chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,400
- 24,979
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ujasiriamali na Ubunifu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udiec), Abraham Temu amesema wanafunzi wote watakaojiunga na chuo hicho mwaka wa masomo wa 2017/18 watasoma kozi ya ubunifu na ujasiriamali.
Amesema hatua hiyo inalenga kutatua changamoto ya mitalaa inayowafanya wahitimu kusubirikuajiriwa na Serikali badala ya kujiajiri.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa amesema tatizo linalosababishawanafunzi kuendelea kuwa tegemezi wa ajira ni mitalaa ya zamani ambayo haijafanyiwa marekebisho, hivyo wengi wamekuwa wakisoma na kutegemea Serikali iwape ajira.“Miaka 20 iliyopita wahitimu wa vyuo walikuwa wakipata ajira, lakini hali sasa imebadilika, hivyo tunawataka kubadilika na muwe chanzo cha kuajiri watu ili kufuta fikra za zamani za kusubiri kuajiriwa,” amesema Issa alipofungua Jukwaa la Ujasiriamali la Wanafunzi (Duef)katika chuo hicho.
Ametoa wito kwa wanafunzi wa UDSM kuwa wabunifu ili kuleta matokeo chanya kwao na kwa maendeleo ya Taifa.
Temu amesema Udiec husaidia kuboresha mawazo ya ubunifu na ujasiriamali kutoka kwa wanafunzi ili waweze kupata mitaji itakayowawezesha kutimiza ndoto zao.“Tunakusanya mawazo na kuyaangalia ili kuwapa mbinu mbadala ya kufanikiwa, tunaamini wanafunzi hawa watafika mbali,” alisema Temu.
Chanzo: Mwananchi Online