Uendeshwaji wa kesi za uchochezi na makosa ya mtandao

ze X

Member
Joined
Apr 27, 2016
Posts
52
Reaction score
43
Leo katika mahakama ya wilaya ya Mbozi, jeshi la polisi liliwapandisha kizimbani vijana watatu, Mdude Nyagali, Aristotle Mgasi na Omary Muba kwa tuhuma za uchochezi na makosa ya mtandao.

Mdude na wenzie walikamatwa na kuwekwa rumande wiki 3 zilizopita, bila kupelekwa mahakamani kwa sababu ambazo hazikutajwa. Jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, sheria no.09 ya mwaka 1985 (The Criminal procedure act, 1985). Sheria hii inamuhitaji mtuhumiwa kukaa mikononi mwa polisi kwa muda usiozidi masaa 24 kabla ya kufikishwa mahakani.

Lakini Polisi wamevunja sheria hii kwa makusudi. Wamewaweka watuhumiwa rumande zaidi ya wiki 3 bila kuwafikisha mahakani. Polisi wamekamata watu wanaodaiwa kuvunja sheria, lakini nao wakavunja sheria nyingine wakati wakitekeleza sheria inayodaiwa kuvunjwa. Paradox.!!

Pili, Mdude na wenzie walipokamatwa wiki 3 zilizopita walisafirishwa hadi Dar na kuwekwa mahabusu ya Oysterbay kwa lengo la kuwaunganisha na vijana wengine waliokamatwa mikoa mingine ili washtakiwe kwa pamoja. Hii ni kinyume na utaratibu uliozoeleka wa mtuhumiwa kushtakiwa katika eneo alilotenda kosa.

Baadhi ya wanaharakati walipiga kelele na kuomba vijana hao warudishwe mikoa waliyodaiwa kufanya makosa ili kesi zao zisikilizwe huko lakini Polisi hawakukubali. Wakashikilia msimamo wao wa kuwashtaki kwa pamoja jijini Dar.

Baadae mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu akaamua kuivalia njuga kesi hiyo. Akajitolea yeye na mawakili wengine wa Chadema kuwatetea vijana wote waliokamatwa. Polisi kusikia Lissu amenunua kesi "wakaweka mpira kwapani". Wakaona Lissu akisimamia kesi hiyo Jamhuri itaangukia pua kabla ya "misa ya kwanza".

Kwahiyo ukaandaliwa utaratibu wa kuwarudisha mikoa waliyokamatiwa ili wakashtakiwe huko. Yani jambo lilelile ambalo wanaharakati waliomba wiki 3 zilizopita polisi wakakataa, leo polisi haohao wamelazimika kulikubali kwa kumuogopa Tundu Lissu. Interesting.!

Kitendo cha Polisi kuweka "mpira kwapani" mapema namna hii, ni kiashiria kwamba wameanza kukata tamaa, na inadhihirisha kuwa wanamuogopa Lissu na mawakili wengine wa Chadema. Hata hivyo Polisi walichosahau ni kwamba hata huko mikoani walikowapeleka watuhumiwa kuna mawakili makini mno, na wasifikiri kesi itakuwa rahisi.

Tatu, ndugu Fanueli Mkisi ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limezuia wananchi kuingia ndani ya chumba cha mahakama leo wakati kesi ikisikilizwa. Sijui kwanini Polisi wamewanyima wananchi haki yao ya kisheria ya kufuatilia mwenendo wa kesi hii. Si sahihi polisi kuzuia wananchi kusikiliza kesi inayohusu watoto wao, rafiki zao, ndugu zao unless watuhumiwa wawe wamefanya uhaini (treason) au kosa jingine kubwa litakalolazimisha kesi kuendeshwa "in camera"

Lakini kosa la kuandika facebook mnazuia watu wasiingie mahakamani?? This is not fair. Kwani wamefanya kosa gani hadi kesi iendeshwe "in camera?". Hata kesi za mauaji haziendeshwi "in camera", sasa iweje hii ya kina Mdude ya iwe "in camera"??

