UDSM ianzishe course ya Postgraduate in Medical law

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,394
4,748
UDSM chuo changu cha zamani ni wakati muafaka wa kuanzisha course ya medical law au medical ethics ...

Natambua uzoefu wa UDSM katika tasnia ya sheria ...

Pia natambua uhitaji mkubwa wa wataalamu wa aina hii hapa nchini,kwani kumekuwepo visanga vingi vinavyohusiana na huduma za afya nchini.

Tumeshuhudia wataalamu wa afya wakilalamikiwa sana na wananchi kuhusu maswala kadhaa ambayo baadhi ni ya kweli na baadhi ni ya kimfumo na baadhi sio ya kweli.

Kesi za aina hii huishia hewani hewani kwa kuwa kuna mvutano wa taaluma mbili yaani sheria na tiba!

Ili kuondoa mikanganyiko hii na mingine mingi inayotarajiwa kujitokeza ni vyema tukapata wataalamu wa tasnia ya sheria ya tiba na wataalamu hawa lazima wawe na taaluma iliyounganishwa.

Hii pia ni fursa ya kiajira nchini na nchi za majirani wetu.

HUU NI USHAURI TU!
 
Back
Top Bottom