Ufafanuzi kuhusu Uungu

Ufafanuzi kuhusu Uungu

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Wapendwa WanaJF

Katika kitabu cha ufunuo 5:1-14 imeweka bayana kuhusu Mungu na kufunua uongo wa ile nadharia inayodai kuwa Baba ndiye Huyo huyo Mwana na kwamba ndiye huyohuyo Roho. Kitabu cha Ufunuo kimeweka Bayana kuwa Baba na Mwana ni wawili tofauti na kwamba sii Mtu Mmoja. Baba sii Mwana na Mwana sii Baba. Baba na Mwana ni nafsi Mbili tofauti zilizo Umoja. Katika Ufu5:1-5 Biblia inamfunua Mungu Baba akiwa ameketi katika Kiti cha Enzi akiwa ameshikilia Kitabu ambacho kimeandikwa ndani na nyuma na kimetiwa Muhuri saba. Katika Kitabu cha Ufu5:6-7 tunamwona Yesu akiwa anawakilishwa na Mwanakondoo aliyechinjwa na kisha akamwendea Mungu Baba, na akakitwaa kile kitabu kilichoko Mkononi mwake na kuvunja Muhuri zake.

Kama Baba ndo huyohuyo Mwana kama baadhi ya watu wanavyo sema haiingii akilini kwamba Baba ameketi kitini pa enzi, halafu huyohuyo ajiendee Mwenyewe na kukitwaa kitabu ambacho kiko katika Mkono ambao ni wa kwake Mwenyewe!!! Lazima Baba na Mwana wawe ni nafsi Mbili tofauti kabisa. Lakini pia Ufunuo sura ya tano inawapinga wale wanaodai kuwa Imetupasa kumwabudu Baba pekee na sii Mwana, na kudai kuwa ni dhambi kumwabudu Mwana. Ufunuo sura ya tano imeweka bayana kuwa Wote Baba na Mwana wanaabudiwa na viumbe vyote vya Mbinguni na kwamba Mwana anayo haki sawa ya Kuabudiwa kama Baba. Yesu kama Mwana wa Mungu, ana haki ya kustahili Ibada na kusujudiwa kama vile Baba yake wa Mbinguni. Biblia yasema hivi: “Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele. Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu. [Ufu5:13-14]

Katika kitabu cha ufunuo5:6 Kristo amefunuliwa kama Mwanakondoo mwenye Macho saba na macho saba yamefananuliwa kuwa ni Roho saba za Mungu ambazo zimetumwa dunia yote. Kulingana na Kitabu cha Ufunuo Roho Mtakatifu ni Macho ya Mwanakondoo. Macho huwa ni viungo na sehemu ya mnyama hivyo Roho Mtakatifu ni Roho ya Mungu na Roho ya Yesu. Roho Mtakatifu anamilikiwa na Mungu pamoja na Kristo na ambaye hutumwa na Mungu na Kristo dunia yote ili kumwakilisha Mungu na Kristo na kuwafanya Mungu na Kristo waweze kuwepo kila Mahali. Lakini pia tunaona katika kitabu cha Ufunuo kuwa Roho Mtakatifu ni Roho ambayo hutoka kwa Mungu na hutumwa kama mjumbe huru na anayejitegemea mbali na Baba na Mwana. Ingawa Roho sii Mtu mwingine ama Mungu mwingine aliye tofauti na Mungu na Kristo bali ni Roho yao, lakini Mungu anaweza kuituma Roho yake kama Mjumbe huru na ambaye anajitegemea Mwenyewe.

Karibuni kwa maoni
Mbarikiwe sana
 
Ngoja waje wenyewe, but nachojua mimi kuna Mungu baba, Mungu mwana, na roho mtakatifu, hawa hufanya kazi pamoja kwa umoja.
 
Kwanza yakupasa uelewe kuwa mungu siyo kitu (matter) so huwezi kufananisha na kitu chochote. Unaposoma maandiko mbalimbali kuhusu mungu huwezi elewa sababu waandishi wanatumia mifano ya uwili (duality) katika kufikisha mawazo yao na mungu hayupo katika duality yupo katika oneness ndio maana husikia mungu yupo mahali popote.
In logic kitu ambacho kipo mahali popote basi hakipo hapa wala pale that's why nikasema mungu sio kitu.
Ili uweze kuelewa mungu njia pekee unaweza kufanya ni kuwa mungu. Leo nikikuona wewe naweza kukudefine hivi na nikahisi nakujua. Akija mwingine atakudefine vile na kuhisi anakujua. Sisi wawili tutakuwa na majibu tofauti lakini wewe huwezi kuwa tofauti na ulivo na unajijua. Jibu pekee kuhusu wewe unalo mwenyewe. So ukitaka kumjua mungu ni vema ukawa mungu ili usiwe na misconception.
Kuwa mungu ni nini. Kuwa mungu ni kuondoka katika duality na kuwa katika oneness. Hapo utakuwa umepata majibu ambayo hayana perception. Hakuna mungu baba mwana wa nani. Mungu ni mungu. Hayo maandiko yapo katika duality ndio maana yanachanganya kuelewa. Ila ukipata hata chance kidogo katika oneness utaanza kuelewa.
Kuna maandiko yanasema kuwa yesu alisema baba yupo ndani yangu na mimi nipo ndani ya baba. Pia kuna sehemu wanasema hapo zamani kulikuwa na neno na neno alikuwapo kwa mungu na neno alikuwa mungu. Pia wakasema milima na kila kitu vitapita kasoro neno. Je neno ni nini? Kile kilichopo milele ndio kitabaki ambacho ni neno. Neno ndio mungu. Kwa mungu hakuna duality yani leo jana na kesho kuna now ambayo ndio milele. So huwezi kuelewa mungu kama kuna duality unatemnelea........