Nne, Mdude na wenzie wamenyimwa dhamana kwa madai kuwa Hakimu aliyeachiwa kiti kuendesha kesi hiyo hakuwa na mamlaka ya kutoa dhamana japo dhamana zao zilikua wazi.

Awali kesi hiyo ilikua ikisikilizwa na Hakimu wa mahakama ya wilaya, ambaye aliondoka na kumuachia kiti hakimu wa mahakama ya mwanzo. Hakimu huyo wa mahakama ya mwanzo alisema dhamana za kina Mdude zipo wazi lakini hawezi kuruhusu watoke kwa sababu yeye hana mamlaka ya kutoa dhamana. Kwahiyo Mdude na wenzie wamerudishwa rumande hadi September 27 kesi yao itakapotajwa tena.

Kwa maoni yangu walichokifanya mahakimu hawa ni hujuma dhidi ya kina Mdude. Kwanini Hakimu wa mahakama ya wilaya aondoke kabla kesi haijaisha na kwanini amuachie kiti hakimu wa mahakama ya mwanzo? Je nikisema walipanga kufanya hivyo ili kuwanyima dhamana vijana hao nitakua nimekosea?

Lakini je ni kweli Hakimu wa mahakama ya mwanzo hawezi kutoa dhamana akikalia kiti cha hakimu mkazi wa wilaya? Sheria inasemaje? Sheria inayohusu mamlaka za mahakama no.141 ya mwaka 1979 (The appellate jurisdiction act, 1979), inaeleza mamlaka za kisheria (jurisdiction) kwa kila mahakama nchini.

Pamoja na mambo mengine sheria hiyo inatoa mamlaka kwa "taasisi/mahakama" sio "mtu/hakimu". Kwahiyo kitendo cha hakimu wa mahakama ya mwanzo kupewa kiti cha hakimu mkazi kwa muda it means alipewa pia mamlaka ya hakimu mkazi. Kwahiyo hakimu hakua na sababu ya kujitetea kuwa eti "hana mamlaka" ya kutoa dhamana, unless kama kesi hiyo ingeanzia mahakama ya mwanzo ndio hoja yake ingekua valid.

Lakini kama alipewa nafasi ya kukaimu kiti cha District Magistrate basi alipewa pia "savoir faire" ya kuexercise jurisdiction ya District Magistrate court. Kwahiyo hakua na sababu yoyote ya kusema hana mamlaka. Utetezi wa hakimu huyu ni batili na haramu. Yani kabla hata hajafikiria kuutoa tayari ulikua batili (null and void ab initio). Hizi ni hujuma zinazoendelea kufanywa na dola dhidi ya demokrasia na utawala wa sheria nchini.

All in all tuzidi kuwaombea kina Mdude na mawakili wanaowatetea ili MUNGU awape nguvu na maarifa ya kupigania haki, demokrasia na utawala wa sheria bila kuogopa lolote. The battle is not yet over.

Malisa GJ.!
 
Asante sana mkuu , juzi Bageni amehukumiwa kunyongwa hadi kufa , japo alikuwa kiongozi wa polisi , hii inatosha kuwa alert polisi kwamba kutumika haiwezi kuwa kinga yao .
 
By Malisa GJ,

.....Lakini kama alipewa nafasi ya kukaimu kiti cha District Magistrate basi alipewa pia "savoir faire" ya kuexercise jurisdiction ya District Magistrate court. Kwahiyo hakua na sababu yoyote ya kusema hana mamlaka. Utetezi wa hakimu huyu ni batili na haramu. Yani kabla hata hajafikiria kuutoa tayari ulikua batili (null and void ab initio). Hizi ni hujuma zinazoendelea kufanywa na dola dhidi ya demokrasia na utawala wa sheria nchini......
Malisa GJ.!
Eti, nyie watalaamu wa sheria, hapa hakuna viashiria vya kuenda kinyume na ethics/miiko ya uhakimu kweli?
Kama ni ndio, nadhani inawezekana kuwashughulikia wahusika kwa kutumia sheria hiyohiyo wanayoichezea.....
Kama ni kweli, itakuwa ni aibu kubwa mnoo kwa mwanasheria "msomi" kuendeshwa na polisi!
Kama ni kweli wamefanya haya mambo kwa makusudi, Wahusika chukuweni hatua kuwa-adabisha hawa mahakimu waliokengeuka.
 
