Ndugu zangu Watanzania maoni yenu wengi nimeyaona, kila mtu amejaribu kutoa lake la moyoni kuhusiana na UNABII ninaosimamia. Na nimeona nitoe ufafanunuzi vizuri kwa faida yenu na wengine ambao hawawezi kutoa maoni na kwa faida ya taifa na dunia wanaosubiri MAKUSUDI MAKUU YA MUNGU YATENDEKE HAPA DUNIANI KWENYE KIPINDI HIKI.
Tokea Adamu na Hawa walipomuasi Mungu; Mungu ameingilia makusudi yake makuu moja kwa moja hapa duniani marambili.
1. Ni kisa cha GHARIKA YA WAKATI WA NUHU ambapoNuhu Mungu alimuandaa kusimamia tukio hilo,
2. na KISA chapili ni UKOMBOZI WA WANA WA ISRAELI KUTOKA MISRI CHINI YA UONGOZI WA MUSA, Ambapo Mungu alimwandaa nabii Musa kusimamia zoezi hilo.
3. Kwa sasa tena ameniandaa mimi tokea nilipozaliwa na hasa mafunzo ya kuja kuongoza makusudi ya MUNGU HAPA DUNIANI yalianza 1986. Kwa hiyo ndugu zangu ninachotaka kutimiza ni interception ya 3 au TUKIO KUU LA 3 la MUNGU kufanya makusudi yake moja kwa moja HAPA DUNIANI.
Mungu amenipanga kupitia taifa langu Tanzania, Tanzania itakuwa ikipokea miongozo ya Mungu kupitia mimi na serikali ya Tanzania itaratibu hiyo miongozo na kisha serikali ya Marekani na Uingereza kwapamoja watasimamia utekelezaji wake duniani au katika mataifa yote duniani.
ILA Mungu amepanga hayo makusudi makuu kabla ya kuanza MTU WA KWANZA KUYAJUA NAKUYAFUNGUA NI MH. RAIS JAKAYA KIKWETE ambaye ndiye Rais aliyeko madarakani wakati makusudi hayo yanataka kuanza. Bila ya KUYAFUNGUA hayataanza na ndiyo maana MABALAA yataendelea kulipata taifa letu hadi atambue na akubali kuyasikiliza kwa HIARI au KWA LAZIMA
KWA HI YO NDUGU ZANGU MNA HAKI YA KILA MTU KUSEMA LAKE LAKINI NAWAOMBA SANA LIOMBEENI JAMBO HILI LITENDEKE KWA SABABU NDILO SULUHISHO LA MATATIZO YA BINADAMU YALIYOTUKUMBA CHINI YA UTAWALA WA SHETANI WA MIAKA 6000 ILIYOPITA.
Huko kwenye madawa ya Asili na Teknolojia mlikoniona nilikuwa chini ya mafunzo ya jambo hili linalokuja.
Asanteni.
NABII JKBUBERWA NABII KAMA MUSA (Kumbukumbu 18:18,19)