Ufafanuzi wa IPTL kwa Bunge

Ufafanuzi wa IPTL kwa Bunge

Ukweli ndio huo Sasa nendeni mkalale. Au mtukaneni jaji Utamwa.
 
Unasema mahakama iliondoa IPTL kwenye ufilisi na kutambua PAP kama mmiliki wa asilimia 100% wa IPTL, Je unamaanisha directors of IPTL were in charge with the dealings of the company na wakauza IPTL kwa PAP?

If this is the case, what evidence do you have that PAP legally owns IPTL? PAP claims to have acquired IPTL in 2010 huku PAP hiyo hiyo ulikua incorporated in 2011.

At the same time, mbona majority shareholder Mechmar hamtambui PAP?

Again, when did IPTL (specifically Mechmar) sell its shares to PAP? Keep in mind SCB-HK has an interest over IPTL shares.

Katika maelezo yako hakuna mahali unapoelezea jinsi PAP ilivyonunua IPTL kwa sababu unajua hapa ndo utata ulipo.

Unasema tu PAP ametambuliwa kama mmiliki wa IPTL kwa asilimia 100% bila kithibitisho chochote.

Malipo kwa PAP ni batili na hapo ndipo wizi ulipofanyika.
 
huyu IPTL atakua ni mtu mkubwa sana,hii taarifa ya ufafanuzi ambayo haijasomwa mjengoni kaipata wapi,sio muhongo kweli huyu au maswi?
 
Huu wizi kadraft Naibu waziri wa fedha. Yeye ndie signatory wa akaunti.
 
Taarifa ya serikali???Jamani huyu mtu IPTL kajiunga leo leo na anaibuka na hizi taarifa,kuna nyingine anamtuhumu Zito na Mengi kwa kuchochea huu mgogoro!Jamani huku kwetu hatuna umeme sijui ndio IPTL wamekasirika?? IPTL naomba kujua hii taarifa ya serikali imesomwa lini bungeni na nani ameiwasilisha?Pia wewe kama muhasibu wa TANESCO imekuwaje haraka sana uipate ripoti hii!!

Jamani huyu siyo mhasibu tu! Huyu ni Sospeter mwenyewe amejichanganya tu akawahi kuitupia hapa kabla ya bungeni. Naona nondo za Kafulia zimemchanganya mpaka amepanic!!
 
Last edited by a moderator:
tume ikiundwa ndo itakata mzizi wa fitina,vinginevyo itakuwa hamna kitu. Itakuwa kama Kinana anvyowadanganya watanzania kuwa KATIBA MPYA haina maana,sijui bila kuwa nakitaba itawabana vip hawa wanaotafuna mabilion yote haya. KINANA inabidi achukuzwe akiri atakuwa hayuko sawa upstairs.
 
At the same time, mbona majority shareholder Mechmar hamtambui PAP?

Again, when did IPTL (specifically Mechmar) sell its shares to PAP? Keep in mind SCB-HK has an interest over IPTL shares.
Huo ndiyo wizi wa wazi
 
Huu ni wizi mtupu! watu wenye kufanya tafakuri hawawezi danganyika kiraisi hivyo, kwa propaganda za huyu IPTL. The issues na facts are very simple:-

1. Ni kweli kuwa fedha ziliwekwa kwenye akaunti ya Escrow zilikuwa zinalipwa na TANESCO kutokana na mgogoro wa gharama za malipo kati ya TANESCO na IPTL. TANESCO ilidai kuwa inalipa gharama za juu kutokana na IPTL kutumia fedha za mkopo kama mtaji, kukokotoa gharama za umeme wakati fedha halisi za mtaji wa IPTL si zaidi ya Dola za Marekani 1,000. Hivyo basi wakakubaliana wafungue Escrow account na mgogoro wao upelekwe kenye mahakama ya usuluhishi ya ICSID marekani, kupata tafsiri jinsi ya kukotoa hizi garama na kesi itakpoisha hesabu zipigwe TANESCO na IPTL wagawane fedha za escrow, kulingana na uamuzi wa mahakama. Kesi hii ipo na haijafikia tamati, kama inavyodaiwa, lakini wajanja washavuta fedha zao za ugoro.

2. Kesi iliyokuwapo mbele ya jaji Utamwa, haikuhusu fedha za Escrow, bali ilikuwa ni ugomnvi wa IPTL shareholders. Rugemalira kupitia kampuni yake VIP Engineering, alifungua kesi mahakama kuu akiomba IPTL itangazwe mufilisi aka iwe wound up, kwa madai mbalimbali yakiwepo ya fraud na opression of minority shareholders . TANESCO was not a part to this dispute nor was the escow money, ila walichofanya wajanja kwenye kesi hii ni kucompromise the claims, create a ruse settlement and drag the escrow money into this settlement na kugawana ngawira za TANESCO kwa kisingizio cha uamuzi wa mahakama!

3. etc
 
Swali la kujiuliza kwa nini release ya pesa haikuhusisha wabia wote VIP na Mechram ya malaysia?Jee haioni kuwa huyu mbia mkubwa mwenye mitambo alikua ni muhimu ktk deal lolote lile?

Hii isikuumize kichwa chako bali unatakiwa kumjua na kumchambua kwanza Jaji (Kumbuka wale majaji walioteuliwa fasta fasta) aliyetoa maamuzi hayo ya kesi tatanishi ya IPTL akishirikiana na hao wanasiasa wachumia tumbo pamoja na Bosi aliyekuwapo TANESCO wakati huo, halafu pia kumbuka ndani ya kesi ile mlikuwa na IMMMA Advocates ambao tayari huko nyuma wana sifa nyingi na kashfa za michoro kama hii e.g Deepgreen Finance Ltd, Tangold, etc, Kumbuka pia kuwa Ridhwan Kikwete alishawahi kufanya kazi na IMMMA advocates hivyo kuunganisha mambo pale White House kwao ni kama mgonjwa na uji...anyway tutafika tu!
 
watu wanapiga mbesa kwa kwenda mbele ndani ya nchi yangu hii hii kwa mtaji wa lap top na rangi zao tu? Halafu mie napozwa na ka wimbo ka ruge tu.....hellooo helloo tanzania eeehx2

na serikali inajitoa ufahamu kabisa kuwa sio muhusika na wala hizo pesa hazimhusu,wakati huo huo tena yeye ni mdhamini????

Kidumu chama cha mapinduzi

kidumu chama twawala
 
Nasoma na kuitafakaaari kwa umakiiiini ili
Nipime mbivu na mbichi bila ushabiki
 
Ni muhimu mkataba baina ya IPTL na serikali ukawekwa hadharani kwani mkataba huo ambao ulisainiwa wakati chama kimeshika hatamu ya uongozi, Zipo taarifa Kwamba uliasainiwa na viongozi wa chama, sio serikali. Kuna haja ya serikali kujisafisha na taarifa hizi.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Juzi IPTL kaja na hoja ya kumtetea waziri akijiita akauntanti wa TANESCO na akimponda Nimrod Mkono. Wajanja tulijua fix tuu.
 
Umejiunga 12 MAY 2014 .........Naona una shughuli maalum.

Ni kweli tulimshtukia alikuja na thread ya kutetea wizi na kumsifia waziri huku akimponda mkono advocates eti kawalia Tanesco mabilion na kesi haikuwa upande wao. Mkono si ndiyo massm conduit?
 
maswali ni mengi, majibu yanahitajika sana, vema tume ikaundwa kuchunguza hii kashfa.
 
Back
Top Bottom