Matukio kama haya yawe documented na kuripotiwa kunakohusika kwa ushahidi hakuna anayejua kesho
 
By Malisa GJ,

Leo katika mahakama ya wilaya ya Mbozi, jeshi la polisi liliwapandisha kizimbani vijana watatu, Mdude Nyagali, Aristotle Mgasi na Omary Muba kwa tuhuma za uchochezi na makosa ya mtandao.

Mdude na wenzie walikamatwa na kuwekwa rumande wiki 3 zilizopita, bila kupelekwa mahakamani kwa sababu ambazo hazikutajwa. Jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, sheria no.09 ya mwaka 1985 (The Criminal procedure act, 1985). Sheria hii inamuhitaji mtuhumiwa kukaa mikononi mwa polisi kwa muda usiozidi masaa 24 kabla ya kufikishwa mahakani.

Lakini Polisi wamevunja sheria hii kwa makusudi. Wamewaweka watuhumiwa rumande zaidi ya wiki 3 bila kuwafikisha mahakani. Polisi wamekamata watu wanaodaiwa kuvunja sheria, lakini nao wakavunja sheria nyingine wakati wakitekeleza sheria inayodaiwa kuvunjwa. Paradox.!!

Pili, Mdude na wenzie walipokamatwa wiki 3 zilizopita walisafirishwa hadi Dar na kuwekwa mahabusu ya Oysterbay kwa lengo la kuwaunganisha na vijana wengine waliokamatwa mikoa mingine ili washtakiwe kwa pamoja. Hii ni kinyume na utaratibu uliozoeleka wa mtuhumiwa kushtakiwa katika eneo alilotenda kosa.

Baadhi ya wanaharakati walipiga kelele na kuomba vijana hao warudishwe mikoa waliyodaiwa kufanya makosa ili kesi zao zisikilizwe huko lakini Polisi hawakukubali. Wakashikilia msimamo wao wa kuwashtaki kwa pamoja jijini Dar.

Baadae mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu akaamua kuivalia njuga kesi hiyo. Akajitolea yeye na mawakili wengine wa Chadema kuwatetea vijana wote waliokamatwa. Polisi kusikia Lissu amenunua kesi "wakaweka mpira kwapani". Wakaona Lissu akisimamia kesi hiyo Jamhuri itaangukia pua kabla ya "misa ya kwanza".

Kwahiyo ukaandaliwa utaratibu wa kuwarudisha mikoa waliyokamatiwa ili wakashtakiwe huko. Yani jambo lilelile ambalo wanaharakati waliomba wiki 3 zilizopita polisi wakakataa, leo polisi haohao wamelazimika kulikubali kwa kumuogopa Tundu Lissu. Interesting.!

Kitendo cha Polisi kuweka "mpira kwapani" mapema namna hii, ni kiashiria kwamba wameanza kukata tamaa, na inadhihirisha kuwa wanamuogopa Lissu na mawakili wengine wa Chadema. Hata hivyo Polisi walichosahau ni kwamba hata huko mikoani walikowapeleka watuhumiwa kuna mawakili makini mno, na wasifikiri kesi itakuwa rahisi.

Tatu, ndugu Fanueli Mkisi ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limezuia wananchi kuingia ndani ya chumba cha mahakama leo wakati kesi ikisikilizwa. Sijui kwanini Polisi wamewanyima wananchi haki yao ya kisheria ya kufuatilia mwenendo wa kesi hii. Si sahihi polisi kuzuia wananchi kusikiliza kesi inayohusu watoto wao, rafiki zao, ndugu zao unless watuhumiwa wawe wamefanya uhaini (treason) au kosa jingine kubwa litakalolazimisha kesi kuendeshwa "in camera"

Lakini kosa la kuandika facebook mnazuia watu wasiingie mahakamani?? This is not fair. Kwani wamefanya kosa gani hadi kesi iendeshwe "in camera?". Hata kesi za mauaji haziendeshwi "in camera", sasa iweje hii ya kina Mdude ya iwe "in camera"??

