Ufafanuzi kuhusu elimu ya Mbura Chiragwile

Ufafanuzi kuhusu elimu ya Mbura Chiragwile

Team Mbura

New Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
1
Reaction score
0
Wakuu,

Kuna uzi mmoja ambao uliletwa jana,tarehe 15/01/2015 ukimnadi Kamanda Mbura Chiragwile kuingia katika Harakati za Kumng'oa ndugu Nimrod Mkono katika uchaguzi wa mwaka 2015,Musoma Vijijini.

Wachangiaji wengi katika ule uzi walijikuta wanatoka katika mada kuu na kuanza kumjadili Ndugu Mbura kama ni Engineer ama sio.
Kwa heshima na Taadhima tunapenda kutumia fursa hii kutoa ufafanuzi wa Elimu ya Kamanda Mbura Chiragwile.

Kwanza ifahamike kuwa Engineering ni moja kati ya fani Mbali mbali zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Dar E Salaam ukiacha Sheria,Ualimu,Uhasibu,Uchumi etl.

Wengine wakaenda mbali na kusema Mbura hakuwa hata na Vigezo vya kudahiliwa katika Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (Coet) kwa mwaka wake wa udahili.

Nipende kutoa CV fupi ya Bwana Mbura Chiragwile.

Ni kweli Bwana Mbura hakusoma Engineering,Bwana Mbuna alisoma Bsc in Electronics Science and Communications kutoka katika enzi hizo kijulikanacho kama FIVE (Faculty of Informatics and Virtue Education),University of Dar Es Salaam kwa Miaka mi 3

Bwana Mbura amefanya kazi na Makampuni makubwa kabisa ya Mawasiliano Ulimwenguni,Huawei Techonologies na Nokia Networks,pia Bwana Mbura ameshawahi kufanya kazi Zantel,Nothern Engineering na Soft Link International.

Pia Bwana Mbura ni Diwani kupitia ticket ya CHADEMA Pale Kigoma Mjini.

Bwana Mbura alimaliza kidato cha nne kutoka shule ya Ufundi Tanga na kupata Division one kali tu.

Bwana Mbura alichaguliwa kuendelea na Masomo yake ya kidato cha tano katika shule ya wanafunzi wenye Vipaji Pekee ki akili ya Ilboru,Arusha,akisoma Masomo ya Pizikia,Kemia na Hisabati (PCM) na kufanikiwa kupata one kali tu ya point 5,akijipatia Daraja A katika somo la Hisabati na Daraja B katika Masomo ya Kemia na Fizikia.

Kwa Muktadha huu,Ndugu Mbura angeweza na alikuwa ana qualifications za kusoma chuo chochote kile na Course yoyote ile hapa Tanzania na Ulimwenguni kwa ujumla,kusema kuwa hakuwa na Qualifications za kusoma Engineering,i.e Bsc in Computer Engineering &IT ama Bsc Telecommunications Engineering ni Uzuzu uliopita mipaka.

Natumai kwa Maelezo haya,mtakuwa mmemuelewa ndugu Mbura kwa undani Kabisa.

Tanzania inahitaji vijana wasomi kama Mbura kuingia Bungeni na Serikalini kwa ujumla.

Tumpe Support Ndugu Mbura aweze kutimiza ndoto zake za kuwatumikiwa wa Tanzania nje ya ulingo wa Teknolojia ambayo imetamalaki Kichwani mwake
 
Kila la kheri kwa Kamanda na tunashukuru kwa ufafanuzi ila unapojibu hoja jaribu kutumia lugha inayoepuka matusi.
 
Hakuna tusi hapo naona dawa itawaingia walewaliokuwa wanajilinganisha na kubeza elimu ya huyu ndugu. Huyu ndugu amaweza kufanya vizuri maana hajawahi kufanya kazi kwenye hii corrupt government ya wadanganyika.
 
Pamoja mkuu.Mbura mwanangu sana nilikuwa nae sana huko ktk telecom job
 
Safi sana kamanda kila heri ingawaje huyo mzee wa loans board inahitajika strategics kumng'oa.
 
Huyu mshkaji nakumbuka nilikua kwenye team yake ya urais daruso kumbe k ni kamanda mwenzetu mchagueni.
 
Aaah Mr. President... I used to know him by that name kwa sabb nilijua one day atakuwa president wa hii nchi,

Naona unasadikisha dream yako maan!
Kila la kheri my class mate, u r very capable.
 
Afterall what Is in a name?! Bora hâta Kamanda Chiragwile ana technical knowledge background, sijui matomaso wana lipi la kusema kuhusu hawa madokta of nothing, maprofesa without training wanaoibuka asubuhi na jioni kila kukicha?! Go go Chiragwile, maCCM tumewashika pabaya, wamebakia kuweka mapingamizi, hoja NIL. UKAWA UNAONGOZA CCM INATAWALA; Freedom Is comming 2morrow, Aluta Continua.
 
Mshkaji Yuki vizur nakumbuka wakati Niko nae job waajiri hawatamsahau pale walipopindisha sheria ss akina hoya ndiyo alikuwawa mtetezi wetu Northern Engineering wanamfahamu vizuri kutokana na sheria zao kandamizi za kazi
 
Nakumbuka alikuwa diwani wa kwanza kuwa na ofisi ya diwani Manispaa ya Kigoma ujiji. Alifungua ofisi akaweka secretary na mtu ukiwa na shida naye alikuwa anapatikana pale kila jioni baada ya mihangaiko ya kazi zake binafsi.

Sijui kama ile ofisi bado ipo sijapita muda mrefu kidogo ngoja nitapita siku moja nimtie moyo aendelee na moyo huo huo sisi wanaKigoma tulimkubari sana japo sio mtu wa huku tulimuamini tukampa dhamana Musoma mtashindwa nini?
 
Hongera sana Kamanda CDM imekupa dhamana sasa itendee kazi
 
Nimrodi Mkono hagombei jumbo la Musoma vijijini Bali jimbo la Butiama!
 
Back
Top Bottom