Uenyekiti wa CCM ni wa kurithishana kifalme

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,896
6,912
UENYEKITI CCM WA KURITHISHANA KIFALME NI DEMOKRASIA?

Kitendawili cha uenyekiti CCM kitaifa kurithishana bila uchaguzi uchaguzi, bali kuachiana madaraka kama urithi wa kifalme kuna haja ya kutathmini upya.

Mazoea hujenga tabia kutokana na kuvunja Katiba.

Hata hivyo inafaa kama kipengere cha Katiba yao kuna mwanya huo, sio utaratibu kidemokrasia.

CCM sasa kumejengeka mfumo usio wa kidemokrasia hata viongozi wengine waandamizi kama:
1. Mwenyekiti CCM Taifa.
2. Makamu mwenyekiti bara na visiwani
3. Katibu Mkuu
4. Naibu katibu mkuu bara na visiwani.

Huwezi kugombea wala kupigiwa kura, isipokuwa ridhaa ya mwenyekiti anavyoona inafaa.

Upatikanaji wa viongozi tajwa hapo juu ni wa mfumo wa kupendeleana kiuteuzi usiofuata mfumo wa kidemokrasia.
 
It was okay until "The other guy" came...

A glimpse ya namna wengi wetu tulivyo wabinafsi, wachache mno wanaojali tu maslahi mapana ya taifa. Alipokuja yule anayeamini chama lazima kiwepo na kifanye yote kwa maslahi tu ya nchi/taifa ghafla sana wapingaji wakawa wengi sana, na katiba ikachambuliwa vyema kwamba hairuhusu kurithishana uongozi, halafu hamna uzoefu wa kuongoza chama. Ilipofanyika kwa wenye uzoefu lakini maslahi ya taifa yakawa on bottom of the list then it was okay???? Weird and ridiculous, Ubinafsi at highest order!!!!
 
"Kwenye uongozi wangu sitaki mtu mwenye kofia mbili".Hapa kazi tu
 
"Ukiona Adui anakusifia rudi nyuma na ujitafakari lakini ukiona anakuponda jua umewatwanga Kisawasawa"- Dr.Pombe Magufuli John
 
Mfumo huu wa ccm wa kubebana bila ushindani wa uchaguzi madhara yake ni kuibuka na kushamiri hali ya kujipendekeza kwa kila njia ili kupata ridhaa ya upendeleo wa uteuzi chamani na serikalini.
 
Ewe Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na nchi, utuangalie kwa jicho la huruma sisi waja wako ili nchi na vyama vyetu vya siasa viongozwe kwa mujibu wa katiba. Amina
 
Kwa hili hawachekani wanapishana style tu na ni karibu vyama vyote. Kuna wanaokabidhiana kwa mazoea yao badala ya uchaguzi, kunawanao washawishi wengine wasigombee au waondoe majina yao, wengine hata mikutano yao huisikii. Mola atusaidie.
 
Back
Top Bottom