Nadhani naeleweka kidogo
 
Tatizo lako kuu wewe mtoa mada ni kumfananisha Mungu na binadamu. Hujasoma Biblia na kuitafakari hivyo huna moral authority (haki) ya kuandika ulichoandika. Biblia iko wazi kwamba Mungu ni roho. Sasa wewe unazungumzia Baba kuketi kwenye kiti na Mwana kuketi kwenye kiti kingine....Nikuulize:-Kama Mungu ni roho, je, Roho zinakaa kwenye kiti?

Unamzungumzia Mungu ambaye ni Roho kama unavyomzungumia mtu
ambaye ana mwili. Ni vitu viwili tofauti. Kwa hivyo hata ulinganisho wako unaotaka kuuleta hauna msingi wala manriki.

Hivi wewe mtoa mada unajua kwamba Biblia inaeleza kwamba Mungu ana nafsi tatu? Na hiyo hiyo Biblia inasema wewe uliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu (kwa sababu na wewe pia unazo nafsi tatu)? Unajua kwamba wewe una mwili tunaouona na nafsi ambayo hatuioni na roho ambayo pia hautioni? Unajua kwamba nafsi yako na roho yako ni nafsi zako mbili zinazotofautiana na ndio maana nafsi yako inaweza kumtamani mke wa mtu (lakini kama wewe ni mcha Mungu) roho yako inaikataza nafsi yako kwa hiyo mwili wako (ambao unasukumwa na nafsi-felings) unaacha kutenda dhambi?

Nakushauri mtoa mada kasome Biblia UPYAAA....
 
Tatizo lako kuu wewe mtoa mada ni kumfananisha Mungu na binadamu. Hujasoma Biblia na kuitafakari hivyo huna moral authority (haki) ya kuandika ulichoandika. Biblia iko wazi kwamba Mungu ni roho. Sasa wewe unazungumzia Baba kuketi kwenye kiti na Mwana kuketi kwenye kiti kingine....Nikuulize:-Kama Mungu ni roho, je, Roho zinakaa kwenye kiti?

Unamzungumzia Mungu ambaye ni Roho kama unavyomzungumia mtu
ambaye ana mwili. Ni vitu viwili tofauti. Kwa hivyo hata ulinganisho wako unaotaka kuuleta hauna msingi wala manriki.

Hivi wewe mtoa mada unajua kwamba Biblia inaeleza kwamba Mungu ana nafsi tatu? Na hiyo hiyo Biblia inasema wewe uliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu (kwa sababu na wewe pia unazo nafsi tatu)? Unajua kwamba wewe una mwili tunaouona na nafsi ambayo hatuioni na roho ambayo pia hautioni? Unajua kwamba nafsi yako na roho yako ni nafsi zako mbili zinazotofautiana na ndio maana nafsi yako inaweza kumtamani mke wa mtu (lakini kama wewe ni mcha Mungu) roho yako inaikataza nafsi yako kwa hiyo mwili wako (ambao unasukumwa na nafsi-felings) unaacha kutenda dhambi?

Nakushauri mtoa mada kasome Biblia UPYAAA....
Mpendwa itapendeza zaidi ukitupatia vifungu au fungu linalosema kuwa Mungu anazo nafsi tatu ili sasa mjadala ukae vizuri.
 
Nenda kasome ufunuo 4 na ufunuo 5 Mungu amefunuliwa sii kama Roho fulani isiyo na Umbo Bali ingawa Mungu ni Roho, Mungu analo umbo pia kwani alimuumba Binadamu kwa mfano wake. Ufunuo 4 nq Tano sijaonyeshwa mimi mpendwa. Nenda kasome utaona yohana ameonyeshwa mmoja ameketi ktk kiti cha Enzi na mwonekano wake umetajwa. Na ktk Ufunuo5 Huyo aliyeketi ktk kiti cha Enzi anafunuliwa tena akiwa ameshikilia kitabu. Roho isiyo na Umbo haiwezi kuwa na mikono na kushikilia kitabu.
 
Back
Top Bottom