Nne, Mdude na wenzie wamenyimwa dhamana kwa madai kuwa Hakimu aliyeachiwa kiti kuendesha kesi hiyo hakuwa na mamlaka ya kutoa dhamana japo dhamana zao zilikua wazi.

Awali kesi hiyo ilikua ikisikilizwa na Hakimu wa mahakama ya wilaya, ambaye aliondoka na kumuachia kiti hakimu wa mahakama ya mwanzo. Hakimu huyo wa mahakama ya mwanzo alisema dhamana za kina Mdude zipo wazi lakini hawezi kuruhusu watoke kwa sababu yeye hana mamlaka ya kutoa dhamana. Kwahiyo Mdude na wenzie wamerudishwa rumande hadi September 27 kesi yao itakapotajwa tena.

Kwa maoni yangu walichokifanya mahakimu hawa ni hujuma dhidi ya kina Mdude. Kwanini Hakimu wa mahakama ya wilaya aondoke kabla kesi haijaisha na kwanini amuachie kiti hakimu wa mahakama ya mwanzo? Je nikisema walipanga kufanya hivyo ili kuwanyima dhamana vijana hao nitakua nimekosea?

Lakini je ni kweli Hakimu wa mahakama ya mwanzo hawezi kutoa dhamana akikalia kiti cha hakimu mkazi wa wilaya? Sheria inasemaje? Sheria inayohusu mamlaka za mahakama no.141 ya mwaka 1979 (The appellate jurisdiction act, 1979), inaeleza mamlaka za kisheria (jurisdiction) kwa kila mahakama nchini.

Pamoja na mambo mengine sheria hiyo inatoa mamlaka kwa "taasisi/mahakama" sio "mtu/hakimu". Kwahiyo kitendo cha hakimu wa mahakama ya mwanzo kupewa kiti cha hakimu mkazi kwa muda it means alipewa pia mamlaka ya hakimu mkazi. Kwahiyo hakimu hakua na sababu ya kujitetea kuwa eti "hana mamlaka" ya kutoa dhamana, unless kama kesi hiyo ingeanzia mahakama ya mwanzo ndio hoja yake ingekua valid.

Lakini kama alipewa nafasi ya kukaimu kiti cha District Magistrate basi alipewa pia "savoir faire" ya kuexercise jurisdiction ya District Magistrate court. Kwahiyo hakua na sababu yoyote ya kusema hana mamlaka. Utetezi wa hakimu huyu ni batili na haramu. Yani kabla hata hajafikiria kuutoa tayari ulikua batili (null and void ab initio). Hizi ni hujuma zinazoendelea kufanywa na dola dhidi ya demokrasia na utawala wa sheria nchini.

All in all tuzidi kuwaombea kina Mdude na mawakili wanaowatetea ili MUNGU awape nguvu na maarifa ya kupigania haki, demokrasia na utawala wa sheria bila kuogopa lolote. The battle is not yet over.

Malisa GJ.!
Demokrasi ikivuka mpaka huwa ina hasara yake kutumia mitandao vibaya huwa ina madhara yake. Kwa mfano visu huwa vinatengenezwa kwa matumizi yetu ya nyumbani ya kila siku lakini kwa wakati huo huo kuna watu ama mtu anatumia kwa njia isiyofaa (kumchoma mwenzake) sasa ndio unaona hasara ya kisu. Matusi na lugha isiyofaa katika mitandao pia ni hatari sana Serikali isipochukua hatua za haraka kuzuia hali hii nchi itatumbukia katika wimbi la vijana kukosa adabu kwa viongozi halafu na wazazi wao.
Tutumie mitandao vizuri kwa ajili ya kukosoana kwa yaliokuwa ya kweli na kutoa ushauri na maoni mazuri.
 
Hakika yake mwenye haki itamwokoa. Bali yeye afanyaye fitina atanaswa katika hila zake.
 
