Nafikiri "kushindwa" kwa UDSM kutoa orodha za waliochaguliwa (multiple na single selection) ni kielelezo "kizuri" cha mfumo huu kushindwa. Na Bahati mbaya hadi sasa TCU wako kimya wakijua kwenye tangazo lao wamesema wenye multiple selections wa=confirm kabla ya tarehe 5/9/2018.
Nasikia kuna vyuo navyo vimeanza kuwa pigia wanafunzi simu kuhakikisha wana confirm kwao sijui kutumia nini nje ya utaratibu uliyo wekwa, hii yote inatokana na mfumo huu kushindwa kufanya kazi kwa sababu ambazo hatuja ambiwa.
Mwaka ule walipotoa CAS tulisema MULTIPLE SELECTIONS ndiyo kiama cha mfumo huu wa wanafunzi kuomba vyuoni moja kwa moja. TCU itabidi walitafakari hili wakishirikiana na vyuo. Lakini kwa sasa watoe tamko kusogeza mwisho wa round hii mbele na kuomba radhi kwa wadau (kama uungwana unavyo hitaji).
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.