Ufafanuzi: Ada Elimumsingi

Marumeso

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,410
1,322
Wadau shule zitafunguliwa siku si nyingi zijazo. Kumekuwa na kauli nyingi za kuchanganya kuhusu ada na michango ya shule za msingi na sekondari hasa kwa shule binafsi.

Je msimamo ukoje? ada itakuwa ileile 380,000 km ilivyotangazwa au tusubiri shule zitoe list mpya ya ada?
 
Subiri kwanza.

Ni kweli wanasema subira yavuta kheri lakini ilipaswa hadi sasa wazazi wajue watalipa nini kwa sababu wamiliki wa shule waligomea ada iliyotajwa na serikali na mbaya zaidi kwa sasa msisitizo umekuwa ni kwa shule za serikali tu
 
JPM na serikali yake waliufyata baada ya kupigwa mkwara na wamiliki wa shule binafsi. Walitishia kutofungua shule zao... JPM na serikali yake kimyaaaa!!! Waliahidi kutoa waraka mpya wa ada elekezi tarehe 15/12/2015 kimyaaa!! Chezea mabepari wewe,!!!?
 
Hakuna cha mabepari wala majamaa. Acheni wenye uwezo wasomeshe watoto wao wanakotaka.Lile suala la biashara huria limeisha?Kama priorities zako ni kulewa na starehe zingine,usinyime nafasi wenye priorities za maendeleo ya family zao.
 
Ada za shule binafsi hazitaguswa kamwe kwa sababu (1) wengi ya wamiliki wake ni viongozi na watumish serikalini (2) ukimya wa watz; watz hatuna kawaida ya kuungana (umoja) hasa ktk masuala ya msingi yanayotuathiri kwa pamoja. Utashangaa nyie mnagomea kitu fulani wanakuja wenzetu wanakubali kiulaini.
 
Wadau shule zitafunguliwa siku si nyingi zijazo. Kumekuwa na kauli nyingi za kuchanganya kuhusu ada na michango ya shule za msingi na sekondari hasa kwa shule binafsi.

Je msimamo ukoje? ada itakuwa ileile 380,000 km ilivyotangazwa au tusubiri shule zitoe list mpya ya ada?

Ada na michango yote ya shule huambatanishwa kwenye Ripoti ya Maendeleo ya mwanafunzi.Nilipowafuata wanangu baada ya kufunga shule,nilikabidhiwa bahasha zenye Ripoti kamili ya Maendeleo yao pamoja na michango na ada ya muhula mpya ambao utaanza 4/1/2016.

Kwa kuwa ni jukumu langu kuwapatia wanangu Elimu bora bila kusita nililipa ada 2/12/2015 kupitia akaunti ya shule.Wewe msubiri Magufuli akupe mwongozo wa hatima ya watoto wako utadhani ulimshirikisha wakati wa kuzaliwa kwao.
 
Back
Top Bottom