Kwa muendelezo huu wa kamatakamata na kuzuia dhamana za watuhumiwa, na hakuna sauti inayosikilizwa ya kutetea haki hiyo ya kusema, nafikiria kufunga acc yangu ya JF.
 
Demokrasi ikivuka mpaka huwa ina hasara yake kutumia mitandao vibaya huwa ina madhara yake. Kwa mfano visu huwa vinatengenezwa kwa matumizi yetu ya nyumbani ya kila siku lakini kwa wakati huo huo kuna watu ama mtu anatumia kwa njia isiyofaa (kumchoma mwenzake) sasa ndio unaona hasara ya kisu. Matusi na lugha isiyofaa katika mitandao pia ni hatari sana Serikali isipochukua hatua za haraka kuzuia hali hii nchi itatumbukia katika wimbi la vijana kukosa adabu kwa viongozi halafu na wazazi wao.
Tutumie mitandao vizuri kwa ajili ya kukosoana kwa yaliokuwa ya kweli na kutoa ushauri na maoni mazuri.

Define matusi/tusi
 
mkuu,siri-kali imelewa utawala,imesha sahau hayo mamlaka ya kiutawala ilipewa na nani..muda utatupatia majibu sahihi sana.
 
Demokrasi ikivuka mpaka huwa ina hasara yake kutumia mitandao vibaya huwa ina madhara yake. Kwa mfano visu huwa vinatengenezwa kwa matumizi yetu ya nyumbani ya kila siku lakini kwa wakati huo huo kuna watu ama mtu anatumia kwa njia isiyofaa (kumchoma mwenzake) sasa ndio unaona hasara ya kisu. Matusi na lugha isiyofaa katika mitandao pia ni hatari sana Serikali isipochukua hatua za haraka kuzuia hali hii nchi itatumbukia katika wimbi la vijana kukosa adabu kwa viongozi halafu na wazazi wao.
Tutumie mitandao vizuri kwa ajili ya kukosoana kwa yaliokuwa ya kweli na kutoa ushauri na maoni mazuri.

Irrelevant!!

Naona wewe hukusoma na kuelewa kilicholetwa na mleta mada.

Mleta hoja anaoengelea jinsi kesi inavyoendeshwa "kimizengwe", wewe unaleta ishu kutumia kisu kinyume na matumizi yake!

Kesi tayari iko mahakamani wewe na hapo ndipo patakapoamuliwa kama kisu kimetumika sawa sawa na malengo ya matumizi yake au vinginevyo.

Itoshe kusema kuwa, wewe ndiye unayeona hivyo (wametumia vibaya kisu/mitandao). Tusubiri sasa wahusika watakavyojitetea na mwisho maamuzi ya mahakama ndiyo tutakuwa na guts za kusema wametumia kisu kinyume na matumizi yake!!
 
Demokrasi ikivuka mpaka huwa ina hasara yake kutumia mitandao vibaya huwa ina madhara yake. Kwa mfano visu huwa vinatengenezwa kwa matumizi yetu ya nyumbani ya kila siku lakini kwa wakati huo huo kuna watu ama mtu anatumia kwa njia isiyofaa (kumchoma mwenzake) sasa ndio unaona hasara ya kisu. Matusi na lugha isiyofaa katika mitandao pia ni hatari sana Serikali isipochukua hatua za haraka kuzuia hali hii nchi itatumbukia katika wimbi la vijana kukosa adabu kwa viongozi halafu na wazazi wao.
Tutumie mitandao vizuri kwa ajili ya kukosoana kwa yaliokuwa ya kweli na kutoa ushauri na maoni mazuri.
Mbona kiongozi mkuu anatoa lugha ya matusi hamsemi? AU yeye ameishatoka kwenye level ya ubinadamu tayari ameishakuwa Mungu wa Watanzania hivyo hapaswi kusemwa anapotoa lugha yenye ukakasi? Huyu naye arekebishe matamushi yake. Hata wasio viongozi wana feelings na wanapozihakiwa wanaumia ndo maana kwa vile hawawezi kutokea hadharani kujibu kejeri walizofanyiwa na watawala basi uamua kutumia mitandao kufikisha ujumbe wao.
 
Back
Top Bottom