible yasema kuwa MAPIGO HAYO HAYAKUWAPATA WANA WA ISRAELI ..... yaliwapata WAMISRI TU .... Je hao vyura, chawa, maji kuwa damu, VIFO VYA WAZALIWA WA KWANZA nk. majanga yote hayo yaliwapata WAMISRI pekee kwa kuwa WANA WA ISRAEL hawakuwamo MISRI? .... Why na wao yasiwapate?
Kumbuka wana wa Israeli walikuwa na eneo lao maalum la kuishi. Ndani ya nchi ya misri kuliteuliwa eneo la makazi kwa ajili ya waisraeli. Eneo hili liliitwa Rameses, ambalo farao alimwambia Yosef awape nduguze. Eneo hili lilikuwa bora, ardhi yenye rutuba.
 
sammyluv mkuu labda kama utakuwa umesoma kwa haraka haraka,ila popote panapomuhusu Mungu wa Waisraeli nimeanza na "M" kubwa,na pale pa miungu ya Wamisri nimeanza na "M" ndogo!
 
Maji ya mto nili yaligeuka tope, sababu ya mvua kubwa iliyonyesha nyanda za juu. Chura si mvumilivu kwenye tope, hasa akitaka kuzaliana.
Nikuchekeshe kidogo? Chawa waliibuka baada ya wamisri kuishi siku nyingi bila kuoga wala kusafisha mavazi yao, baada ya kukosa maji safi.
funny huh.

Hata farao aikuwa haogi ata mavazi yake hayasafishwi.

Waelezeee watu kuhusu ile mvua ya mawe na nzige pia.

siko vile nilivyokuwa, haimaanishi nipo tofauti.
 
Kumbuka wana wa Israeli walikuwa na eneo lao maalum la kuishi. Ndani ya nchi ya misri kuliteuliwa eneo la makazi kwa ajili ya waisraeli. Eneo hili liliitwa Rameses, ambalo farao alimwambia Yosef awape nduguze. Eneo hili lilikuwa bora, ardhi yenye rutuba.
Correction: Eneo walopewa WAEBRANIA liliitwa GOSHEN na si RAMESES kama usemavyo wewe .....

Nikirejea kuhusu MAPIGO si ENEO lilowaponya WAEBRANIA na HASIRA ya Mungu bali ni KINGA yake kwao kwa maana walikuwa ni taifa TEULE ....

Mungu alikusudia kuwalinda WAEBRANIA na hayo MAPIGO yalowapata WAMISRI ili wairejee nchi ya AHADI alokuwa amemwahidi Nabii IBRAHIM .... na ndo mana alitoa MAAGIZO wachinje, wale na kisha WAPAKAZE DAMU KATIKA MIIMO YA MILANGO YAO ili wajiepushe na madhara ya MALAIKA atakaepita usiku AKIDHURU WAZALIWA WA KWANZA wa mwanadamu na mnyama .....

WAEBRANIA walipona na VIFO VYA WAZALIWA WA KWANZA vilivyowapata WAMISRI si kwa kuwa waliishi GOSHEN bali kwa kuwa Mungu aliamua kuwalinda kwa KINGA YA DAMU KTK MIIMO YA MILANGO YAO ..... Jambo ambalo kwa WAMISRI halikufanyika ....
 
Haya mapigo kumi yana nadharia mbalimbali. Kuna nadhalia moja, ambayo na mimi naiamini sana inasema kama ifuatavyo:
  1. PIGO LA NILE KUWA DAMU: Mto naili hutiririsha maji yake kutoka nyanda za juu za Ethiopia na sudani. Huko unakoanzia kuna nchi yenye udongo mwekundu. Ilitokea mvua kubwe ilinyesha, udongo mwekundu ukasombwa na hatimae mto nile kuwa mwekundu sababu ya udongo. maji ya nili hayakugeuka damu, bali lilikuwa tope jekundu.
  2. PIGO LA VYURA: Baada ya mto nili kujaa tope jekundu, vyura wake (mtoni) walishindwa kuishi katika hali ile na iliwalazimu kutoka nje ya mto, hivyo kulandalanda katika nchi ya misri wakitafuta maji safi kwa ajili ya kuzaliana, ikizingatiwa kipindi cha maji mengi ndipo vyura huzaliana.
  3. PIGO LA NZI: Wale vyura waliokimbia mtoni na kurandaranda nchi kavu waliishia kufa kwa sababu ya kutozoea mazingira. hivyo inzi wakapata ahueni ya kuzaliana kwa sababu ya uchafu uliosababishwa na kufa kwa vyura hao.
  4. MARADHI: Kuenea kwa maiti/mizoga ya vyura, harufu mbaya na kuzagaa kwa mainzi kulisababisha nchi kukumbwa na maradhi ya mlipuko, ukiwemo ugonjwa wa majipu.
  5. NYOKA.: Hawa viumbe walienea nchini wakisaka vyura. vyura walipotoweka mitoni iliwalazimu nyoka kutafuta vyura wengine au chakula kingine popote kilipo.
  6. VIFO; hivi vilitokea sababu ya maradhi kama iliyoainishwa hapo juu, pamoja na kukosekana ka maji safi ya kunywa.
That means hiyo mvua iliyofanya mto ukajaa tope lenye rangi nyekundu ilinyesha mara moja tu katika historia ya dunia na haikuwahi kunyesha tena?
 
