Habari Mkuu,Kama upo Simu2000,Panda magari yaendayo msasani waambie wakushushe kituo kinaitwa UBALOZI,Ukishashuka utaona Pikipiki hapo kama mfuko upo vizuri ni Jero au Buku mpaka TMJ maana ni 400m tu,Kama unaweza kutembea muulize mtu yeyote hapo Shoppers Plaza au May Fair Plazer ipo wapi? Watakwambia Nyoosha hiyo barabara ya kwenda Kawe moja kwa moja utaona Shopping Malls ya upande wa kushoto ni Shoppers na ya kulia ni May Fair,ukishafika karibu na hizo Malls uliza Mtu yeyote hapo TMJ ipo wapi? Atakuonyesha Jengo hilo Hapo Mbele yako.