Soma kitabu cha Mwanzo 47:11. waisraeli walitengamana makazi na waisrael. Matatizo waliyopata wamisri hayakuingia katika eneo waliloishi waisrael
Narejea tena MSISITIZO kupona kwa WAEBRANIA si kwa sababu waliishi ktk eneo la GOSHEN bali ni MKONO WA MUNGU (Nia ya Mungu kuwaokoa)

Kwa maelezo zaidi soma BIBLIA kwa UTULIVU na UMAKINI
KUTOKA 12:7,12,13,29

KUTOKA 12:13 .... Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo, nami nitakapoiona ile DAMU, NITAPITA JUU yenu (pass over) lisiwapate pigo lolote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri ....
 
Maji ya mto nili yaligeuka tope, sababu ya mvua kubwa iliyonyesha nyanda za juu. Chura si mvumilivu kwenye tope, hasa akitaka kuzaliana.
Nikuchekeshe kidogo? Chawa waliibuka baada ya wamisri kuishi siku nyingi bila kuoga wala kusafisha mavazi yao, baada ya kukosa maji safi.
Haya kwa nini kwenye pigo la mwisho ni mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na mnyama ndo walikufa?
 
Haya mapigo kumi yana nadharia mbalimbali. Kuna nadhalia moja, ambayo na mimi naiamini sana inasema kama ifuatavyo:
  1. PIGO LA NILE KUWA DAMU: Mto naili hutiririsha maji yake kutoka nyanda za juu za Ethiopia na sudani. Huko unakoanzia kuna nchi yenye udongo mwekundu. Ilitokea mvua kubwe ilinyesha, udongo mwekundu ukasombwa na hatimae mto nile kuwa mwekundu sababu ya udongo. maji ya nili hayakugeuka damu, bali lilikuwa tope jekundu.
  2. PIGO LA VYURA: Baada ya mto nili kujaa tope jekundu, vyura wake (mtoni) walishindwa kuishi katika hali ile na iliwalazimu kutoka nje ya mto, hivyo kulandalanda katika nchi ya misri wakitafuta maji safi kwa ajili ya kuzaliana, ikizingatiwa kipindi cha maji mengi ndipo vyura huzaliana.
  3. PIGO LA NZI: Wale vyura waliokimbia mtoni na kurandaranda nchi kavu waliishia kufa kwa sababu ya kutozoea mazingira. hivyo inzi wakapata ahueni ya kuzaliana kwa sababu ya uchafu uliosababishwa na kufa kwa vyura hao.
  4. MARADHI: Kuenea kwa maiti/mizoga ya vyura, harufu mbaya na kuzagaa kwa mainzi kulisababisha nchi kukumbwa na maradhi ya mlipuko, ukiwemo ugonjwa wa majipu.
  5. NYOKA.: Hawa viumbe walienea nchini wakisaka vyura. vyura walipotoweka mitoni iliwalazimu nyoka kutafuta vyura wengine au chakula kingine popote kilipo.
  6. VIFO; hivi vilitokea sababu ya maradhi kama iliyoainishwa hapo juu, pamoja na kukosekana ka maji safi ya kunywa.
Kwa hiyo unataka kutuaminisha ile milima ya udongo mwekundu ili safishika ikawa mieupe. Au mvua hainyeshi tena katika milima yenye udongo mwekundu? Maana tungesikiaga hilo tukio likijirudia pindi mvua zinyeshapo kwenye milima ile. Ulicho andika ni sawa na Theory ya binaadamu alianza kama nyani!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom